JOB SCAN {MATOKEO YA NAFASI ZA KAZI LEO} JUMATANO MEI 9, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/EXAMINATIONS OFFICER

Qualification: Bachelor degree in Educations or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


ACCOUNTANCY GRADE I 

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


SENIOR INTERNAL AUDITOR

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy and CPA (T) or – ACCA or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR ADMINISTRATOR OFFICER

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Public Administration, Sociology, Human Resource Management or
equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR SYSTEMS ADMINISTRATOR

Qualification: Must be Holder of Bachelor degree or Advanced Diploma in Computer Science, Information Systems, Electrinics or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

RECORDS MANAGEMENT ASSISTANTS II – 2 POSITIONS

Qualification: Form IV Certificate together with Certificate in records Management from a recognized Institution or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

CLINICAL OFFICER II 

Qualification: Ordinary Diploma in Clinical Medicine from a recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LABORATORY TECHNICIAN II 

Qualification: Ordinary Diploma in Laboratory Technology from recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

COOPERATIVE DEVELOPMENT

Qualification: Masters Degree in Coopetarive or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

YOUTH WORK/GENDER STUDIES

Qualification: Master’s degree in work Gender Studies or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LINGUISTICS
Qualification: Master’s degree in Linguistics or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


POLITICAL SCIENCE

Qualification: Master’s degree in Political Science or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

BUSINESS ADMINISTRATION /HUMAN RESOURCE MANAGEMENT

Qualification: Master degree in Business Administration, Human Resource Management or equivalent

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ASSISTANT LECTURER – 5 POSITIONS

Qualification :( Bachelor’s Degree) to teach up to NTA level 8

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/ASSISTANT LIBRARIAN TRAINEE

Qualification: Bachelor degree in librarianship or equivalent qualification
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SOCIAL STUDIES (SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION)

Qualification: Bachelor degree in Sociology, Political Science, Public Administration or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ACCOUNTANCY
Qualification: Bachelor degree in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANTS – 3 POSTS

Qualification: Bachelor degree in either Computer Science or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


FITTER MECHANICS – 2 POSITIONS

Qualification: Holder of Trade test grade 11/1 from a recognized Institution VETA, form IV or VI Certificate

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012


ELECTRICIAN
Qualification: Holder of Trade test certificate grade test certificate grade 3, 2 or 1, form IV or VI certificate

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

PLANT OPERATORS – 7 POSITIONS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Electrical / Machemical Engineering

Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

MECHANICAL TECHNICIANS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Mechanical Engineering
Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012

ELECTRICAL TECHNICIANS – 2 POSTS

Qualification: Holder of FTC or Ordinary Diploma in Electrical Engineering
Apply: Senior Manager Human Resources Taneso Ltd Umeme Park Box 9024, Dar es Salaam

Details: The Express April 27, 2012

Deadline:  May   09, 2012


 

Advertisements

UTATA WA UMRI WA LULU; PINGAMIZI LAWEKWA NA UPANDE WA UTETEZI.

  • Wanasheria wasema ni utaratibu wa kawaida katika kesi

  • Hatua hiyo haina maana hoja ya mshitakiwa imekataliwa.

UMRI wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba Jumatatu Mei 7, 2012 ulizua utata katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mawakili wanaomtetea kutaka kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo ili akashtakiwe kwenye Mahakama ya Watoto.

Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 2:50 asubuhi akiwa peke yake kwenye gari linalobeba mahabusu, huku akisindikizwa na magari mengine mawili.

Alipoingia mahakamani alikuwa amezingirwa na askari Magereza na Polisi zaidi ya 10 na kuufanya  umati mkubwa wa watu uliofurika mahakamani hapo kushindwa kumwona vizuri.

Miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo ni baba mzazi wa msanii huyo, Michael Kimemeta na ndugu zake wengine kadhaa.  

