VYAMA HASIMU VYA CCM NA CHADEMA VYA HASIMIANA KWENYE MSIBA WA BOB MAKANI.

  • Mukama amwaga sifa kwakusema, Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja.

  • Mbowe a toa ufafanuzi na kurekebisha kauli hiyo akisema, ”Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa”

  • Dulu za kisiasa za itafsiri kauli ya Mkama ilikuwa na lengo la kuwachochea watu waliofika msibani waingie kwenye kwenye malumbano ya siasa kwa kuwa aminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

Ushindani wa vyama pendwa vya CCM na CHADEMA umechukuwa sura mpya katika kile kilicho tafsiriwa kuwa ni vijembe vya kisiasa vilivyo tawala msiba wa muasisi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Bob Nyanga Mohammed Makani.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Jumatatu June 11 2012 wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama chake katika viwanja vya Karimjee ziliko fanyika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, alimsifu Makani akisema alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana.

Akaongeza kusema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza wa CHADEMA kutoka nje ya kanda ya kaskazini kati ya waasisi wenzake tisa. 

Alihashiria kuwa pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Duru za kisiasa zinasema kuwa Mukama alikuwa na lengo la kuuaminisha umati uliyofurika msibani kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

Mbali na sifa nyingi alizomwagia marehemu, Mukama pia alisema CHADEMA wanatakiwa kuweka kumbukumbu hiyo kwa kuwa alikuwa ni mtu shupavu asiyependa kuongea wala kuhubiri kwa muda mrefu na asiyekumbatia udini, ukabila na ukanda.

Hata hivyo, wakati Mukama akieleza hayo, viongozi wengi wa CHADEMA walionekana kushangazwa na kauli hiyo.
Mwenyekiti  wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ”Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa”. 

Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana. 

Katika orodha hiyo, Mbowe aliwataja waasisi na mikoa yao kuwa ni Edwin Mtei (Arusha), Makani (Shinyanga), Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa), Edward Barongo (Kagera), Mary Kabigi (Mbeya), Menrad Mtungi (Kagera), Costa Shinganya (Kigoma), Evalist Maembe (Morogoro) na Steven Wassira (Mara).

Mbowe alisema kuwa kitendo cha kusema kuwa CHADEMA kiliasisiwa na watu tisa kutoka eneo moja la kanda ya kaskazini ni uchafuzi wa kihistoria ndani ya chama hicho.

“Mimi wakati huo nilikuwa mdogo na shughuli zangu zilikuwa ni kuandaa vikao na mikakati ndani ya chama. Nashangaa sana wakati nakumbuka historia ya chama hiki, hivyo watu wasijaribu kuipotosha,” alisema Mbowe.

RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete naye alielezea kuhuzunishwa kwake na msiba huo na kusema kuwa Bob Makani alikuwa ni mtu muhimu na msaada mkubwa katika michango yake aliyowahi kuitoa katika kukuza uchumi wa nchi.

“Nilisikia taarifa za msiba ambao ulinihuzunisha na kushtuka sana nikajaribu kumpigia simu Mwenyekiti wa Chama, Mbowe, lakini hakupatikana kwa kuwa alikuwa katika shughuli kubwa huko Ruangwa, nikamtumia ujumbe mfupi na baada ya kuupokea akanipigia na mimi nilikuwa katika shughuli sikupatikana, hivyo nikampigia tena baadaye ndipo tukazungumza,” alisema Kikwete.

Rais Kikwete alisema kuwa ni vema kuhuzunika kwamba tumepoteza mtu muhimu lakini pia iendane sambamba na kusherehekea na kuyaenzi mambo yake mazuri ambayo ameyafanya wakati wa uhai wake.

PROFESA BAREGU

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Baregu alisema anamkumbuka marehemu Bob Makani kama mwasisi wa mageuzi ambaye alikuwa shupavu na mwaminifu katika kukijenga chama hicho.

