VODACOM YAPUNGUZA GHARAMA ZA MAWASILIANO YA SIMU TANZANIA.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.

•    Ujumbe mfupi (SMS) umepunguzwa kwa asilimia 45.
•    SMS zinazo sambazwa na tovuti ya Facebook na Twitter ni bure kabisa.


KAMPUNI ya simu za mikononi ya Vodacom, imepunguza kiwango chake cha gharama za upigaji simu, utumaji wa ujumbe mfupi na huduma za mtandao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema wamezindua kampeni mpya itakayokuwa na punguzo hilo kwa nia ya kukidhi mahitaji ya walio wengi katika soko la mawasiliano la simu za mkononi, hususan vijana na itawawezesha kupata taarifa nzito za kila wakati na kuwasiliana kwa simu za sauti, ujumbe mfupi na intaneti kwa bei nafuu.

Katika kampeni mpya iitwayo Wajanja, wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla watatozwa kiwango cha chini kabisa cha robo shilingi kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi.

Ofa hii mpya vile vile itawatoza bei ya chini kabisa ya ujumbe mfupi ya sh 25 kwenda mtandao wowote Tanzania, pamoja na kusambaza tovuti ya Facebook na Twitter bure.

Alisema kampuni hiyo imepunguza bei ya ujumbe mfupi kwa asilimia 45. Hakika si vijana tu watakaofurahia ofa hii mpya bali wateja wote wa Vodacom wa huduma ya kulipia kabla watafaidika na huduma pamoja na viwango hivi vipya vya chini.

Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, ya Afrika Kusini ambayo nayo ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK.

Vodacom Group (Pty) inamiliki asilimia 65 ya hisa zote huku nyingine 35 zikimilikiwa na mwanahisa wa Kitanzania na kampuni ya One Mirambo Ltd.

Advertisements

WANASHERIA WASEMA HAKUNA UTATA, UTEUZI MAWAZIRI KUTOKANA NA WABUNGE WATEULE.

Rais Jakaya Kikwete akimuapisha mmoja wa manaibu waziri

•    Mbowe, Kafulila wasema katiba na utaratibu umekiukwa,
•    Spika wa Bunge Anne Makinda amtetea Rais kwa kusema hakuna kipengele chochote cha sheria kilicho vunjwa.
•    Mwanasheria Mkuu wa Serikali asisitiza kwamba wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni wabunge

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ameshutumiwa na baadhi ya wananchi pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kuwa amevunja katiba kwa kuwateua wabunge na kuwapa Uwaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.

Wabunge wapya walioteuliwa na kupewa uwaziri ni Profesa Sospeter Muhongo aliyepewa Wizara ya Nishati na Madini na manaibu wawili wa Wizara ya Fedha; Janeth Mbene na Saada Mkuya Salum.

Mawaziri hao ni miongoni mwa wabunge wanne walioteuliwa kwa mujibu wa mamlaka ya rais aliyopewa na Katiba ambapo amepewa nafasi 10 za uteuzi. Mwingine aliyeteuliwa kuwa mbunge ni Mwenyekiti wa chama cha siasa cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema Rais Jakaya Kikwete hajavunja kipengele chochote cha sheria kuwateua wabunge na kuwapa Uwaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge.

Akifafanua kuhusu utata huo, Makinda alisema alichofanya Rais Kikwete ni sahihi kwa sababu aliowateua amewapa uwaziri ili wawajibike katika serikali yake.

Kwa mujibu wa Makinda, wateule hao wakishaapishwa kuwa mawaziri, wana haki ya kuanza kufanya kazi za kiwaziri kwenye wizara walizopangiwa.

Hata hivyo, Makinda akasema kanuni zitakuwa zinawafunga kuingia Bungeni na kujibu maswali bila kuapishwa kuwa wabunge.

Lakini akasema mara baada ya kuapishwa ndipo wataruhusiwa kuendesha shughuli za serikali Bungeni kama vile kujibu maswali ya wabunge.


Walichosema Mbowe, Kafulila

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema katika viwanja vya Unga Limited, juzi alitumia fursa hiyo kuponda uteuzi wa Baraza la Mawaziri akisema Rais Kikwete amevunja katiba kwa kuwateua watu ambao hawajaapishwa kuwa wabunge kushika nafasi za uwaziri.

Licha ya kuvunja katiba kwenye uteuzi, Rais pia amekiuka kwa kuwateua Wazanzibari kwenye wizara ambazo siyo za Muungano kama Afya aliyokabidhiwa na Dk Husein Mwinyi.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR, David Kafulila alisema Rais Kikwete amekiuka katiba kwa kuteua wabunge wateule kuwa mawaziri.