Kesi hiyo ikitajwa kwa mara ya 3 Jumatatu Mei 7, 2012 huku mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Keneth Fungamtama, wakiwasilisha maombi kuhusu suala hilo la umri wa mteja wao wakitaka asishtakiwe mahakamani hapo kama ilivyo sasa.

Fungamtama ambaye alikuwa akisaidiana na Mawakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto.

“Mshtakiwa ana umri wa miaka 17 na tuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa,” alidai Fungamtama.

Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18.

Wakili huyo aliendelea kunukuu vifungu mbalimbali vya Sheria ya Mtoto kama 98 (i) na 114 (ii), ambavyo alidai kuwa vyote vinawapa nguvu ya kuwasilisha maombi yao hayo ya kuihamisha kesi hiyo.

“Hata katika suala la Mahakama, vifungu vyote vya sheria hii vimefafanua, hivyo tunawasilisha maombi yetu kwamba mteja wetu ana umri wa miaka 17 na shauri hili lingepaswa kusikilizwa Mahakama ya Watoto,” alidai.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliomba wapewe muda zaidi kwa sababu bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo.

“Kesi hii imekuja mahakamani hapa kama ya mauaji na upelelezi bado haujakamilika.

Tunaposema haujakamilika, tunapeleleza kila kitu, likiwamo suala la umri,” alieleza Kaganda.

Alisema hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa kilichowasilishwa mahakamani hapo, linasomeka Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo, kwa jina la Elizabeth Michael.

“Tunaomba muda tuweze kuchunguza kuhusu umri wa mshtakiwa kwa sababu aliwaeleza polisi kwamba ana umri wa miaka 18 halafu mawakili wake wanakuja kueleza hapa mahakamani kwamba ana umri wa miaka 17,” alidai Kaganda.

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kutokana na mvuto wa kesi hiyo katika jamii, wanaomba wapewe muda zaidi kufanya upelelezi ili kumtendea haki mshtakiwa huyo.

Kuhusu cheti hicho kusomeka Diana Elizabeth, Wakili Fungamtama alikiri na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili.

Fungamtama alidai kuwa hawana pingamizi na maombi ya upande wa mashtaka kwamba wapewe muda zaidi wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa, ingawa alidai kuwa suala hilo halina ugumu.

Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi Augustina Mbando alisema: “Mahakama imesikiliza maombi yaliyoletwa na Fungamtama na Kaganda na imeona kesi iliyopo hapa ni ya mauaji na jinsi kesi hii ilivyo, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika.”

“Kama defence (upande wa utetezi) wana maombi yoyote wanaweza kufanya hivyo kupitia Mahakama Kuu,”

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam msanii huyo wa kike, alimuua Kanumba.

MWONGOZO KUHUSU PINGAMIZI LA MWANZO KISHERIA

Pingamizi la mwanzo ni utaratibu katika sheria ambao unaruhusu moja kati ya pande mbili katika ama kesi ya jinai au shauri la madai kupinga kwa kukazia makosa yaliojitokeza ama katika maelezo ya matukio au/na sheria kama yalivyosomwa au kuandikwa na upande mwengine.

Pingamizi la mwanzo mara nyingi kama sio zote linakuwa katika namna ya maandishi likiutaarifu upande wa pili kuwa ktk siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi au shauri husika basi mdai/mshitaki au mdaiwa/mshitakiwa atapinga ama matukio fulani yanayodaiwa kuwa ameyafanya na/ama sheria fulani imetumika visivyo. Mara nyingi pingamizi linatakiwa liwekwe

WANASHERIA WASEMA NI UTARATIBU WA KAWAIDA KATIKA KESI.
HATUA HIYO HAINA MAANA HOJA YA MSHITAKIWA IMEKATALIWA.

MSIMAMO WA CCM KUHUSU TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA WANACHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishia amani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake.

Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao, yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo mwaka jana.

Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.

Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa kisiasa.

Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa kiutafiti.

Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi ya tuhuma, hiyo.

Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.

Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.

Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.

Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi

Ideology and Publicity Secretary