TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

DK. ULIMBOKA

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Imetolewa na 
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

Advertisements

8 thoughts on “TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

  1. yote waliosema madkt ni yamsingi sasa hawa serkali wanaona ugumu gani kutekeleza wakati pesa sio yao!!? pesa ni yetu siye wananchi.

  2. DAMU NI UHAI ULIO WEKWA NA MUNGU NA DUNIAN KOTE HAKUNA FORMULAR YA KUTENGENEZA DAMU.NA TWAKUMBUKA MUNGU ALITAKA KUSHUKA KUMCHAKAZA MAKONDE KAIN KWAJILI ALIMWAGA DAM YA MTU MMOJA.PANDE ZOTE MBILI TUANGALIE DAMU HIZI ZINAZO MWAGIKA ZISIJE ZIKAWA LAANA KATIKA NCHI.Nasisi tunaomba yoyote anayehusika kokote na kusababisha damu kumwagika kwaajili binafsi ABEBE LAANA YEYE KWA JINA LA YESU.

  3. malengo ya madaktari ni mazuri lakini njia waliotumia ya kutuua sisi wanyonge ndio sio sahihi. Siwezi furahi kuona ndugu yangu anakufa huku madaktari wakimwangalia halafu niwaunge mkono hata siku moja, nitawaita madaktari wa sasa ni wauaji na ni madaktari maslahi waliopoteza utu na kusaliti kiapo chao eti wakidai maslahi kwa kutuua. Siungani nao kwa njia hii, tena wasije ona wananchi wakiwachukia na kushusha heshima yao iliyokuwa imejengeka. Napenda kuwasihi madaktari kuwa njia waliotumia sio nzuri kwani itajenga chuki kwa waathirika wa mgomo hasa watakaopoteza jamaa zao. Watumie njia nyingine mbona zipo nyingi jamani.

  4. Mpo na mgomo,,,mbbona dr ulimboka mmemuhudumia..? Mngeendelea na mgomo pia….bac na raia wengine tuhudumieni pia…! Haki iwe kwa wote….mnajifanya mnalitakia mema taifa letu wakati mnatuagamiza wananchi….mmesomeshwa na kodi zetu wenyewe leo hii hamtaki kutuhudumia…njia ya madai yenu si sahihi mliyotumia.

  5. Acheni kua na ubongo mdogo wote mnao pinga mgomo….leo hii mnaona madaktari wabaya, kesho taaluma yako itaonewa na hata kua na mtu wa kukutetea na hiki ndicho kinachowapa serikali yetu dhaifu nguvu ya kuendelea kuwaonea madaktari…nakiri kwamba njia wanazotumia si sahihi sana lakini ndio njia pekee iliyopo kwaiyo wewe kama mtu mzima kaa chini tafakari, madaktari wapo tayari kupoteza uhai wao kwe maslahi yenu, je mtawapinga na kuwasema vibaya au mtawaunga mkono….hebu jengeni ukali wa haki na mchague upande ulio sahihi na unaowatakia mema ya muda mrefu sio wa muda mfupi……tukiwaunga mkono madaktari 2tatatua hili tatizo mapema zaidi na kupunguza casualties lakini 2kiendelea kuwaunga mkono mafisadi tutaumia zaidi na hilio nawaapia kabisa….madaktari ni watu wenye busara, na pale mstaarabu anapokasirika ujue kuna jambo kubwa lililomkera….bila ushirikiano wenu mgomo hautaisha na ndugu zetu wengi wataumia…..fanya uamuzi sahihi,,,,,chagua upande sahihi….jioni njema!

  6. watanzania wenzangu hasa vijana,jamani tufanyeni kazi mambo ya migomo isiyo na tija haitupeleki popote,ninyi madaktari,serikali ilishasema itaboresha sasa mnagoma nini kwani bunge la bajeti si ndo lipo bungeni jamani.mbona mnakuwa kama hamjui kwamba kila kitu ni kwa bajeti?kuweni wazalendo,mbona huko kwenye hospitali binafsi mnapofanya part time hamgomi tena mnanyenyekea kama nini.me ningekuwa mwajiri wene ningewafukuza kazi wote.

Comments are closed.