BONANZA LA WANAHABARI KUTIMUA VUMBI JULY 15 2012 MEGATRADE WACHANGIA MILIONI 2

Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Limited Bw.Goodluck Kway akiwa anamkabidhi Katibu wa chama cha Waandishi wa habari za michezo Mkoa wa Arusha Bw. Musa Juma, hundi ya shilingi Milioni mbili kama mchango wao kutoka kwa kampuni hiyo kwaajili ya maandalizi ya Bonanza.

BONANZA la saba la waandishi wa habari kanda ya kaskazini linaloandaliwa na chama cha waandishi wa habari(TASWA) yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 July 2012 katika viwanja vya General Tyre jiji Arusha yameshaanza ambapo Megatrade wamejitokeza kudhamini mashindano hayo.

Akizungumza  jijini Arusha katika makabidhiano na waandishi wa habari Meneja biashara wa kampuni ya Megatrade Investment Limited Bw.Goodluck Kway alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kudhamini bonanza hilo kupitia kinywaji chake cha K Vant GIN, kwakuona umuhimu wa vyombo vya habari hapa Nchini

Bw.Kway alisema kuwa wao kama kampuni wanajiskia furaha sana kudhamini tamasha hilo ikiwa ni mchango kwa wanahabari wote  huku akidai kuwa katika bonanza lingine watajaribu kudhamini kwa kiasi kikubwa zaidi

“Leo hapa tunakadidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milion 2, nikidogo lakini najua kitaweza kuwapiga jeki kamati ya maandalizi ya bonanza hilo”Alisema Bw.Kway

Kwa upande wake Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo Mkoa wa Arusha Bw.Musa Juma aliishukuru kampuni hiyo kwa kuweza kuwadhamini katika bonanza hilo litakalo washirikisha wanahabari wa kanda ya kaskazini

Alisema kuwa kampuni hiyo ya Megatrade Investment Limited imeweza kuwakabidhi hundi ya shilingi milioni 2 kama mchango wao huku akitaja makampuni mengine yaliyodhamini kuwa ni kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ndio mdhamini mkuu, Tanapa, Ngorongoro na Alfa Tel

Bw.Musa alisema kuwa lengo hasa  la tamasha ni kuburudisha,kujenga mwili,kujenga mahusiano kwa wanahabari na wadau  mbalimbali ikiwa ni kukuza utalii Mkoani Arusha

Alitoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini bonanza hilo ili kuweza kufanikisha na wao waweze kutoa zawadi zenye ubora ili wanahabari waweze kujitokeza kwa wingi katika nyanda za michezo

Advertisements