MAONI YENU YA HOJA YA MUUNGANO YANAJADILIKA; WARIOBA

 • WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU, JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA

  Tume yangu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na itakusanya maoni yote na kuyaratibu, ili kupata Katiba wanayoitaka wananchi wenyewe.

 • Muswada wa kwanza ulitaja muungano kama jambo takatifu, lakini marekebisho yaliyofuatia yalibadilisha na kuweka kuwa mambo ya msingi.

 • Tume inayazingatia kwa sababu huwezi kuunda Katiba kama hakuna nchi

MWENYEKITI wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao hata kama ni ya kutaka kuvunja Muungano katika mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya. 

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja kipindi ambacho kuna vuguvugu za kutaka Zanzibar ijitenge, linalofanywa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIK), na kusababisha machafuko visiwani humo.

Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari Jumane June 19 2012 na kutangaza kuanza rasmi kazi kwa tume hiyo tangu ilipozinduliwa rasmi April 13, mwaka huu, aliweka wazi msimamo huo unaoondoa mkanganyiko katika suala hilo.

Katiba tuliyonayo inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano,” alifafanua Jaji Warioba. Kuhusu tume hiyo kufanya kazi Zanzibar kabla Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi, Jaji Warioba alisema Katiba ya Zanzibar haisemi hivyo, badala yake inaelekeza kutoa taarifa tu. 

“Utaratibu uliopo ni sheria kuwekwa mezani, ndivyo ilivyo. Sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano zinatakiwa ziwekwe mezani, Baraza haliendi kujadili bali linapewa tu taarifa,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:,  “Sheria hii ilitungwa Novemba mwaka jana na Baraza limekutana Januari mwaka huu.

Kwa utaratibu wa kawaida ilitakiwa iwekwe mezani kwenye Baraza mwezi huo, lakini kukawa na marekebisho mwezi Februari, baada ya hapo tukaipeleka. Sisi tume wala hatuna wasiwasi kwa sababu hilo limeshapita.” Kifungu cha 132 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinasema:

 “Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kifungu cha 132 (2) kinasema, “ Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.”

“Tume inafanya kazi kwa kufuata sheria. Na kwa kuwa katika mchakato ni lazima tuanze na Katiba ya sasa, kwanza wananchi waseme upungufu wake. Wananchi wako huru kupendekeza, kwa mfano, kuwepo kwa Serikali yaani Bunge na Mahakama, labda wanataka tuwe na Rais dikteta, waseme,” alisema Jaji Warioba na kuongeza: “Kuhusu Muungano, tutayapokea maoni yote. Kama wanataka mambo ya Muungano yapunguzwe, au yaongezwe, Serikali moja au mbili au wanataka tuvunje Muungano, yote tutayapokea. Tusiseme watu wamezuiwa, hakuna aliyezuiwa.” 

Akifafanua kifungu cha tisa cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayotumika katika mchakato huo, Jaji Warioba alisema Katiba haiwezi kuundwa kama hakuna nchi, ndiyo maana, suala la Muungano limewekwa kuwa la msingi.  Kifungu hicho kinazungumzia mambo ya msingi (tunu za taifa), ambayo Tume ya Katiba itayazingatia wakati wa kukusanya maoni ya wananchi.  “Muswada wa kwanza uliyataja hayo mambo ya msingi kama matakatifu, lakini marekebisho yaliyofuatia yalibadilisha na kuweka kuwa mambo ya msingi. Tume inayazingatia kwa sababu huwezi kuunda Katiba kama hakuna nchi.

Hivi karibuni visiwa vya Zanzibar na viunga vyake vyake vilikumbwa na vurugu kubwa baada ya kundi la Uamsho kufanya vurugu na kutaka visiwa hivyo vijitenge kuwa dola huru Hata hivyo, vurugu hizo zilidhibitiwa na Jeshi la Polisi, lakiniJumatatu June 18 2012 zililipuka upya na polisi kulazimika tena kutumia nguvu kudhibiti.

Advertisements

4 thoughts on “MAONI YENU YA HOJA YA MUUNGANO YANAJADILIKA; WARIOBA

 1. Kwanza; wazanzibari wana serikali ya mapinduzi na bunge lao. Sisi pia tuwe na bunge letu Dodoma wazanzibari wasiruhusiwe kabisa. Pili; liundwe bunge la muungano, kama lilivyoundwa bunge la Est Africa. Tatu; Kama wafanya kazi wote wa serikali, wabunge waende kazini jumatatu hadi ijumaa mwaka mzima isipokua wakati wa likizo tu(30 days) hatuwezi kuendelea kama bunge linakutana mara nne/tano kwa msimu ..wahamie Dodoma, wafanye kazi nawaishi kwa mshahara huu waopata hivi sasa, wasijiongezee pesa, tayari wanajilipa pesa nyingi sana. U.s congess, U.S Senate, House of Ommons etc, etc hawakutani ka msimu kuongoza nchi, kama Katiba yetu ilivyopitwa na wakati… 90% ya sheria zetu zimepitwa na wakati,tutafanya vipi mabadiliko kama bado tutaendelea kukutana kwa msimu tu….????

 2. Warioba acha kutukela ww unatumia nafasi yako ki chama na sivyo watanzania tutakavyo,Kaeni mkijua sisi mabosi wenu tumewachoka maana mmeshindwa kututumikia.

 3. Warioba acha kutukela ww unatumia nafasi yako ki chama na sivyo watanzania tutakavyo,Kaeni mkijua sisi mabosi wenu tumewachoka maana mmeshindwa kututumikia.

 4. It will quickly spread a number of years. For the more-severe,
  miliaria rubra, he gets slightly larger, red bumps or papules develop into characteristic blisters or vesicles.
  Children or adults who contract risks of heart disease are almost 10 times
  more likely to be present. Therefore, Vitamin E oil directly to the operation theatre.

  According to Kids Health, anyone can get risks of heart disease.

Comments are closed.