NIONGEZE KIPATO KWA GARAMA YA NDOA YANGU?

Mwishoni mwa wiki ya Aprili 20, Mimi na Mwandishi mwenzangu wa kike kutoka katika kampuni tofauti ya hapa Arusha tulipata fursa ya kualikwa Nchi jirani katika semina ya siku 3 inayo husiana na mambo na maswala ya uwekezaji katika Afrika ya mashariki.

Wenyeji wetu walituhakikishia kutulipia garama zote za malazi na chakula, ila wakituambia kuwa tunapaswa kujitafutia wenyewe sehemu ambayo tutaona inatufaa lakini walipendekeza tufikia kwenye hoteli mojawapo maarufu Katika jiji la Nairobi.

Baada ya kutoka Airport na kucheki in kwenye hotel ambayo  kiukweli ni nzuri na bei yake kidogo ikawa ipo juu, ila wenyeji wetu walitupa fedha ya kutosha kabisa.

Wakati tunajadiliana jinsi ya kufanya yule mwandishi mwenzangu wa Kike akasema, Kwa nini tusichukue chumba kimoja tuchangie sote hili tuweze kubana matumizi? Nilijua anafanya utani lakini akasisitiza kwamba mwisho wa siku inabidi tupate fedha za ziada kwa hajiri ya matumizi yetu mengine.

Bila kinyongo nikaafiki na kuchukuwa chumba kimoja kilichobakia ambacho kilikuwa na kitanda kimoja. Ile kuingia tu ndani, yule dada akasema anataka kuoga sababu ya uchovu wa safari akajifunga taulo kavua nguo na kuingia bafuni. Hapo kijasho chembamba kikaanza kunitoka na kuwaza ifikapo muda wa kulala itakuwaje? Sababu yeye ni mke wa mtu na mimi ndiyo kwanza nimeingia kwenye mahusiano mapya  nikiwa na lengo la kufunga ndoa.

Nikajiapisha sintofanya chochote na huyu dada kwanza tunaheshimiana sana. Na mimi nikaenda kuoga baada ya yeye kutoka nilivyo rudi nikakuta amevaa nguo tayari. Tukaanza kuongea hapo kwa muda na baada ya kama dakika 45 tukashuka chini kwenda kula chakula cha jioni ‘dinner’ mpaka kwenye saa 5 usiku tukarudi Chumbani.

Kufika tu yule dada kavua nguo zake hii sasa alivua mbele yangu akavaa night dress na kujilaza kivivu kitandani.

Na mimi nikajipa moyo nikabadili nguo nikavaa bukta na kujilaza kitandani. Tukiwa kitandani huku tumejifunika shuka moja tukaanza kuzungumza na kukumbushana matukio tunayo pambana nayo kila siku.

Mara usingizi ukanipitia kushtuka nimemkumbatia nikijua ni mpenzi wangu,  kuangalia na yeye kanikumbatia huku mguu wake ukiwa juu yangu. Kiukweli hali ilikuwa ngumu sana mpaka mapigo ya moyo yalibadilika.

Hapo usingizi ulipotea na nikakosa hata nguvu za kujinasua nikawa nimemkumbatia mpaka asubuhi.

Palipokucha yule dada hakuonyesha mstuko wowote haraka haraka akaingia bafuni katoka na kuvaa suti yake na mimi kwa unyonge nikaelekea bafuni kutoka tukaelekea inapofanyika semina.

Wakati wa semina muda wote najiuliza hii ndio siku ya kwanza kweli nitaweza maliza siku 3 bila kuingiza penzi langu jipya matatani?

Media 2 Solution imefanya editing kwenye kisa hiki kwa sababu ya kulinda tukio halisi lililotokea Thanks.

Advertisements