Kafulila alisema katiba inamuelekeza Rais kuteua mawaziri miongoni mwa wabunge na mbunge hutambuliwa kwenye nafasi hiyo baada ya kuapishwa.

“Nashangaa hawa hawajawa wabunge lakini amewateua kuwa mawaziri,” alinukuliwa Kafulila akihoji.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema ametoa ufafanuzi kwa kusisitiza kwamba wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria.

Aidha, alisema Katiba ya Nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo (wa kuteuliwa na Rais) kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo, awe ameapishwa Bungeni kwanza.

“Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba: “Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.” Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake.

“Wabunge aliowateua Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii,” alieleza Jaji Werema na kuongeza: “Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa Viti Maalumu au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e).

“Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.” Alisema Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo, awe ameapishwa Bungeni kwanza.

“Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

“Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria.

“Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa.

Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho,” alieleza zaidi Jaji Werema.

Aidha, Baraza jipya la Mawaziri lililosukwa upya na Rais Jakaya Kikwete, linaanza kazi Jumatatu Mei 7, 2012. baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri wapya.

Mabadiliko ya baraza hilo yanatokana na kashfa ya ubadhirifu wa mali ya umma iliyoibuliwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ambapo wabunge na baadhi ya wananchi walitaka wahusika wote wakiwamo mawaziri wa sekta husika wachukuliwe hatua.

Kuhusu ni lini wabunge hao wapya wataaapishwa kuwa na nguvu ya kufanya kazi zao bungeni, Anne makinda alisema kwa mujibu wa kanuni za bunge wataapishwa kabla ya kuanza vikao vya bunge lijalo la Bajeti litakalofanyika mjini Dododoma Juni mwaka huu.

MAWAZIRI WAPYA WAAPISHWA; WASEMA YALIYO MOYONI MWAO

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wateule baada ya kuapishwa rasmi Ikulu Dar es Salaam

•    Wahaidi kukabiliana na changamoto.
•    Makamba asema kazi yake ya kwanza ni kupitia upya garama za simu hapa nchini.
•    Dk. Mgimwa asema hakuna kitakacho shindikana, yeye kujikita zaidi na mfumko wa bei.

Rais Jakaya Kikwete amewaapisha mawaziri wapya pamoja na manaibu wake wakuu Jumatatu Mei 07, 2012 ikulu jijini Dar es Salaam.

Awali rais alifanya uteuzi huo kwa kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake kwa kuingiza sura 13 mpya huku mawaziri na naibu mawaziri nane wakitupwa nje ya baraza hilo.

Katika mabadiliko hayo, amewapandisha naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha mawaziri nane na naibu mawaziri sita, huku mawaziri na naibu mawaziri 22 wakibaki katika wizara zao za awali.

Mawaziri wapya watio apishwa na Wizara zao kwenye mabano ni Mbunge wa Handeni,  Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa (Fedha) na Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa  Sospeter Muhongo (Nishati na Madini).

Manaibu Mawaziri wapya ni Mbunge wa Rufiji, Dk Seif Suleiman Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (Nishati na Madini-  Nishati), Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba (Uchukuzi) na Mbunge wa Mvomero, Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Wengine ni Mbunge wa Makete, Dk Binilith Mahenge (Maji), Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Maselle (Nishati na Madini ), Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (Katiba na Sheria) na wabunge wa kuteuliwa, Janet Mbene na Saada Mkuya Salum ambao wote wamekuwa Manaibu Waziri wa Fedha.

Naibu Mawaziri waliopandishwa na kuwa mawaziri kamili ni Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Dk Fenella Mukangala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii).

Baada ya kuapishwa baadhi ya mawaziri walinukuliwa wakisema malengo yao pamoja na vipaumbele vyao katika nafasi zao hizo mpya.

Dk Mgimwa
Waziri mpya wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa, alinukuliwa akisema kuapishwa kwake ni jambo la heshima hivyo ni lazima kujituma na kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania.

Alipoulizwa jinsi atakavyo kabiliana na changamoto ndani ya wizara hiyo ikiwa ni pamoja na tuhuma zilizomng ‘oa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mustapha Mkulo, Dk Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Kalenga alisema kabla ya kufanya lolote ni lazima kujiridhisha.

“Bungeni tulikuwa tunazungumza mengi kuhusu wizara hii lakini niseme kwamba ni lazima ufanye tathmini na ukishajua hali halisi ya tatizo ndio unaweza kuzungumza suluhisho la tatizo husika ni nini, hakuna kisichowezekana,” alinukuliwa Dk Mgimwa

Makamba
Kwa upande wake Naibu mpya wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, January Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema moja ya mambo ya kufanya katika wizara hiyo ni kutazama upya gharama za mitandao ya simu.

