KATIKA KESI YA LULU KWA TAFSIRI YANGU; SHERIA YA MTOTO NO 21 YA 2009 KIFUNGU CHA 113 (1) NA KWA HATUA YA KESI HUSIKA ILIPOFIKIA HAKIMU MKAZI WA KISUTU YUKO SAWA.

  • Pingamizi ni sehemu ya kesi kwahiyo inapaswa kusikilizwa na mahakama husika.

    Ombi namba 46 ya mwaka 2012, mawakili wa utetezi wanaiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

    Pingamizi la awali hali wekwi kama hakuna kesi, na mara nyingi kama sio zote mahakama inayo sikiliza pingamizi ndio mahakama inayo sikiliza kesi husika

MAOMBI ya uchunguzi wa umri wa muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael (Lulu) anayekabiliwa na kesi ya mauaji, yamepangwa kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mei 28, 2012.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Maombi hayo yaliwasilishwa Mahakama Kuu na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala, Mei 17 wakidai mteja wao ana umri wa miaka 17 tofauti na hati ya mashataka inayo onyesha umri wa miaka 18.

Habari ambazo zilipatikana Ijumaa Mei 18, 2012 kutoka mahakama kuu na kuthibitishwa na Wakili Kibatala zinasema kuwa maombi hayo yamepangwa kuanza kusikilizwa Mei 28 na atakaye sikiliza ni mheshimiwa Jaji Dk Fauz Twaib.

Katika maombi namba 46 ya mwaka 2012, mawakili hao wanaomtetea msanii huyo wanaiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.

Jopo la mawakili hao maarufu linadai kuwa linaamini kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.

Lakini pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7, 2012 wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto.

Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.

Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.

“Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliyekuwa na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wetu alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto,” alidai Wakili Fungamtama.

Hata hivyo upande wa mashitaka kupitia kwa wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.

Katika uamuzi wake, Hakim Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote.

Hivyo Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo, aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.

Msanii huyo bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu.

Bahada ya malumbano hayo nimejaribu kuipitia sheria ya mtoto no 21 ya mwaka 2009, hususani kifungu cha 113 (1).

Kifungu hicho Kinasema wazi, “ikiwa mtu yoyote akiwa anashitakiwa au hapana, akapelekwa mahakamani kwa namna nyingine zaidi ya kutoa ushahidi, na ikaonekana na mahakama kuwa ni mtoto, mahakama itatakiwa kufanya uchunguzi wa umri wa mtu huyo”.

Je kipengele hiki kinatumika wakati gani?

Swali la Msingi ni je kifungu hiki kinaruhusu kutumika hata kwa hatua ambayo mahakama ipo kwa sasa {Kesi ya Lulu} katika committal proceedings kufanya due inquiry kuhusiana na umri wa mtu anayehisiwa / dhaniwa kuwa ni mtoto?

Labda ningependa watu wajue nini maana ya committal proceedings  and why committal proceeding?

Committal proceeding kwa kiswahili rahisi ni utaratibu wa kisheria ambao mahakama fulani ambayo haina nguvu kisheria kusikiliza kesi tajwa inapewa nguvu ya kukusanya taarifa zote mhimu na kuziwasilisha katika mahakama husika.

Mfano mzuri ni pale panapotokea kesi ya mauaji ambapo mahakama kuu tu ndio yenye nguvu kisheria kusikiliza kesi hizo.

Mahakama ama ya mwanzo, wilaya, au hakimu mkazi inatumika katika hatua za awali kama kumuandikia hati ya wito, kumsomea mashitaka, na kadhalika ila mshitakiwa hatotakiwa kujibu lolote {kama ilivyo sasa kwenye kesi ya Lulu}.

Kwanini utaratibu huu umewekwa?

Utaratibu huu umewekwa kwa mahakama za chini kuisaidia mahakama kuu katika mambo ya awali kabla ya kusikiliza kesi hizo zilizotengwa maalumu kwa ajili ya mahakama kuu.

Hii husaidia kuharakisha mwenendo wa kesi kwani ikifika mahakama kuu basi mambo mengi ya awali huwa yameshakamilishwa katika mahakama za huku chini na pia kupunguzia mzigo mahakama kuu.

Hivyo kinachofanyika sasa hivi katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuhusiana na kesi ya mauaji inayomkabili muigizaji chipukizi Lulu ni committal proceedings ambako kesi inaishia kutajwa na si kusikilizwa.

Hii ni kwasababu kesi ya mauaji inaangukia katika makundi ya kesi zinazoweza kusikilizwa mahakama kuu tu na mahakama ya rufaa iwapo kutakuwa na rufaa.

Swali la kujiuliza ni je katika hatua ya awali ya kesi kutajwa tena na mahakama ambayo haina nguvu kisheria kusikiliza kesi hiyo pingamizi lolote linaweza kusikilizwa?

Kwa tafsiri yangu ya sheria ni kwa kukubali kusikiliza pingamizi katika kesi ambayo mahakama haina nguvu kisheria kusikiliza kesi husika ni kukiuka sheria kwakuwa tayari utakuwa umeanza kusikiliza sehemu ya kesi ambayo ni pingamizi.

Kwanini nasema hivyo, pingamizi la awali haliwekwi kama hakuna kesi, na pili, mara nyingi kama sio zote mahakama inayosikiliza pingamizi ndio mahakama inayosikiliza kesi husika.

Hivyo kukubali mahakama ya hakimu mkazi kisutu isikilize pingamizi la umri wa lulu ni sawa na kusikiliza sehemu ya kesi hiyo.

Kifungu hicho cha sheria ya mtoto walichokitaja hakikumaanisha kuwa hata katika committal proceeding mahakama chini ya mahakama kuu inaweza kufanya due inquiry kuhusu umri.

Iwapo draftmen walikuwa wanamaanisha hivyo basi wangeonyesha wazi kuwa iwapo mahakama itakuwa ina wasi wasi na umri wa mtu Fulani kuwa yawezekana ni mtoto basi hata kama kesi iyo ipo katika committal proceeding ichunguzwe vinginevyo inabaki kuwa kama hakimu mkazi kisutu alivyooamua.

Ni mahakama kuu tu ndio ina uwezo wa kusikiliza pingamizi la mwanzo kuhusiana na kesi ya mauaji kwakuwa ni mahakama pekee kisheria yenye nguvu kusikiliza kesi hiyo.

Ndio maana hata mawakili waliomba mahakama kuu wamesema kama maamuzi yaliofanywa mahakama ya hakimu mkazi kisutu ni sahihi basi mahakama kuu ilisikilize pingamizi hilo.

Watu waelewe pia hakimu mkazi huyu hakukataa pingamizi ila alikataa kusikiliza pingamizi.

Advertisements