AIR TANZANIA YAKODI BOEING 737-500 KUTOKA AERO VISTA YA DUBAI

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limekodi ndege aina ya Boeing 737-500 ambayo inatarajia kuwasili Alhamisi Mei 10, 2012 Mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo ilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 imekodiwa kutoka katika kampuni ya Aero Vista iliyopo nchini Dubai na tayari imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) nchini Misri ilikoperekwa kwa ajili ya uchunguzi.

“Wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCCA) wamekamilisha uchunguzi wa ndege ambayo kwa sasa ipo jijini Cairo, Misri na ndege itarejea nchini kwetu Alhamisi Mei 10, 2012 mchana. Ndege hiyo imeshawekwa Nembo ya Kampuni ya ATCL na baada ya kuwasili tunategemea itaanza kufanya safari mara moja,” sehemu ya taarifa hiyo ilisema.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 12 kwenye daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 kwenye daraja la kawaida (economy class).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Bw. Paul Chizi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita alitoa maelezo kwa uchache juu ya ujio wa ndege hiyo lakini hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na ndege hiyo.

Chizi alisema kuwa mipango ya ujio wa ndege hiyo ilikuwa ni mipango ya muda mfupi iliyowekwa ili kuboresha huduma za ndege alisisitiza kuwa kampuni tayari ina mpango wa muda mrefu ambao utafanyiwa kazi kikamilifu.

ATCL hivikaribuni imezindua tovuti ikiwa katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kuongeza ubora wa ndege hiyo ya kitaifa.

Tovuti hiyo itawawezesha wateja kupata taarifa ya safari za ndege bila ya kufika katika ofisi za kampuni hiyo au mawakala na kuwawezesha wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijami
Advertisements

JOB SCAN {MATOKEO YA NAFASI ZA KAZI LEO} ALHAMISI MEI 10, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/EXAMINATIONS OFFICER

Qualification: Bachelor degree in Educations or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


ACCOUNTANCY GRADE I 

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications.

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


SENIOR INTERNAL AUDITOR

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Accountancy and CPA (T) or – ACCA or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR ADMINISTRATOR OFFICER

Qualification: Bachelor degree or Advanced Diploma in Public Administration, Sociology, Human Resource Management or
equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SENIOR SYSTEMS ADMINISTRATOR

Qualification: Must be Holder of Bachelor degree or Advanced Diploma in Computer Science, Information Systems, Electrinics or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

RECORDS MANAGEMENT ASSISTANTS II – 2 POSITIONS

Qualification: Form IV Certificate together with Certificate in records Management from a recognized Institution or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

CLINICAL OFFICER II 

Qualification: Ordinary Diploma in Clinical Medicine from a recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LABORATORY TECHNICIAN II 

Qualification: Ordinary Diploma in Laboratory Technology from recognized Institution or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

COOPERATIVE DEVELOPMENT

Qualification: Masters Degree in Coopetarive or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

YOUTH WORK/GENDER STUDIES

Qualification: Master’s degree in work Gender Studies or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

LINGUISTICS
Qualification: Master’s degree in Linguistics or equivalent
qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012


POLITICAL SCIENCE

Qualification: Master’s degree in Political Science or equivalent qualifications

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

BUSINESS ADMINISTRATION /HUMAN RESOURCE MANAGEMENT

Qualification: Master degree in Business Administration, Human Resource Management or equivalent

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ASSISTANT LECTURER – 5 POSITIONS

Qualification :( Bachelor’s Degree) to teach up to NTA level 8

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANT/ASSISTANT LIBRARIAN TRAINEE

Qualification: Bachelor degree in librarianship or equivalent qualification
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

SOCIAL STUDIES (SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION)

Qualification: Bachelor degree in Sociology, Political Science, Public Administration or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

ACCOUNTANCY
Qualification: Bachelor degree in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

TUTORIAL ASSISTANTS – 3 POSTS

Qualification: Bachelor degree in either Computer Science or equivalent qualification

Apply: Secretary, Public Service Recruitment Box 63100, Dar es Salaam
Details: Daily News April 30, 2012

Deadline:  May   14, 2012

JOHN MYIKA; TAARIFA YA CCM INADHIHIRISHA MAMBO KADHAA YA MSINGI

MOSI, kwamba chama legelege huzaa serikali legelege.