“Wizara hii inagusa maisha ya kila siku ya Mtanzania hivyo kuna ulazima wa kutizama gharama za mitandao ya simu ili iendane na maisha halisi ya mtanzania” alisema Makamba.

Akizungumzia masuala ya sayansi, Makamba alisema kuwa kuna ulazima wa kutizama upya msingi wa elimu ya sayansi kuanzia shule ya msingi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma somo hilo.

Pia, aligusia mikakati iliyowekwa awali ya asilimia moja ya pato la taifa kuingizwa katika ufanyaji wa tafiti mbalimbali na kwamba umefikia wakati wa suala hilo kuanza kutekelezwa kikamilifu.

“Tunatakiwa kuondoa urasimu wa matumizi ya teknolojia, hakuna haja ya watumishi wa Serikali na wananchi kupanga foleni kwa ajili ya kuchukua fomu, huu ni wakati wa fomu kujazwa katika mitandao tu,” alisema Makamba.

Hata hivyo, Makamba alisema kuwa mambo mengi anayoyaona na kuyazungumza hata bungeni yameshaanza kufanyiwa kazi na wizara hiyo.

Rashid

Naibu Waziri mpya wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Suleiman Rashid alisema kuwa kipaumbele katika wizara hiyo ni kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi, tena kwa ubora mkubwa.


“Huduma ya afya inatakiwa kuwafikia watu wote nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mgonjwa anasafirishwa eneo moja mpaka jingine kwa usalama” alisema Dk Rashid.


Rashid ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji alisema kuwa wizara inatakiwa kushughulikia sera na kutengeneza mipango mizuri ili watumishi wake wafanye kazi katika mazingira bora kwa faida yao na Watanzania wote.


Tizeba
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa alisema kwa kuwa ni msaidizi wa waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe, atahakikisha kila jambo analofanya bosi wake linakwenda sawa.


“Namshuruku sana Rais Kikwete, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa kuwa wao ndio waliopendekeza mimi kuteuliwa kuwa waziri, nitatumia elimu yangu na uzoefu katika Serikali katika utendaji wangu wa kazi” alisema Dk Tizeba.


Mahenge
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Dk Binilith Mahenge ambaye ni Mbunge wa Makete, alisema kuwa atazungumza zaidi mara baada ya kuapishwa.

 

Masele
Akizungumzia kuapishwa kwake Masele alisema kwanza atapambana kudhibiti mali ya umma, kuhakikisha udhibiti wa madini na kupata thamani halisi ya kile kinachozalishwa.


Pia alisema atashughulikia matatizo ya wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakinyonywa ili waweze kupata haki zao stahiki na kuinua uchumi wao.


“Niwahakikishie Watanzania kwamba nimepewa nafasi kubwa na nitafanya kazi kwa uadilifu, “alisema Masele.


Aliongeza kuwa; “Tutahakikisha tunazipitia sheria na kuhakikisha wamiliki wa migodi wanawasaidia wananchi na kila sehemu ulipo mgodi tutashughulikia ili wananchi na serikali vyote vinufaike.”

Alisema kuna watu wanapotosha kuhusu elimu yake, lakini ana Shahada ya Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ambako alihitimu mwaka 2004.

Pia amewahi kufanya kazi katika benki kabla ya kupata nafasi ya kuwa Meneja Kanda ya Ziwa wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Tigo.

KATIKA DHANA YA UWAJIBIKAJI WATENDAJI KWENYE WIZARA ZENYE SHUTUMA WAJIUZURU.

Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaapisha mawaziri wateule Jumatatu Mei 7, 2012. kushika nafasi hizo mpya, Tayari baadhi ya wabunge wamewataka mawaziri hao wasifanye sherehe kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa; zikiwemo zilizosababisha mabadiliko yanayowapa nafasi.

Tunaunga mkono japo tungependa mabadiriko zaidi lakini sura mpaya ndani ya baraza hilo la mawaziri linatufanya turejeshe imani kidogo na serikali yetu. 

Kwa upande wetu tunafahamu kuwa moja ya sababu ya matokeo hayo ni uwepo wa watendaji wa Serikali ambao wamechangia kwa sehemu kubwa kuzembea katika nafasi zao na kumlazimu Rais Kikwete kuwawajibisha mawaziri kisiasa.

Watendaji hao wanajua kuwa baada ya mawaziri kuwajibika, wanafuata wao ili iwe fundisho kuwa utendaji mbovu utakaosababisha waziri, au Serikali kuwajibika kisiasa.

