AFYA YA DK. ULIMBOKA YAZIDI KUZOROTA.

Dr Stephen Ulimboka in intensive care at Muhimbili Orthopaedic Institute yesterday after he was kidnapped, tortured and dumped on the outskirts of Dar es Salaam on Wednesday PHOTO FIDELIS FELIX

 • NI KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU TU NDIZO TUNAZO SUBIRI….

 • YAELEZWA BADO YUKO CHUMBA CHA WAGONJWA MAUTUTI.

 • MPAKA SASA AJITAMBUHI.

 • MADAKTALI WAANGAIKA KUCHANGISHA MICHANGO.


Taarifa za kuaminika sinaeleza kuwa hali  ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hapa nchini, Dk. Stephen Ulimboka, inazidi kuzorota na sasa amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika hospitali anakotibiwa huko Afrika Kusini,  madaktari walio karibu naye wamesema kuwa sasa wanasubiri ‘Kudra’ za Mwenyezi Mungu’ tu.

Kiongozi huyo ambaye alitekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita anatibiwa katika hospitali nchini Afrika Kusini ambayo hadi sasa haijawekwa wazi.

Taarifa za Dk Ulimboka kuwa mahututi zilianza kupatikana siku ya Ijumaa Julai 6, 2012 lakini hakuna daktari yeyote aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo na kila aliyekuwa akiulizwa kujibu kuwa taarifa hizo zilikuwa uvumi tu.

 “Asubuhi wote tulisikia kwamba hali yake (Dk Ulimboka) ni mbaya na yuko kwenye ‘koma’, lakini taarifa hizo sijazithibitisha kujua zina ukweli kiasi gani,” alisema Kiongozi wa jopo la madaktari linaloshughulikia matibabu ya Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahama Ijumaa Julai 6, 2012 huku Katibu wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila akisema alikuwa haelewi uvumi huo ulitoka wapi kwani yeye hakuwa na taarifa hizo.

Jumamosi Julai 7, 2012 Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage alithibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa Dk Ulimboka yuko mahututi.

Dk Ulimboka alisafirishwa baada ya jopo la madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lililokuwa likimtibu kutoa ripoti ya kubadilika ghafla kwa afya yake na kushauri asafirishwe nje kwa ajili ya vipimo na matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini.

kiongozi huyo wa Jumuiya ya Madaktari hapa nchini aliyelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi yumo katika ‘koma’, ambayo ni hali ya nusu mfu – nusu hai, na anahitaji zaidi sala za Watanzania. Dk. Chitage alimweleza mwandishi wetu.

“Taarifa tulizonazo ni kuwa hali ya mgonjwa bado si nzuri na amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, huwezi kusema anaendelea vizuri, jambo muhimu hapa ni kumwomba Mungu awaongezee maarifa madaktari wale ili kupigania uhai wa mwenzetu.” alisema Dk Chitage huku akionyesha kukata tamaa.

Taarifa kuhusu Dk Ulimboka pia zilithibitishwa na Dk Mkopi akisema: “Kwa leo sijawasiliana na ndugu yake moja kwa moja, lakini habari nilizonazo ni kuwa hali yake bado siyo nzuri.”

Inadaiwa Dk. Ulimboka amepata madhara makubwa katika figo zake ambapo ilidaiwa moja ilipata ufa na nyingine iligoma kufanya kazi, baadhi ya mbavu zake zimepata majeraha.
Kichwa cha daktari huyo pia kilipata hitilafu kutokana na kipigo hicho kinachodaiwa kufanywa na maofisa Usalama wa Taifa ingawa serikali imekana kuhusika na kitendo hicho cha kinyama.

Katika hatua nyingine, madaktari wanaendelea kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Dk Ulimboka na katika awamu hii ya pili, imeelezwa kuwa takriban Dola za Marekani 30,000 zinahitajika.

Dk Mkopi alikiri madaktari hao kuendelea kuchangishana lakini hakuwa tayari kueleza kiasi ambacho kimepatikana mpaka sasa.
Advertisements

3 thoughts on “AFYA YA DK. ULIMBOKA YAZIDI KUZOROTA.

 1. tutamwombeaje wakati yeye ndiyo anayeshabikia watu kufa?? maana yeye anashinikiza mgomo wakati akijua impact ya huo mgomo ni idadi kubwa ya watu kufa, sasa inakuwaje leo mseme watanzania wamuombee.muombeeni wenyewe.

 2. Sina hakika kama mimi ni mtu sahihi wa kujibu hoja yako dada yangu Mariah! lakini kwa ufaham wangu mdogo tusipotoshwe na baadhi ya vyombo vya habari au kauri za upande mmoja.

  Binafsi mimi sipendi au hakuna mtu anye furahia mgomo wa madaktari. kwasababu ni sisi pamoja na ndugu zetu ndiyo wanao teseka kwa kukosa uduma.

  Lakini dada yangu Mariah! tujiulize tena bila ushabiki uduma ambazo zinatolewa katika hospitali zetu ni sahihi? na ninani anaye paswa kupigani kuboreshwa kwa uduma hizo. inawezekana ukaboresha uduma za Afya bila kuwajari watoa uduma hizo? kama na pamoja na madai haya muda mrefu ya kuomba huduma hizi ziboreshwe bila mafanikio kipi kifanyike.

  bila kuegemea upande wowote najua tutateseka sana kama mgomo huu ukiendelea lakini nafikili hatuna njia nyingine mbadala ya kuishindikiza serikali hii ituboreshe hali ya uduma za afya.

Comments are closed.