WANANCHI, WANAHABARI, MADAKTARI, WANANCHI UKWELI NI UPI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI? HEBU TAZAMA TASWILA YA MUHIMBILI JUMATANO JULY 4, 2012

 • KAMA NI PROPAGANDA NI KWA FAIDA YA NANI NA WATU WANAZIDI KUFA.

 • WAANDISHI WANAOHUSIKA WANAFANYA HIVYO KWA MANUFAA YA NANI?

 • MIMI NA WEWE TUNAFANYA NINI ILI KURUDISHA HUDUMA YA AFYA? TUENDELEE KUPIGA SIASA AU TUTOE MAONI YA SULUHU?

 • HEBU TAZAMA JENGO LA WATOTO! LIPO JEUPE… HII INAMAANA WATOTO WATAKUWA WANAKUFA TU. MUHIMBILI AMBAYO WATU WALIKUWA WAKILALA HADI SAKAFUNI LEO IMEGEUKA GHOST HOSPITAL NA BADO KAMATI YA ULINZI NA USALAMA DAR WANASEMA HUDUMA ZINARIDHISHA!!!!

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  PICHA ILIYOPIGWA SIKU YA JUMATANO JULY 4, 2012 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PICHA NA HISANI YA MO BLOG

  OUR TAKE; Inakatisha Tamaa! Ni habari gani ya kweli? Au tumwamini nani tena? Ni chombo gani huru kwa sasa kinachoweza kuripoti ukweli na kutanguliza utaifa kwanza! Au  mpaka pale tutaheshimiana na kuthaminiana kama wanadamu ndipo kila mmoja wetu ataweza kujivunia utaifa wake!!

  Hii haikubaliki kabisa…. Kwa picha hizi na taarifa ya serikali kuwa mgomo umekwisha Napata hisia kuwa Sasa Tanganyika hatuna budi kujivunia mafanikio tuliyoyoyapata kwa upande wa AFYA kama tumeweza kutokomeza maradhi kiasi cha wodi zote kubaki tupu!!!! pongezi sana kwa serikali yetu japo mnaikejeri mnasema ni DHAIFU. Sasa mmejionea wenyewe, na baada ya mafanikio haya kwa upande wa AFYA sasa nguvu zetu zote tunazielekeza kwenye ELIMU. 

Advertisements

8 thoughts on “WANANCHI, WANAHABARI, MADAKTARI, WANANCHI UKWELI NI UPI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI? HEBU TAZAMA TASWILA YA MUHIMBILI JUMATANO JULY 4, 2012

 1. hii imenigusa sana. Lakini tumshukuru mungu kwa kila jambo na tuzidi kumwomba ili atunusuru na hali mbaya sana inayotukabili. Kimsingi wanaoumia ni sisi wananchi hasa wale walala hoi. Ni wazi kuwa madaktari wanadai haki ya msingi sio tu kwa wao wenyewe bali kwa taifa zima pia. Tuombe kwa nguvu hii mambo ipite japo twaumia. Mungu wa miungu na atupiganie.

 2. ohhh!my GOD what does this mean,hizi propaganda hata shetani alikua akizifanya pindi mungu alipo mtuma MUSA kwenda kuwakomboa wana wa ISRAEL,pale mungu alipoonesha miujiza yake kwa farao,shetani naye akapeleka vimiujiza vyake uchwara ili kumpa kiburi farao kuwa nae anaweza,sasa haya ndo yanayofanywa na serikali kuaminisha watu kua imesikilizwa kumbe HOLA!!!!!!!!!!!!!!

 3. Jeuri, dharau, unafiki na uroho wa viongozi wa Tanzania ndiyo itakayoliangamiza Taifa letu. Haiingii akilini watu wanadai kuboreshwa kwa mazingira ya utoaji wa huduma muhimu kama afya na elimu; wanatokea viongozi wachache tena kwa kiburi na jeuri wanasema hakuna fedha ama liwalo na liwe lakini wanakuwa na jeuri ya kusema wanaodai waondoke kwani wana fedha za kutosha kuagiza madaktari wa nje ama kuingia ubia na hospitali binafsi. Hivi kwa uelewa wao finyu wanafikiri hospitali binafsi wanapata wapi madaktari kwa ajili ya shughuli zao.

  Nafikiri imefika wakati Watanzania tuoneshe umoja wa hali ya juu kwani kiburi cha hawa viongozi ni matokeo ya kugawanyika kwetu na uhuru walioachiwa katika kukomba rasilimali za Taifa letu. Leo hii tunaambiwa kuwa kuna viongozi wanamiliki mabilioni na matrilioni ya shilingi kwenye akaunti za nje lakini watanzania wanakufa kwa kukosa madawa ama huduma nyingine za msingi kama elimu na maji.

  Rais wa nchi anasafiri kiholela na msafara wa watu zaidi ya hamsini pasipo kufikiri hali ya wananchi wake; rais kama huyo atakuwa na huruma kwa wananchi wake kweli?? Gharama kwa safari moja ya rais ingeweza kuboresha huduma ya zahanati ngapi hapa Tanzania.

  Hata pale wanapougua wao huwahishwa India na kwingineko kwa ajili ya kupata huduma ya daraja la kwa tena kwa gharama ya fedha za walipa kodi, mtanzania mnyonge atapata wapi huduma kama hiyo kama sio kuishia kwenye miti shamba na kwenye vikombe kama ilivyotokea Samunge huko Loliondo.

 4. Watanzani sote ni watu wa mizaa sana hatujui kuchukulia mambo kwa uzito tena hili wanalijua viongozi wetu ndiyo mana wanafanya wapendalo

 5. KWELI HALI INATISHA LAKINI SERIKALI IFANYE NINI WAKATI IMEWASOMESHA MADAKTARI KWA GHARAMA KUBWA SANA NA WENGI BADO HAWAJALIPA MKOPO WALIOKOPESHWA NA SERIKALI WAKATI WAPO ELIMU YA JUU. NAVYOJUA KAZI YA UDAKTARI NI WITO NA DAKTARI ANATAKIWA AWE NA HURUMA KWA MGONJWA MAANA NDIYE ANAYEJUA UKUBWA WA TATIZO. LAKINI CHA AJABU HUYO DR NDIYE WA KWANZA KUTUMIA MATATIZO YA WAGONJWA KAMA FIMBO YA KUIKOMOA SERIKALI. HIVI KWA MAELEZO YA MH RAIS JUU YA MATAKWA YA MADAKTARI NCHI INAWEZA KUTEKELEZA HILO? LEO MADAKTARI WANADAI WABORESHEWE MAISHA YAO KWA KUPATA MSHAHARA MKUBWA NA POSHO KIBAO HADI KUFIKA MILIONI 7.7. KESHO WALIMU NAO WATAANZA, MANESI NA VYOMBO VYA DOLA. MAANA KAMA IMEWEZEKANA KWA MADAKTARI KWA NINI ISIWEZEKANE KWA WENGINE? JE YAWEZEKANA WOTE TUWE MADAKTARI? KILA MMOJA NI MUHIMU KWA NAFASI YAKE. NASAPOTI MSIMAMO WA SERIKALI KUKATAA KUBURUZWA NA MADAKTARI. WASHTAKIWE KWA KESI YA MAUAJI KWA KUSABABISHA VIFO VYA WENGI KWA SABABU YA MGOMO WAO NA WAKITIWA HATIANI WANYONGWE KABISA.

Comments are closed.