JENERALI MSTAAFU ERNEST MWITA KYARO AFARIKI DUNIA

Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kyaro (87), alifariki 04/10/2012 saa nne asubuhi akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.

Jenerali Mstaafu Kyaro alikuwa mmoja wa wapiganaji waliomng’oa Idi Amin. Mkuu wa Majeshi wakati huo alikuwa Marehemu Jenerali Abdallah Twalipo na aliyepewa jukumu la kuyaongoza majeshi yetu vitani alikuwa Jenerali David Musuguri.

Katika salamu zake kwa Jenerali Mwamunyange, Rais Kikwete amemwomba Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi kumfikishia salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa familia ya Jenerali Mstaafu Kyaro na kwa makamanda na wapiganaji wote wa majeshi ya ulinzi kwa kumpoteza mdau, mwenzi wao na kiongozi wao.

Alisema, “Nimepokea kwa huzuni nyingi na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kyaro ambaye ameaga dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza, ambako alikuwa amelazwa.

“Nilimfahamu vizuri na nilifanya kazi na Jenerali Kyaro wakati wa enzi ya uhai wake.”

Rais Kikwete aliongeza kuwa hayati Kyaro alikuwa Mtanzania mzalendo wa kuigwa, mwadilifu na mwaminifu kwa taifa lake, mchapakazi hodari na mpiganaji na kamanda wa mfano kwa waliokuwa chini yake

Advertisements