Ulegelege wa serikali katika kushughulikia masuala ya mauji ya raia ni matokeo ya CCM kushindwa kuonyesha kwa vitendo inavyothamini utu na uhai wa binadamu.

CCM isingekuwa legelege ingeiwezesha serikali inayoongozwa na wanachama wake kufanya uchunguzi wa vifo vyenye utata (inquest) kupitia mahakama maalum (coronary court).

Pili, kwamba CCM imekosa uhalali wa kimaadili wa kukumea vitendo hivyo na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwa wanazungumza maneno matupu ya amani na utulivu huku viongozi na wanachama wake wanafanya matendo ya vurugu na umwahaji damu.

Nape anasema hakuna ushahidi wa kimazingira, wakati anajua kwamba mpaka sasa kuna majalada yamefunguliwa dhidi ya viongozi wa CCM Kiteto, Busanda, Biharamulo kwa vitendo vya umwagaji damu kwenye kampeni za chaguzi ndogo.

CCM inajua pia kifo cha kiongozi wa CHADEMA Arumeru mpaka sasa kuna viongozi wake wamekamatwa na kuhojiwa na polisi.

CCM inajua kuwa makada wake wametajwa kwa majina kwenye tukio la kukatwa mapanga kwa wabunge wa CHADEMA Mwanza tukio ambalo mashahidi wameeleza kuwa hata Askari polisi wameshuhudia na kuachia litokee.

CCM inajua kilichomo mpaka sasa kwenye jalada la uchunguzi la mauji ya Mbwana Masudi kule Igunga.

Orodha ni ndefu ya watu na matukio, hivyo taarifa ya CCM ya kutoa kanusho la ujumla ni ishara ya kuficha ukweli na kugeuza mjadala suala ambalo halitafanikiwa, tamko hili la Nape ni kama Al Sahaf kule Iraq, CCM ikae vikao vyake vya kikatiba itoe maamuzi ya chama hicho kuhusu suala hili la umwagaji damu na mauaji ambayo yanatuhumiwa kufanywa na viongozi wa chama hicho pamoja na vyombo vya dola sio kwa wanaCHADEMA tu bali hata kwa wananchi wa kawaida.

Inapaswa kuwa kutoka kauli ya amiri jeshi mkuu na kiongozi wa serikali Rais Jakaya Kikwete. Tunachohitaji kusikia ni hatua kuchukuliwa kwa wahusika kama kweli hawajatumwa na CCM na serikali na sio propaganda.

Tatu, imekuwa ni kawaida ya CCM kuanza kwa kuukana ukweli unapotolewa lakini hatimaye hukiri sehemu ya ukweli huo kama zilivyokuwa kauli za CCM mara baada ya kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi.

Walianza kwa kanusho lakini hatimaye wakakubali kuna ufisadi ila wakadai mafisadi ni baadhi ya wanachama na sio chama, lakini mpaka leo wameshindwa kujivua gamba kama walivyodai.

Hata hili, wameanza kwa kukukana baadaye wanatesema ni la wanachama wachache waliotenda jinai bila kutumwa na chama, lakini ukweli utabaki kwamba haiwezekani matendo yote haya yakajirudiarudia bila vyombo vya ulinzi na usalama kufahamu.

Na tunazo taarifa juu ya mikakati ya CCM ya vurugu na vikundi wanavyotumia kufanya uharamia, na yapo majalada ambayo yamefunguliwa polisi. CCM inahitaji ushahidi gani zaidi toka kwa CHADEMA na umma?