“Chama kitaendelea kukua kwa kasi kama wanachama wake watawaiga waasisi wake kama alivyofanya marehemu Bob Makani enzi za uhai wake,” alisema.

Profesa Baregu alisema hata kipindi alichokuwa akiumwa, aliendelea kuonekana kwenye shughuli za chama.

PROFESA LIPUMBA

Kwa niaba ya vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, alimwelezea Makani kuwa alikuwa mtu mzuri na kwamba CHADEMA inatakiwa kuiga mfano wake wa kuunganisha watu.

Alisema alikuwa ni mwana mageuzi aliyeasisi harakati za mabadiliko ya Katiba na kusema alipata suluba pamoja naye katika mapambano hayo. Pia alikumbushia enzi zao za shule akisema Makani alikuwa na akili nyingi darasani.

EDWIN MTEI

Muasisi wa CHADEMA ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Edwin Mtei, alimtaka Makani kuwa alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, na ameeleza masikitiko yake ya
kuondokewa na mwenzake.

Mtei alisema Makani kwa nafasi yake katika BoT alikuwa ni mtu aliyejali maslahi ya nchi na pia mwepesi wa kutoa taarifa za fedha.

DK. WILLIBROD SLAA

Akisoma wasifu wa marehemu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema walifaidi utawala wa sheria na aina ya uongozi wa Makani kutokana na kuwa mwanasheria.

Alisema Makani ni mfano wa kuigwa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyekuwa na kipaji cha kuelewa wananchi ambapo urefu wake uliweza kuonekana kila mahali alipoenda sambamba na ucheshi wake.

Asema kuwa Makani alizaliwa mwaka 1936 katika Hospitali ya Kolandoto, Shinyanga na kusoma shule ya msingi Ibadakuli mkoani humo. Alifauru sekondari na kupelekwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambako alifuzu na kupata Shahada ya Kwanza katika Uchumi (BA Economics).


Makani ni mwasisi wa CHADEMA mwenye kadi namba tatu baada ya Edwin Mtei, na marehemu Brown Ngwilulupi. Mwaka wa 1998 akachaguliwa kuwa mwenyekiti chama hadi 2003.Mwaka wa 1961 alikwenda Chuo Kikuu cha Liverpool, nchini Uingereza na 1965 akatunukiwa Shahada ya Sheria (LLB) alirudi nchini ambapo aliajiriwa na serikali kama Mwanasheria wa Serikali kwa muda mfupi kabla hajapandishwa cheo na kuwa Exchange Control Manager wa Benki Kuu.

Makani pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi za wakurugenzi katika Shirika la Ndege Tanzania, Williamson Diamond, Tanzania Breweries, Benki ya Taifa ya Biashara na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society.

Advertisements

6 thoughts on “VYAMA HASIMU VYA CCM NA CHADEMA VYA HASIMIANA KWENYE MSIBA WA BOB MAKANI.

  1. Asante kamanda!! Hii inadhihirisha Ushindi na kujiamini kuliko ndani ya CDM. Hakuna mambo ya Yes! Yes! hapa. Ila kwao kumebakia nini? AIBU! AIBU! AIBU! Katika kila liwatokalo. CCM sasa basi, someni nyakati!!!

  2. Kwa nin watu wanafanya msiba uwanja wa siasa? tulitarajia hapa watu watulie wakimuombea marehemuapumzike kwa amani na pia kukumbuka yale yote mema aliyosimamia! Mkama namfananisha na magimbi fulani kule kwetu hata uyapike kwa mwezi hayaivi ndio kichwa cha Mukama!!

  3. Tumempenda sana ndugu Makani lakini mungu amempenda zaidi hivyo tuwe na subira ktk kipindi hichi kigumu cha maombolezo,cha muhimu ni kuiga yale yote mema aliyoyafanya kipindi cha uhai wake.POLENI SANA CHADEMA NA WATANZANIA WOTE

Comments are closed.