Mazingira hayo ya uwepo wa watendaji wanaosubiri kuwajibishwa, yanaweza kuwa kikwazo cha kazi kwa mawaziri hawa hasa kama atalazimika kufanya kazi kwa karibu na mtendaji anayetuhumiwa au ambaye anajijua anahusika na uzembe uliosababisha Serikali kuwajibika kisiasa.

Lakini tunashauri uzembe wa mtendaji ambaye anafuata nyayo za mawaziri waliowajibika kisiasa, usitumike kuwakwaza wateule wapya kwa namna yoyote kwa kuwa vikwazo vya namna hiyo, mwisho wake vina athari katika mustakabali wa maisha ya Watanzania.

Tunashauri kwamba lingekuwa jambo la uungwana na zaidi uzalendo kwa watendaji hao kuwa mstari wa mbele kuonesha kujuta na kuwasaidia wateule wapya kutekeleza majukumu yao wakati wakisubiri adhabu yao.

Katika kujenga dhana ya uwajibikaji katika jamii ya Watanzania, haitakuwa vibaya kwa mtendaji ambaye amehusika moja kwa moja na uzembe na anajijua kwa hilo, kujiuzulu ili kujijengea heshima katika mustakabali wa maisha yake katika utumishi wa umma.

Inajulikana kuwa kujiuzulu si rahisi, ni vigumu na wakati fulani inahitaji kujikana. Lakini ni jambo lililo wazi kwamba wengi waliojiuzulu na kukiri makosa, walijijengea heshima kulikowaliosubiri kuondolewa kwa kuwa mwanadamu kukosea kaumbiwa.


FAMILY PLANNING IS NOT THE ONLY GLOOMY ASSESSMENT OF THE COUNTRY’S ECONOMIC PROSPECTS.

Tanzania Prime Minister Mizengo Pinda

At the 2005 World Summit, the international community reaffirmed its commitment to cut in half the number of people living in extreme poverty by 2015 and achieve the eight Millennium Development Goals (MDGs), a series of time-bound and quantified targets to attack poverty’s root causes in a multi-dimensional way.

The scale of the challenges, and the benefits of success to individuals, communities and the family of nation, are enormous: Global population is expected to increase from about 7billion today to 9.3 billion by 2050, and the population of the 48 Least Developed Countries will more than double to reach 1.7 billion.

Almost all of the net increase in population is occurring in the urban areas developing countries, and in many of them, the number of people living in poverty is rising.

Moreover, the supportive development environment that prevailed in the early years of this decade is now threatened as the world faces a global economic slowdown and a food security crisis. At the same time, the effects of climate change are becoming more apparent.

Recent remarks by Tanzania Prime Minister Mizengo Pinda regarding rapid population growth and its impact on the living standards of Tanzanians come at a time when the country is struggling with poverty.

Tanzania is estimated to have a population growth rate of 2.9 per cent and Mr Pinda’s suggestion that we turn to family planning is a gloomy assessment of the country’s economic prospects.

Substantial evidence suggests that slower population growth and investments in reproductive health and HIV prevention (particularly among adolescents), education, women’s empowerment and gender equality reduce poverty.

Carrying out the Programme of Action adopted at the International Conference Population and Development (ICPD) in Cairo and reaching its goal of universal access to reproductive health information and services by 2015 is an essential condition for achieving the MDGs.

A central premise of the ICPD is that the size, growth, age structure and rural-urban distribution of a country’s population have a critical impact on its development prospects and on the living standards of the poor.

Poverty is multidimensional: impoverished people are deprived of services, resources and opportunities, as well as income.

The ICPD realized that investing in people and empowering individual women and men with education, equal opportunities and the means to determine the number, timing and spacing of their children could create the conditions to allow the poor to break out of the poverty trap.

It is not always true that huge populations always have a negative impact on economic growth. Some of the major economic giants in the world such as the United States of America and China have huge populations, yet their poverty levels are relatively low compared to most countries.

Huge populations are only harmful to the economy if they are compounded by other factors, such as the level of productivity of the population, the level of education and government policy. Infrastructure and health facilities may also be an issue.

Countries such as Tanzania, where economic planning is relatively poor, are always in danger of experiencing the negative impact of a huge population. For starters, we have not invested enough resources in education, which is a major economic driver.

As a result of this failure, many people—especially those who live in rural areas—are not only unable to achieve optimum productivity but they are also ignorant of reproductive health issues.

Lower fertility and slower population growth temporarily increase the relative size of the workforce, opening an historic, one-time only demographic window.

