MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BARRICK GOLD MINE WAMZUIA MWANAHARAKATI KUTOKA TANZANIA KUHUDHURIA.

Amani Mustafa Mhinda akihutubia wanaharakati nje ya jengo ampako mkutano wa Barrick ulifanyika

Mkutano wa mwaka huu wa Barrick gold mine uliofanyika Toronto Nchini Canada May 3,2012. ulimzuia mwanaharakati wa Haki za binadamu na mwanasheria wa masuala ya Maliasili Amani Mustafa Mhinda, ambaye pia ni Mkurugenzi wa asasi ya kijamii ya HAKIMADINI, inayoshugulika na haki za binadamu katika maeneo ya machimbo ya madini.

Mhinda alikuwa amedhamiria kueleza wahudhuriaji wa Mkutano huo kuhusu umuhimu wa  kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo na jamii zinazoishi katika maeneo ya machimbo, ili ziweze kunufaika na rasilimali ya madini ya Tanzania, pamoja na kulinda na kutetea haki zao, ambayo pia ni agenda kuu ya HAKIMADINI yenye makao yake makuu mjini Arusha.   

Pamoja na kuwa na ajenda hiyo,  Barrick Gold na uongozi wake walimzuia kuingia  katika eneo la mkutano huo.

Akinukuliwa na gazeti moja la kitaifa la Canada liitwalo The Canadian, Mhinda alieleza  uhalali wake wa kuhudhuria mkutano huu huku akinukuu matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na makampuni ya uchimbaji

“Kama shirika lisilo la kiserikali la kitanzania na wananchi wa Tanzania, tunataka kuona mauaji   na uvunjwaji wa haki za binadamu  unaohusishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya Canada yanamalizwa. Niko hapa kumwakilisha watanzania wengi ambao ni wahanga  wa mgodi huu pamoja na Mama Otaigo, aliyefariki mwezi wa nne kwa kunywa maji yenye sumu yaliyopo karibu na Mgodi wa North Mara”. Amani alisema

Mwanaharakati huyo pamoja na wanaharakati wengine wa masuala ya haki za binadamu walinyimwa kuzungumza kuhusu matendo ya kinyanyasaji yanayofanyika kwenye maeneo ya machimbo ya  madini nchini Tanzania katika mkutano  Mkuu wa Mwaka wa Barrick Gold mine.

Hatua hiyo ya kampuni ya Barrick Gold Mine kuwazuia wanaharakati wa Tanzania na  kuwaruhusu wenzao wa nchi kama Papua New Guines na Chile kuliushangaza umati wa waalikwa kwenye mkutano huo.

Mhinda alishutumu hatua iliyochukuliwa na Barick Gold ya kumzuia kuingia katika mkutano huo kama “juhudi za wazi za kuficha uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji na wawekezaji wengine kwa jamii za kitanzania”.

Pamoja na kufungiwa kuingia katika mkutano huo, Amani na wanaharakati wengine walipata nafasi ya kuelezea habari zao kwa maelfu ya watu waliokusanyika nje ya eneo la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Barrick kwa ajili ya kupinga unyanyasaji unaofanywa na kampuni ya Barrick Gold ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji dhahabu duniani, iliyoanzishwa na kusimamiwa na Peter Munk. 

Miongoni mwa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo ni pamoja na Waziri mkuu wa zamani wa Canada. Barick hupata fedha za serikali na misaada ya kidiplomasia. Makao makuu ya barrack yapo Toronto, Canada, wakati  Africa Barrick, ni kampuni ya Uingereza ambayo humilikiwa kwa 70% na Barrick Gold

Advertisements

One thought on “MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BARRICK GOLD MINE WAMZUIA MWANAHARAKATI KUTOKA TANZANIA KUHUDHURIA.

 1. Naamini kuna mengi sana yanayofichwa na hawa wawekezaji kuhusu Tanzania ndiyo maana wamemzuia huyo ndugu kutoka kwenye taifa hili lenye kila kitu lakini likiwa nimoja kati ya mataifa maskini duniani kuingia kwenye mkutano huo.
  Ninaamini ripoti walizokuwa wanatoa kuhusu Tanzania inaweza kuwa nizauongo au uchochezi. Lakini ningependa kujua taarifa hizi alizithibitisha huyo bwana Amani mwenyewe?
  Nafkiri hao wamiliki wahiyo migodi ambao wamepewa kivuli cha uwekezaji wanaagenda za siri kuhusu kazi zao wanavyo zifanya ndiyo maana hawataki wahusika wawepo nakufichua siri hizo.
  Watanzania wameamka, tena nafkiri kiwango cha ujinga wa waziwazi kimepungua sana ndiyo maana wanaogopa kufanya kazi zao kwa uwazi ukweli na uaminifu kutokana na kwamba wamekuwa wakiiba sana na watendaji wabovu wa serikali kuwafumbia macho.
  Naomba ndugu wa M2S mthibitishe habari hizi kwahuyo bwana Amani halafu pia tuweze kujua maoni yake na hatua atakayoichukua baada ya mambo hayo kumpata wakati akiwa anawawakilisha watanzania wanyonge.
  Mungu awabariki.

Comments are closed.