YALIYOJIRI KWA UFUPI BUNGENI KATIKA MJADALA WA BAJETI YA 2012/13 JUMATATU JUNE 18, 2012 JIONI

HAPA NDIPO WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HUKUTANA

Wakati wa mjadala wa bajeti ya mwaka 2012/13 ukianza kujadiliwa wabunge wameonyesha kukosa uvumilivu kutokana na maneno makali waliyokuwa wakiyatumia na kufanya uchangiaji huo kuendeshwa kwa hisia kubwa.

Nitajaribu kuandika kadri walivyosema. Nitawanukuu kadri ya alivyosema, lakini ni wazi sitaweza kuaandika yote (ya muhimu) yaliyosemwa na kwa namna ile ile alivyosema, maana nilikuwa nikitype kwa wakati ule ule aliokuwa akizungumza. 

Kivutio kikubwa kilikuwa kwa, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi-CCM) pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John  Komba, jana walichafua hali ya hewa bungeni kutokana na maneno makali waliyotoa.
Wakati Lissu alisema wabunge, Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kuona aibu kutokana na udanganyifu wanaowafanyia Watanzania kwa kupanga mambo wanayojua hawatayatekeleza kupitia bajeti, akisema ni upuuzi. 

Alifuatiwa na Mwigulu Nchemba, looh! Badala ya kuzungumzia bajeti in details akaanza kumsakama Lissu na wapinzani na bajeti yao akisema wapinzani ni wanafiki, waongo, wana mapepo na wanapaswa kuombewa. Akatupa hata kitabu cha bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni iliyosomwa na Kabwe Zitto Zuberi.

Nchemba kama alivyokurupuka kujibu tamko la Zitto juu ya kufilisika hazina kama ambavyo taarifa za Benki Kuu (BoT) kwenye mtandao zilikuwa zinaonekana kuonesha, na kuripotiwa na blog yetu ya http://www.media2solution.wordpress.com ndivyo ilivyojitokeza tena Jumatatu 18, 2012 jioni. 

Uku akitanguliza mbele kujisema juu ya uwezo wake kiuchumi na kujitaja kuwa yeye ni mchumi wa grade one na aliwahi kufanya kazi BoT. 

Ningeomba kuchukuwa nafasi hii kumsaidia mweshimiwa huyu. Sifa za uwezo wa mtu, kitaaluma, huwa hazisemwi mdomoni. Zinapaswa kuonekana. People have to feel it, have to see it… it has to be felt, heard not to be said with merely words.

Wakati Lissu alielezwa kuwa ametumia maneno ya kuudhi, Nchemba alitakiwa kufuta maneno yake.

Nchemba ambaye alisema wapinzani ni waongo, wana mapepo na anashangaa kwamba Tanzania kuna watu wanawaunga mkono wakati wanapaswa wawe wanatibiwa katika hospitali ya Mirembe.

Neno pepo lilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba kumtaka alifute na yeye akasema: “Nalifuta kwa humu ndani lakini naomba wakaombewe.”

Wakati hao wakitoa lawama hizo, Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John  Komba aliwaita wapinzani vichaa ambao hawafai kuwepo bungeni bali hospitali ya vichaa ya Mirembe, iliyopo Dodoma.

“Ni vizuri mheshimiwa Mwenyekiti tukapimwa akili kabla ya kuingia humu (bungeni) ili wa kwenda Mirembe waende na wakubaki humu wabaki,” alidai Kapteni Komba wakati akibeza hoja za wapinzani za kuikataa bajeti.

Komba alisema bajeti ya mwaka huu ambayo inapingwa, wabunge wa Kenya na Uganda wamekuwa wakiipongeza.

Kilicho onekana ni mtego ambao Lissu aliutega wakati akitoa mchango wa Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani ilivyoishamulia ile ya serikali. 

Wachunguzi wa mamabo ya kisiasa nchini wanadai wabunge hao waliadhirika na kile kinachojulikana kama CHADEMAphobia (or CHADEMAhegemony).

Baadhi ya wasomi wameonyesha hofu yao kwa wabunge wa CCM na kuwashauri pia wasipokuwa makini watajikuta katika hali iliyowasibu mwaka jana wakati wa mjadala wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, ambapo baada ya KUTIFULIWA kwa hoja kabambe, wakaacha kujadili hoja mbele yao, wakaanza kumjadili mtu (Lissu), watu (CHADEMA). Complete out of point, out of touch. Igawa walishinda bungeni lakini aibu iliwapata kwenye mahakama kubwa ya watu, nje ya bunge.

Tundu Lissu alikuwa mmoja wa wachangiaji wa mjadala wa bajeti bungeni. Session ya jioni. Alisema wazi wazi kuwa wakati wa bunge la bajeti ni majira mengine kwa ajili ya masuala ya kipuuzi. Ameita it is silly season. Na hivyo Mkutano huu wa bajeti it is another silly season kwa sababu ni wakati wa kujadili mambo ambayo hayatekelezeki.

