MAWAZIRI 8 WASHINIKIZWA KUMWANDIKIA JK BARUA ZA KUJIUZULU KUIOKOA SERIKALI.

  • Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao ambacho kimewashauri mawaziri wanane kujiuzulu.

    Nimkakati wa kuzuia tishio la Bunge kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu.

  • Wenyewe wasema tutaondoka wengi, wahaidi kuelezea uozo wote kwenye barua zao.

MCHAKATO wa kuhanda hoja ya kumng’oa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa utaratibu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani ukiwa tayari kuwasilishwa Jumatatu Aprili 23 umechukuwa sura mpya baada ya Kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika Aprili 20 usiku kufanya maamuzi ya kuwashinikiza mawaziri 8 kung’oka.

Awali Aprili 19 usiku, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alitoa wito kwa wabunge wote kujiorodhesha kwa nia ya kupata saini za wabunge 71 ambao wangewasilisha kutimiza matakwa ya kisheria kupata asilimia 20 ya wabunge kwa ajili ya kumuondoa Waziri Mkuu.

Mawaziri ambao inasadikiwa tayari wamejipinda kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kwa ushauri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuiokoa serikali ya chama hicho isianguke ni pamoja na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Hatua hiyo imeripotiwa kutowapendeza mawaziri hao, na hivyo kuahidi kuonyesa kwenye barua zao za kujiuzulu kwa Rais Kikwete uozo wote uliosababisha kusakamwa kwao, baadhi wakidai kwamba hawahusiki kwa lolote na mambo wanayo tuhumiwa.

Advertisements

4 thoughts on “MAWAZIRI 8 WASHINIKIZWA KUMWANDIKIA JK BARUA ZA KUJIUZULU KUIOKOA SERIKALI.

  1. nadhani idadi haitoshi,wengi wao hatuna imani nao.wangevunja serekali yoote waanze upya na watu tofauti.hawa woote lao moja.

  2. Ernest, lengo lao siyo awajaridhishwa na utendaji wao bali ni kuonyesha umma wa watanzania kuwa wanajari na wamechukuwa hatua. wanaogopa kula ya kutokuwa na imani inaweza kuingusha serikali yao, Upo hapo Kiongozi.

Comments are closed.