NANI WA KUTUSEMEA KAMA WANAHARAKATI WA HAKI ZA WATOTO MKO KIMYA

Tukiwa bado na majonzi ya kuondokewa na Nguli wa tasnia ya Filam hapa Tanzania Steven Kanumba kuna vitu ambavyo kama watanzania ili vizazi vya baadae visitushutumu kwa maamuzi yetu tunapaswa kuvifanya.

Ni ukweli usiopingika kuwa kuzungumzia scenario ya kifo chenyewe hadharani ni aibu ili kumtunzia heshima marehemu kama alikuwa mtu wa watu na sisi kama wazazi tunapaswa kujuwa hilo. Tunaweza vipi kumuita shujaa kwa kitendo chake cha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto mdogo?

Kwanini serikali wameshindwa kuliona hilo?. Viongozi wote wamejirundika huko, je ni kweli wana moyo wadhati wa kumkomboa mwanamke na mtoto wa Tanzania? Tunu ya milioni kumi iliyopewa familia ya

marehemu ni shukrani ya vitendo hivi vya kidhalimu? Ama kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watoto siyo
kosa, basi akina babu Seha wanafanya nini gerezani?

Wako wapi Child protection agencies and women rights? Hoja nyingine mtoto huyu mdogo aliweza vipi kupewa leseni ya kuendesha gari? au ni huyo Kigogo anayetajwa kuwa nae ana uhusiano nae kimapenzi ndiye aliyefanikisha hilo?

Wanahabari Tunapaswa kumchukulia Elizabeth Michael (Lulu) kutokana na Umri wake. Wote tunajuwa namna ya kumhoji na kumlinda mtoto. Pili hatupaswi kumhukumu huyu mtoto. Au kuweka hitimisho la kuwa ni muhusika mkuu. Kimsingi Lulu hakuwa na sababu (motive) ya kumuua marehemu.

Tuwe wawazi, je ni nani anapaswa kupata bad publicity kati yake na marehemu kwa kosa la kutembea na mtoto mdogo? Je alikuwa anafanya nini na mtoto wa miaka 17, tena imeripotiwa alikuwa anataka wotoke waende kwenye vilabu vya pombe usiku.

Pili kwanini tunashindwa kumtaja huyo Kigogo mwingine ambaye alipiga simu na Lulu kuthibitisha kuwa nae ni mpenzi wake? Sina hakika kama huyu mtoto yuko sawa mentally na statement anazotoa. kumbukwe mambo yaliyomtokea ni makubwa kutokana na umri wake. Kwa kutosimamia misingi yetu na weredi tufahamu kuwa Historia itatuhukumu na sisi.

Wale wanaharakati wa haki za watoto wanamsaidia vipi? Huyu mtoto ni kweli hayupo kwenye shock? Hivi ana akili zake timamu za kuweza kuongea?

Huko mahabusu amepata msaada kutoka kwa Child protection agencies? Je wakati anahojiwa alikuwa na psychiatrist ambaye alipaswa kuhakikisha polisi hawampi pressure kutoa majibu wanayoyataka wao?

Ningeomba katika kipindi hiki kigumu tutajiwe huyo kigogo? Tujue nani alihusika kumpa Lulu leseni ya kuendesha gari? Vilevile tufahamu serikali imetumia vigezo gani kutoa tunu ya milioni kumi kama rambirambi?

Image

MUSTAFA MKULO ASHINDWA KUELEZA FAIDA ZA UBINAFSISHAJI

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Juberi Kabwe aliuliza swali la nyongeza baada ya Naibu Waziri wa wizara ya Fedha, Peraila Silima, awali kueleza serikali imepata faida kutokana na ubinafsishaji.

“Mheshimiwa Spika, naomba nielezwe ni faida gani zimepatikana kutokana na ubinafishaji. Miaka ya 80 tulikuwa na viwanda 12 vya nguo leo kimebaki kimoja. Iko wapi Mwanza Textile, Mbeya Textile, Sungura Textile.

“Viwanda vya nguo vilivyoanzishwa na waasisi wetu kwa ajili ya kuongeza ajira, lakini sasa havipo, naomba nitajiwe faida za ubinafsishaji,” alisema.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo alisema kuna mengi yaliyofanyika na kumtaka mbunge huyo kumpelekea swali ili amjibu.

Kutokana na jibu hilo, Spika alisimama na kueleza kuwa Waziri Mkulo hajajibu swali na kueleza kuwa Zitto alitaka kutolewa mifano ya mafanikio ya ubinafsishaji.

“Hapana hayo sio majibu. Mheshimiwa Zitto anataka mafanikio hayo kwa mifano,” alisema.

Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa kanuni ya 45(3) swali hilo litarudishwa siku zijazo katika mkutano huo, ili lipatiwe majibu ya uhakika.

“Kwa mujibu wa kanuni hiyo, iwapo Spika hataridhika na majibu, swali litabidi lirudiwe, hivyo swali hili litaletwa tena ili lipatiwe majibu na tutalipa nafasi katika mkutano huu,” alisema.

Katika swali la msingi, Naibu Waziri huyo alisema baada ya ubinafsishaji, mashirika mengi yamefufuliwa na yameleta tija ikiwamo kuongeza na kuimarisha uzalishaji, kuongeza fursa za ajira ndani na nje ya mashirika/viwanda pamoja na kuongeza mapato ya serikali.

Peraila alikuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya, aliyetaka kujua Watanzania wamenufaikaje na ubinafsishaji na serikali inatoa kauli gani juu ya kubadilishwa kwa matumizi ya viwanda vingi tofauti na makubaliano ya mkataba wa kubinafsishwa.

Akijibu swali hilo, alisema hiyo ni changamoto kwa serikali na taifa kwa ujuma. Hata hivyo, alisema serikali imewaruhusu baadhi ya wawekezaji kubadili matumizi ya viwanda pale ambapo mabadiliko yalionekana kuwa na manufaa kwa taifa.

Pamoja na hayo, alisema serikali ni makini kusimamia na kufuatilia viwanda/mashirika yote yaliyobinafsishwa, ili kuona malengo na madhumuni ya ubinafsishaji yanatimizwa ipasavyo.

Image

JENERALI MSTAAFU ERNEST MWITA KYARO AFARIKI DUNIA

Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kyaro (87), alifariki 04/10/2012 saa nne asubuhi akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.

Jenerali Mstaafu Kyaro alikuwa mmoja wa wapiganaji waliomng’oa Idi Amin. Mkuu wa Majeshi wakati huo alikuwa Marehemu Jenerali Abdallah Twalipo na aliyepewa jukumu la kuyaongoza majeshi yetu vitani alikuwa Jenerali David Musuguri.

Katika salamu zake kwa Jenerali Mwamunyange, Rais Kikwete amemwomba Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi kumfikishia salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa familia ya Jenerali Mstaafu Kyaro na kwa makamanda na wapiganaji wote wa majeshi ya ulinzi kwa kumpoteza mdau, mwenzi wao na kiongozi wao.

Alisema, “Nimepokea kwa huzuni nyingi na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kyaro ambaye ameaga dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza, ambako alikuwa amelazwa.

“Nilimfahamu vizuri na nilifanya kazi na Jenerali Kyaro wakati wa enzi ya uhai wake.”

Rais Kikwete aliongeza kuwa hayati Kyaro alikuwa Mtanzania mzalendo wa kuigwa, mwadilifu na mwaminifu kwa taifa lake, mchapakazi hodari na mpiganaji na kamanda wa mfano kwa waliokuwa chini yake