KAMATI ZA BUNGE ZA MAHESABU YA SERIKALI ZA MPONGEZA CAG KWA KUTIMIZA WAJIBU WAKE

Image

  • Zitto awataka wabunge kuifanyia kazi ripoti ya CAG.
  • Cheyo ashangazwa na ukuaji wa deni la Taifa.
  • Mrema apendekeza kiundwe kikosi maalumu cha kupambana na mtandao wa wizi ndani ya halmashauri

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametimiza wajibu wake kikatiba kwa kuwasilisha ripoti yake ya matumizi ya fedha za serikali na sasa ni kazi ya wabunge kuhakikisha Bunge linatoka na maazimio juu ya ripoti hiyo.

Mbali na Zitto, kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), John Cheyo alionyesha kushangazwa na kuendelea kukua kwa deni la taifa wakati miradi mingi nchini haina fedha.

“Deni la taifa linatupa matatizo sisi wote hapa kwa sababu mimi sielewi maana tunakopa, lakini miradi yetu haina pesa hapa kuna kitendawili,”alisema Cheyo na kusema Bunge itabidi lijadili na kutegua kitendawili hicho.

Akizungumzia ufisadi huo mara baada ya taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Augustino Mrema, alisema bado CAG ana kibarua kigumu kutokana na kuwepo mtandao wa mafisadi ndani ya halmashauri.

“Kwa ripoti hii ya CAG nchi inadidimia, nchi inasambaratika ni kama tunafanya mchezo wa kuigiza mimi napendekeza kiundwe kikosi kazi maalumu cha kupambana na mtandao wa wizi ndani ya halmashauri nyingi nchini,” alisema Mrema

Alisisitiza kuwa nchi imezidiwa nguvu na wezi na mafisadi ndani ya halmashauri, ambao wamejipanga kila kona kutekeleza wizi wao kwa kuwa haiwezekani kila mwaka kuwepo ripoti za ubadhirifu wa mabilioni. 

Advertisements