NINA SHAKA NA MPANGO WA KODI WA RAIS OBAMA – BUSH

·Asema utadumaza uchumi

·Kuandika kitabu juu ya ukuaji wa sekta binafsi.

RAIS wa zamani wa Marekani George W. Bush tarehe 12/04/2012 alipokuwa kizungumzia sera ya Uchumi ya nchi hiyo aliushambulia mpango wa Rais wa sasa Baraka Oboma ingawa alionyesha majuto juu ya hatua ambazo serikali yake ilifanya kuhusu sera ya uchumi wakati wa kipindi chake cha kwanza cha utawala wake.

“Sidhani kama itakuwa vizuri kwa nchi yetu kama tutashiriki kudhoofisha rais wetu na mimi sitaki kufanya hivyo,” alifafanua Bush wakati wa hotuba yake katika kituo cha Taasisi ya Kihistoria ya New York.

Taasisi ya Bush hiko katika mchakato wa kuandika kitabu juu ya jinsi ya kufikia asilimia 4 ya ukuaji wa sekta binafsi. Akizungumza kwa mzaha kama ilivyo kawahida yake alisema wengi wa wakosoaji wake litakuwa jambo la kustua kwasababu hawakutegemea “kama {yeye} anapenda kusoma vitabu isitoshe uamuzi wake wa sasa wa kuandika kitabu.”

Kisha akaugeukia mpango mzima na sera ya uchumi, akionyesha kanuni pana ambayo anaamini ikifuatwa itasaidia kuchochea ukuaji katika sekta binafsi.

“Ni ukweli ulio wazi kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo hulipa kodi katika ngazi ya mtu binafsi, kwa hiyo kama wewe utaongeza kodi kwa wale wanao julikana kama matajiri ufahamu kuwa utakuwa umewaongezea mzigo wale wanaoleta ajira, je ni kweli ungependa kupunguza huwezo wa waajiri,” alisema, pasipo moja kwa moja kukabiliana na hoja za rais wa sasa Bw. Obama. “Kama lengo ni ukuaji wa sekta binafsi, unapaswa kutambua kuwa njia bora ya kufikia ukuaji ni kubakiza mitaji kwa waumbaji kazi.” alibainisha

Advertisements