BAJETI YA 2012/2013 NI YA KUWANUFAISHA WACHACHE; DK SLAA

  • KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

    TAIFA LINAKOPA ILI IWEJE, KULIPANA MISHAHARA NA POSHO AMA?

  • WIZARA YA NISHATI NA MADINI ITATUMIA SH MILIONI 567 KWA AJIRI YA MAWASILIANO, BADALA YA MILIONI 71.76 ZILIZOTUMIKA MWAKA JANA.

  • ASHANGAA KUONA KILA MWAKA SERIKALI AKILI YAKE INALALIA KUONGEZA KODI KWENYE VILEO NA KUACHA SEKTA NYETI KAMA MADINI.

  • NI KATIKA MAKOSA KAMA HAYO IMENYIMWA MKOPO WA SH BILIONI 480 KWA AJILI YA SHIRIKA LA UGAVI WA UMEME TANZANIA (TANESCO).


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameshangazwa na hotuba ya bajeti iliyosomwa bungeni Alhamis June 14 2012, amenukuliwa akisema inaonyesha wazi kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imeshindwa kutawala na badala yake kuwa danganya  wananchi kwa porojo.

bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Dk. William Mgimwa,  inaonesha kuwa matumizi ya kawaida yametengewa trilioni 10.5, sawa na asilimia 70, na matumizi ya maendeleo yametengewa trilioni 4.5, sawa na asilimia 30, wakati fedha za ndani zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni trilioni 2.2 tu, badala ya 2.7

Alisema kuwa kitendo cha serikali kushindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato na badala yake kuendelea kutegemea vinywaji laini na vileo na kuruhusu wananchi waweke majina yao kwenye pleti za magari badala ya namba za magari ni hatua kuwa hawana ubunifu wa kukuza uchumi.

Kibaya zaidi katika bajeti hii, mapato ya ndani kwa sasa yameongezeka kwa trilioni 1.5, huku matumizi ya kawaida yakipanda kwa trilioni 1.9 wakati fedha za maendeleo zikipungua kwa bilioni 397.8 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2011/12

Aliongeza kuwa hata, vipaumbele ambavyo serikali imeelekeza kwenye bajeti yake, utekelezaji wake utakuwa mgumu kwani fedha zilizotengwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi.

kitendo cha serikali kutenga trilioni 2.2 badala ya trilioni 2.7 ambayo inaleta tofauti ya sh bilioni 500, iliyoainishwa awali katika mpango wa maendeleo, kimeifanya miradi mingi kutengewa fedha kidogo huku mingine mingi ikikosa fedha kabisa

Dk. Slaa ambaye alikuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, alisema licha ya kwamba ni mapema kutoa maoni lakini bajeti imejaa matamko ya kisiasa.

“Hayo aliyosoma Waziri William Mgimwa ni matamko ya kisiasa si hotuba ya bajeti, kwani tunaoelewa bajeti ni vitabu vinne wanavyopewa wabunge, nami navingojea nimeomba nipatiwe ila kama ndiyo hivyo alivyosoma tuko kwenye hali mbaya,” amenukuliwa.

Alisema kuwa kinachoshangaza ni kuongezeka kwa deni la taifa halafu fedha zinazokopwa na serikali imezielekeza kwenye matumizi ya kawaida badala ya maendeleo.

“Taifa linakopa ili iweje, kulipana mishahara na posho ama? Hii ni hatari kwa vizazi vijavyo miaka 30 hadi 40 ijayo. Zamani hata serikali zilizotangulia zilikopa lakini mikopo hiyo ilitumika kujenga viwanda, shule, barabara na huduma nyingine, leo tunafanya hivyo?” alhoji.

Alisema inashangaza kuona serikali inakopa kutoka vyombo vya biashara halafu inapelekea fedha hizo kwenye uendeshaji jambo lililozifanya hata taasisi za fedha za kimataifa kuwanyima mikopo na hivyo wamekimbilia kwenye mabenki.

Alifafanua kuwa ni katika makosa kama hayo imenyimwa mkopo wa sh bilioni 480 kwa ajili ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa Wizara ya Nishati na Madini, Hotuba inaonyesha kuwa imetengewa sh milioni 142 kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya mafunzo ya nje, wakati mwaka jana ilitenga sh milioni 34, hivyo kuwa na ongezeko la milioni 108.

Wizara hiyo itatumia sh milioni 567 kwa ajili ya mawasiliano, badala ya milioni 71.76 ilizotumia katika mwaka wa fedha 2011/12, wakati katika kile kilichoitwa Kitengo cha Utawala na Mawasiliano kitatumia sh bilioni 2.003 badala ya sh milioni 53.87 za mwaka jana.

Nayo Wizara ya Fedha na Uchumi imetengewa sh milioni 582.3 kwa safari za wakubwa za ndani, katika Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, wakati mwaka jana ilitumia sh milioni 283, na safari za nje itatumia sh milioni 874,wakati mwaka jana ilitumia sh milioni 532.

Kuhusu vyanzo vya mapato, Dk. Slaa alisema anashangaa kuona kila mwaka serikali akili yake inalalia kuongeza kodi kwenye vileo na kuacha sekta nyeti kama madini.

“Tumerudia vyanzo vile vile ukiacha hicho cha watu kuruhusiwa kutumia magari yenye majina yao badala ya namba za usajili, sasa labda walevi watakapogoma kunywa ndipo serikali itapata ubunifu wa kuangalia vyanzo vingine,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa aliponda chanzo kipya cha mapato cha kuwaruhusu watu kuweka majina badala ya namba, akidai kuwa hatua hiyo mbali na kuleta matabaka kisaikolojia kwa wenye fedha kujiona wameiweka serikali mfukoni lakini pia ina madhara kuichumi.

“Mafisadi hawaoni uchungu hata kidogo kutumia fedha ila jambo la msingi ni kwamba wamezipataje, sasa kwa hali kama hii watafurahi kwa vile wanaona serikali imewahalalisha bila kujali kama fedha zao ni haramu,” alidai.

Advertisements

3 thoughts on “BAJETI YA 2012/2013 NI YA KUWANUFAISHA WACHACHE; DK SLAA

  1. Wanafunzi mkopo hawapat,madaktar mishahara midogo,walimu wanacheleweshewa mishahara pamoja na midogo.hao kila mara utackia wanajiongezea mishahara,posho na kuendelea ku2mia magal a bei gal,jaman kiongoz ni yule anayejal maisha wananchi wake na wala c kujal kitambi chake.2mbo 2 bt maendeleo nothin.wasome upya budget

  2. Hii serikali ya magamba tumeichoka,kila bajeti hakuna jipya,migodi ya madini inaachwa badala ya kukamuliwa kodi serikali inategemea pombe na sigara.Dawa ya haya yote ni kuikataa serikali ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

  3. Dr. tunafaham sana juu ya uzoefu wako katika maswala ya siasa na binafsi nakili kuwa your my politacal hero. Napenda kuuliza katika hali kama hii ambayo serikali inaonekana kuchoka natena kuendelea kuwa kandamizi kwa wananchi wake wasio na uwezo huku wakubwa wakiendelea kuboreshewa maisha ungependa unge shauri njia ipi itumike kuondoa serikali iliyoko madarakan manake naona siku bado nyingi. la ziada ningependa kupata your email ili tujadiliane mawili matatu hivi

Comments are closed.