BADEA YAIKOPESHA TANZANIA BILIONI 34.5 KUJENGA BARABARA ZANZIBAR.

  • Barabara husika ni kutoka Wete Pemba hadi Chakechake itakayoanza kujengwa Oktoba mwaka huu.

    Waziri wa Fedha na Uchumi
    Dk. William Mgimwa

  • Mradi Kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2014

TANZANIA imepokea msaada wa sh bilioni 34.5 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami visiwani Zanzibar.

Msaada huo umekuja siku moja kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufungua mkutano wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika (ADFB) mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa alisema ujenzi huo utahusisha barabara yenye urefu wa kilometa 22.

Aliitaja barabara husika kuwa ni kutoka Wete Pemba hadi Chakechake itakayoanza kujengwa Oktoba mwaka huu ili kurahisisha mawasiliano ya pande hizo mbili za visiwa, na kuongeza kwamba barabara hiyo itapanuliwa.

“Kabla ya upanuzi, utafanyika upembuzi yakinifu na tathimini ya gharama za mradi huo na fidia kwa wamiliki wa majengo pembezoni mwa barabara hiyo… mradi utakamilika mwanzoni mwa mwaka 2014,” alisema waziri huyo.

Dk. Mgimwa alimuahidi Mkurugenzi Mkuu wa BADEA, Abdelaziz Khelef kuwa, fedha hizo za mkopo na michango iliyotolewa zitatumika kama ilivyokusudiwa ili kuwa chachu ya nchi na taasisi nyingine za fedha kuendelea kuisaidia Tanzania.

Advertisements

One thought on “BADEA YAIKOPESHA TANZANIA BILIONI 34.5 KUJENGA BARABARA ZANZIBAR.

Comments are closed.