With fewer dependent children and older dependents relative to a larger, healthier working-age population, countries can make additional investment that can spur economic growth and help reduce poverty.

Within another generation, the window closes again, as the population ages and dependency increases once more.

If jobs are generated for the working population, this demographic bonus results in higher productivity, savings and growth.

In East Asia where poverty has dropped dramatically, this demographic bonus is estimated to account for about one third of the regions unprecedented economic growth from 1965 to 1990.

In the poorest countries, where fertility remains high, the demographic window will not open for some time, but investments now in reproductive health services can hasten its arrival and ensure future dividends.

Family planning continues to face opposition in many societies on the basis of religious beliefs and the perception that it is harmful to the health of those who are subjected to it.

We need to strike a balance between population growth and productivity. This can only be achieved by positive policies on education, health and infrastructure development.

JOB SCAN {MATOKEO YA NAFASI ZA KAZI LEO} JUMANNE MEI 8, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/EXAMINATIONS OFFICER

Qualification: Bachelor degree in Educations or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


ACCOUNTANCY GRADE I 

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


SENIOR INTERNAL AUDITOR

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy and CPA (T) or – ACCA or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR ADMINISTRATOR OFFICER

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Public Administration, Sociology, Human Resource Management or
equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR SYSTEMS ADMINISTRATOR

Qualification: Must be Holder of Bachelor degree or Advanced Diploma in Computer Science, Information Systems, Electrinics or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

RECORDS MANAGEMENT ASSISTANTS II – 2 POSITIONS

Qualification: Form IV Certificate together with Certificate in records Management from a recognized Institution or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

CLINICAL OFFICER II 

Qualification: Ordinary Diploma in Clinical Medicine from a recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LABORATORY TECHNICIAN II 

Qualification: Ordinary Diploma in Laboratory Technology from recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

COOPERATIVE DEVELOPMENT

Qualification: Masters Degree in Coopetarive or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

YOUTH WORK/GENDER STUDIES

Qualification: Master’s degree in work Gender Studies or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LINGUISTICS
Qualification: Master’s degree in Linguistics or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


POLITICAL SCIENCE

Qualification: Master’s degree in Political Science or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

BUSINESS ADMINISTRATION /HUMAN RESOURCE MANAGEMENT

Qualification: Master degree in Business Administration, Human Resource Management or equivalent

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ASSISTANT LECTURER – 5 POSITIONS

Qualification :( Bachelor’s Degree) to teach up to NTA level 8

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/ASSISTANT LIBRARIAN TRAINEE

Qualification: Bachelor degree in librarianship or equivalent qualification
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SOCIAL STUDIES (SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION)

Qualification: Bachelor degree in Sociology, Political Science, Public Administration or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ACCOUNTANCY
Qualification: Bachelor degree in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANTS – 3 POSTS

Qualification: Bachelor degree in either Computer Science or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ASSISTANT ACCOUNTANTS – 2 POSTS

Qualification: Minimum of Bachelor degree in Accountancy/finance or equivalent from a recognized Institution

Apply: The Excutive Director, Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) Box 8921, Dar es Salaam
Details: Daily News April 23, 2012

Deadline:  May   08, 2012

SYSTEM ADMINISTRATOR AND DATA MANAGEMENT

Qualification: Bachelor degree in Computer Science, Computer Engineering or Information Technology or equivalent from recognized Institution

Apply: The Excutive Director, Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) Box 8921, Dar es Salaam

Details: Daily News April 23, 2012

Deadline:  May   08, 2012


ADMINISTRATION OFFICER – 2 POSTS

Qualification: A minimum of Bachelor degree in Administration / Human Resources Managemnt

Apply: The Excutive Director, Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) Box 8921, Dar es Salaam

Details: Daily News April 23, 2012

Deadline:  May   08, 2012


FITTER MECHANICS – 2 POSITIONS

Qualification: Holder of Trade test grade 11/1 from a recognized Institution VETA, form IV or VI Certificate

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012


ELECTRICIAN
Qualification: Holder of Trade test certificate grade test certificate grade 3, 2 or 1, form IV or VI certificate

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

PLANT OPERATORS – 7 POSITIONS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Electrical / Machemical Engineering

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

MECHANICAL TECHNICIANS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Mechanical Engineering
Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

ELECTRICAL TECHNICIANS – 2 POSTS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Electrical Engineering
Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012


ONLINE BUSINESS MANAGER

Qualification: Graduate in Multimedia/Digital Media business
related degree or equivalent

Apply: Human Resources Manager Mwananchi Communications Ltd Box 19754, Dar es Salaam

Details: The Citizen April 26, 2012

Deadline:  May   08, 2012