Wabunge wengi (ofcoz mnawajua) wanasimama wanasema wanaunga mkono bajeti mia kwa mia kisha wakianza kuchangia wanapinga kila kitu walichosema awali wanaunga mkono. It is another silly season. 

It is another silly season kwa sababu serikali inaleta vitu bungeni na wabunge wanajadili na wengine wanaunga mkono wakati inajulikana wazi kuwa vitu hivyo havitekelezwi.
Amesema kujadili vitu ambavyo havitekelezwi ni kujidanganya wenyewe, kudanganya watoto wetu na kuidanganya nchi hii. Ni aibu kwa kwetu kwa wabunge wote (bunge zima).

Ametolea mfano wa namna serikali ilivyoahidi katika mkutano wa bunge la bajeti uliopita kuwa wataweka trilioni 8.6 kila mwaka kwa ajili ya bajeti ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Anasema kwa sababu ya kuwa ni silly season, wabunge waliitwa Saint Gasper na Rais, wakalishwa, wakanyweshwa juu ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Lakini katika bajeti ya mwaka jana mpango huo ukatengewa trilioni 4. (something), walipohoji wakajibiwa kuwa ni mwaka wa mpito lakini itaanza rasmi mwaka huu.

Lakini mwaka huu tena mpango huo umetengewa trilioni 4.5 badala ya trilioni 8.6 kama ilivyoahidiwa. “They knew they were lying, we knew they were lying, we should be ashamed to this government, ashamed to this budget…ashamed to these Members of Parliament kwa sababu ndiyo wanaopitisha bajeti hii…(hapa Lukuvi akaingilia juu ya matumizi ya lugha za kuudhi kwa kutumia kanuni ya 64 kuwa inakataza matumizi ya lugha za matumizi na Mwenyekiti Mabumba akasisitiza).

“Mara kadhaa wamekuja hapa na kuahidi kuwa wataziba mianya ya ukwepaji kodi, watapunguza misamaha ya kodi. Lugha hizi zimekuwa za siku nyingi sana. Viongozi wa dini wamefanya utafiti na kuja na ripoti waliyoiita The 1 billlion Dollar Question…hii ni disaster ya CCM and nobody else. Mwaka 1998 Kigoda waziri wa madini, sheria ya madini ya mwaka 1998.

“Mwaka 1998 katika bunge hili wakati huo Waziri wa Nishati na Madini alikuwa Kigoda, alisema kuwa sekta ya madini itakuwa ikichangia asilimia 52 ya revenue yote inayotokana na madini. Lakini mpaka sasa tunapata on average dola milioni 100 tena katika utafiti huu wa viongozi wa dini wanasema asilimia 65 zinatokana na kodi za wafanyakazi.
“Na sasa tumepata miungu wapya wanaitwa wawekezaji…our new gods, the untouchable, kila ukigusa aah wawekezaji, ukigusa aah wawekezaji…what have they done for us? Tunaambiwa kuwa sekta ya madini ndiyo inayotoa more foreign exchange than any other…hizo fedha hizo ziko wapi

Alisema hiyo ni aibu na upuuzi na kumfanya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu, Bunge), William Lukuvi kuja juu na kusema ametoa lugha ya maudhi kinyume na taratibu za Bunge.

Advertisements

5 thoughts on “YALIYOJIRI KWA UFUPI BUNGENI KATIKA MJADALA WA BAJETI YA 2012/13 JUMATATU JUNE 18, 2012 JIONI

  1. Aisee kumbe Mwigulu Nchemba hana akili kabisa. Anahitaji kupelekwa Mirembe CCM inakufa anaamua kutupa matope Bungeni kutukana upinzani waigizaji na vichaa na eti wana pepo mtaka vyeo.

    Hasira zake nafikiri ni failure kule arumeru. Anataka kurudia yale ya Lusinde arumeru ama kweli CCM imekwisha. Ametupa bajeti ya Upinzani na kuiita rubbish

  2. Hakuna marefu yasio na ncha. Wananchi tunaelewa sana hata kama nguvu imekuwa ni chombo cha kupindisha ukweli. Kwa sasa uchafu umekuwa ukipewa nguvu za kutosha kuliko mambo ya msingi.
    Wananchi wa sasa wamepevuka kifikra na ni watafiti wazuri sana wa mambo. Hivyo basi umakini uliotukuka waitajika miongoni mwa wanasiasa hasa katika malumbano ya hoja na sio kukurupuka tu.
    Imefika kipindi wabunge tuliowapeleka bungeni kutuwakilisha wanaacha kufanya kile tulichowatuma, wanaanza kujadili watu. Sijui huko tuendako!!

Comments are closed.