TAARIFA KWA UMMA – TAMKO LA J. NASSARI KUHUSU HOTUBA YAKE NMC

Joshua Nassari (MB)

*TAARIFA KWA UMMA*

Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani… hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.

Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake

Joshua Nassari (MB)
Mei 09, 2012.

Advertisements

3 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA – TAMKO LA J. NASSARI KUHUSU HOTUBA YAKE NMC

 1. Ndugu Mhs. wewe kama mwakilishi wetu tunakutegemea sana, tunakuamini sana, jitahidi sana basi kuwa na mausiano mazuri wakati wamazungumzo yako kwa Umma si unajua. Sisi wananchi wachini tunateseka kuona mambo yetu hayaendi twasikia tu malumbano yakisiasa mpaka tunatamani Mwalimu angelikuwepo akajionea nyie wanae mnavyo tuwakilisha sijui na sijui na sijui na sipati picha angelisema nini baba yetu Mwalimu Julius K. Nyerere!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 2. Naamini Nassari hakuwa anamaanisha alichosema. Ila pia najua kuwa hawezi kukanusha (na wala hajakanusha) kuwa alsema hivyo. Na ni kweli maneno yake yamekaa kiuvunjifu wa sheria ya kanuni ya adhabu. Kimsingi polisi wana haki kabisa ya kumchukulia hatua wanazochukua sasa. Na wala wasilaumiwe.

  Ushauri wangu kwa wanasiasa – hasa vijana- ni kuwa wajifunze kuwa makini. Wajue kuchuja nini waseme na wapi. Waache kukurupuka na kubwabwaja tu kwa sababu ya kutafuta cheap popularity au kwa vile wana umati mkubwa (ushabiki). Sheria yetu iko wazi kuwa maneno ya uchochezi ni kosa la jinai.

  Kwa hiyo, kuna haja ya wanasiasa – hasa wenye elimu kama Nassari – kuwa makini na kauli zao. Namshukuru sana Mh Mbowe ambaye, kama kiongozi makini, alikuwa wa kwanza kusense tatizo kwenye matamshi ya Nassari na kusimama hima na kuyarekebisha. Kimsingi alimkemea Nassari politely. Na nina uhakika chama chao wamekaa wakalijadili hilo na ndio maana hata ya hii taarifa ya Nassari. Wazidi kusisitiza umakini kwa wanasiasa wao.

  Nina uhakika hii taarifa ya Nassari inatokana na kosa ambalo analijutia-hata kama ni “ulimi uliteleza”. Ingawa anaweza kuwa hakumaanisha bado inaweza kumbidi kuthibitisha hilo mahakamani kama polisi wataamua kulivalia njuga. Na asiwalaumu kwa hilo.

 3. Mr. Materu, Ningeomba mwongozo kuhusu hii sheria ya uchochezi, kwasababu kwa upande mmoja naona kama inamyanganya mtu au kikundi fulani haki ya kusema kile wanachoona ni sawa au kina maslahii kwao.

  Kwamfano Nassari kwenye kauli yake siyo lazima kuwa alimaanisha kuigawa nchi ila lililo wazi ni kuchoka kwa matumizi mabaya ya fedha zinazotokana na vivutio pamoja na ardhi yao ambayo wananchi walio mchagua awafaidiki nayo.

  waziri aliyekuwa na dhamana ya utarii na maliasilia tunaambiwa aliweza kununua nyumba ya mabilioni iwe kwa kulipwa mshahara au kwa ujanja wake ila lililo wazi ni kuwa fedha hizo zilitokana na nafasi yake hiyo ya uwaziri. ikumbukwe watu wa Arumeru awana hata maji safi ya kunywa, fedha hizo ambazo waziri huyo ametumia zingeweza kujenga zaidi ya visima 100 virefu vya maji ambayo yangetoa huduma kwa mwaka mzima. hapo umoja wa kitaifa ni wa nini?

  kwa kitu kama hicho cha keki ya taifa kuliwa na wachache je tunapaswa kungagania kuendelea kuwa na nchi kubwa ambayo wananchi wa sehemu husika aiwafaidishi?

  Kosa hilo la kujinufaisha wachache mimi ndiyo naona ni uvunjifu wa amani na uchochezi.

  Tena wengi wetu utakao wasikia wakipigani kuwa kunafaida ya kuwa nchi moja bila kutengana ni wanasiasa kwa faida ya kutawala sehemu kubwa. mwananchi wa kawaida wa mtwara ambaye ana nauli hata ya kwenda hospitali haitaji kujuwa au faida ya kuwepo mkoa wa kagera labda kama anaweza kupata ndizi au kahawa kwa bei nafuu. vinginevyo haina faida kwa mwananchi wa kawaida.

Comments are closed.