TARATIBU ZA MAWASILIANO ZA VIONGOZI WA TANZANIA ZIBORESHWE.

Taarifa ya Aprili 22 kutoka katika  Kurugenzi ya mawasiliano na habari ya Ofisi ya Rais Ikulu ilisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa hajakutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumjulisha kile kilichotokea bungeni wiki jana.

Taarifa hii haikueleweka kwa wengi, si mara ya kwanza kwa Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kutoa taarifa ambayo inashindwa kujibu kiu yetu ya maswala ya msingi zaidi ya kutuongezea maswali kama inavyo paswa kuwa.

Kwa mujibu wa taharifa hii inadhihirisha kwamba hakuna mawasiliano ya karibu na ya mara kwa mara baina ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda wakati kwa mujibu wa ibara ya 52(3) na 53 (1) Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa utekelezaji wa maagizo ya Rais anayewajibika kwa Rais.

Pamoja na kutokueleweka kwake tulibaki na maswali ya kujiuliza? Je viongozi hawa wanatumia njia zipi za mawasiliano? Nilazima wakutane hili taarifa ifike? Je kauli hii ina ukweli wowote au ni mbinu mojawapo ya kukwepa uwajibikaji?

Kauli hii inamaana kuu mbili kwetu. Moja ni msukumo mdogo wa utendaji wa Taasisi ya raisi kwa mambo muhimu ya kitaifa. Mbili ni udhaifu wa ofisi ya waziri Mkuu katika kuripoti  masuala ya msingi yanayoikabili nchi yetu.

Hali hii imekuwa ikijirudiarudia katika matukio kadhaa kwenye kipindi cha kati ya mwaka 2008 mpaka 2011; ikiwemo matukio ya kashfa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo.

Aprili 22 Ikulu ilikanusha habari kuwa Rais alikuwa amewasiliana na Waziri Mkuu Pinda kuhusiana na suala la kujiuzulu kwa mawaziri, ikidai kuwa tangu awasili kutoka Brazil, Kikwete alikuwa hajakutana wala kuzungumzia suala hilo na waziri wake.

M2S - C.E.O

Advertisements