BREAKING NEWS JUMANNE JUNE 19 2012 – JOHN MNYIKA ATOLEWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE

JOHN MNYIKA

 TAARIFA KWA UMMA

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.

Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.

Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge.

Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika

19 Juni 2012

Advertisements

3 thoughts on “BREAKING NEWS JUMANNE JUNE 19 2012 – JOHN MNYIKA ATOLEWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE

  1. Kanuni za bunge ziko wazi kama wabunge wanataka mabadiliko ni bora wakaanza na kanuni badala ya kumlaumu spika ambaye amesoma kifungu cha adhabu ambacho kiko wazi.

    Inawezekana itikadi za CCM na chadema zikatupeleka kwenye malumbano lakini ukweli uko wazi Mnyika alikuwa na nafasi moja tu ya haraka ya kuondoa maneno yake ili kifungu cha 64 (b) cha kanuni za bunge kisimwangukie.

  2. LEO KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA BUNGE LA TANZANIA, MBUNGE WA UBUNGO KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO JOHN MNIKA ALIAMURIWA KUTOKA BUNGENI BAADA YA KUKATAA KUFUTA KAULI YAKE TATANISHI YA KUWA RAIS JAKAYA KIKWETE NI DHAIFU.

    MY TAKE :- HII INAMAANA YA KUWA KAULI HII YA MYIKA ITABAKI KATIKA HANSARD ZA BUNGE LA TANZANIA MILELE.

  3. “Msema kweli hukimbiwa na marafiki zake nikipatwa na ajali kama hiyo sitawaonea wivu wale wanaodumu na marafiki zao siku zote. Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo na kujinyima ushirika wa milele unaotarajiwa kutokea baada ya kushindwa kwa uongo’’-Shabarn Robert

Comments are closed.