ARUSHA YAMULIKWA NA JICHO LETU.

Jicho Letu lilipoamua kuzungukia jiji la Arusha pamoja na viunga vyake lilikumbana na kadhia pamoja na taswira ya kustua, Jicho likabaki katika hali ya sintofahamu na kujiuliza je hili ndilo lile jiji la kitalii linalo pendekezwa kuwa makao makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki?

TASWIRA YA MITARO KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Awali Jicho lilisikia sifa ya Jiji hili zikivuma kuwa sehemu hii ni Geneva ya Afrika. Jicho Letu likaamua kufunga safari kuzuru Jiji hili lisilo na Madiwani wala Mbunge.

SEHEMU YA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA IKIONYESHA TASWIRA YA UCHAFU ULIVYO TAPAKA JUMATATU JULAI 9, 2012

Safari ya Jicho Letu ilianzia Kituo cha mabasi!  Mazingira ya Kituo Kikuu cha mabasi yalilishangaza Jicho Letu, hali ya uchafu wa kupindukia, chupa zilizo tapakaa harufu za mikojo zilitosha kuliaminisha Jicho kuwa wale waliosema kuwa jiji la Arusha ni Genever ya Afrika walisema hivyo kwasababu za kisiasa tu.

SEHEMU YA VIJANA WANAO SHINDA BILA KAZI KATIKA MAENEO YA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA HUKU MALI YA UCHAFU IKIONEKANA WAZI WAZI JUMATATU JULAI 9, 2012

Uchunguzi wa Jicho Letu uligundua pamoja na uchafu ulio tapakaa vilevile katika Kituo hicho kuna vijana wengi wasio na kazi maalum bali hushinda maeneo hayo wakivuta bangi hadharani bila ya vyombo husika kuwachukulia  hatua stahiki. Jicho lilistaajabu pale lilipo waona askari wakipita na kuvifumbia macho vitendo hivyo…. Hapo Jicho Letu likapata taswira huwenda pia askari hao walikuwa likizo au nao ni watalii.

MAMA LISHE WAKIWA WANAFANYA BIASHARA KATIKA SEHEMU HATARISHI ZA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Pamoja na uchafu huo kutapakaa sehemu hii ya Kituo cha mabasi yaendayo mikoani Jicho Letu liliwakuta Mama Lishe wakitoa huduma za vyakula katika mazingira hatarishi bila kuhofia magonjwa ya mlipuko kutokana na mazingira ya uchafu hali iliyotishia afya za walaji.

Jicho lilipata bahati ya kuongea na Mwananchi mmoja ambaye aliliambia jicho hili kuwa hali ya uchafu katika maeneo hayo imezidi kuchukuwa kasi huku halmashauri husika ikionyesha kushindwa kabisa kuidhibiti hali hii.

Kwa upande wao Mama Lishe hao wanadai kuwa wamekuwa wakiilipa halmashauri ya Jiji la Arusha fedha za kuuzia eneo hilo zinazochukuliwa na kampuni inayokusanya ushuru wa geti na magari yanayoingia na kutoka katika Kituo hicho.

WACHUHUZI WAKIWA WANAENDELEA KUFANYA BIASHARA ZAO MAENEO YA KANDO KANDO MWA BARABARA KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Jicho Letu liliamua kutoka maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi, njiani lilishindwa kujuwa kama liko Arusha au liko jijini Dar es Salaam tena kipindi kile ambacho mtaa wa kongo ulikuwa maarufu.

jicho Letu liliwaona wafanyabiashara alimaarufu machinga wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya maduka hali inayofanya msongamano katika barabara kadhaa za jiji hili na mabaraza ya maduka. Jicho Letu lilipata kadhia pamoja na kuwa lilikuwa linatembea kwa miguu.

Wafanyabiashara pamoja na wananchi wameitupia lawama halmashauri yao kwa kushindwa kutatua tatizo hili. Wengine walidai kuwa chombo hicho kinaogopa kuchukuwa hatua za kisheria kutokana na sababu za kisiasa huku ikitoa visingizio Lukuki bila ya majibu yakinifu.

TASWIRA YA MBELE YA SOKO KUU LA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Jicho Letu lilipofika Soko Kuu lilikaribishwa na rundo la taka, Jicho Letu liliendelea kustaajabishwa na rundo hili la takataka zilizopo pembezoni mwasoko.

Uchafu umerundikana na kufanya sehemu hii muhimu yanapo patikana maitaji muhim ya kila siku kwa wakazi wa jiji hili kuwa hatarishi na kero kubwa kwa wafanya biashara pamoja na wanunuzi.

Katika hali ya kushangaza Jicho Letu lilimuona kijana mmoja wa makamu akiwa amejipumzisha katikati ya rundo hilo la taka, bila kujari harufu kari iliyokuwa inajitokeza sehemu hiyo yeye aliendelea kulala usingizi. Jicho letu halikufanikiwa kupata jina lake wala muda wa kuongea nae.

MMOJA WA WAFANYABIASHARA YA MBOGOMBOGA AKIWA AMEPANGA BIDHA ZAKE CHINI KATIKA SOKO KUU LA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Katika maeneo hayo ya Soko Kuu Jicho Letu liliwakuta wakinamama wakipanga bidhaa zao chini hali inayohatarisha mazingira ya walaji.

Taswira hizi zililifanya Jicho letu kuchoka kutazama! Lika amua kwenda kujipumzisha na kupanga kurudi siku nyingine katika jiji hili lenye sifa nyingi.

Njiani Jicho Letu likawa lina tafakari matokeo ya uchunguzi wake, hasa pale lilipo ambiwa Halmashauri hiyo ya jiji la Arusha kwasasa imejikita kushughulikia ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali (CAG), Jicho Letu lika jiuliza je? Bwana afya anafanya kazi yeke kweli?

KITUO KIKUU CHA MABASI CHA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012

Likapanga likipata muda tena wa kutazama lazima litatembelea ofisi za wakuu hao. Hali hii ya kutelekezwa jiji hili ni moja ya taswira mbaya na ya kukatisha tama ambayo Jicho lime jione Mwezi huu.

Advertisements

One thought on “ARUSHA YAMULIKWA NA JICHO LETU.

  1. Kweli ni jiji letu ndiyo maana tunakuwa na uwezo wa kutupa taka hovyo. Kama ni buffer hiyo ni stater tu main course inakuja ndani ya jiji lakini kwenye vimitaa vyake. Coming soon…

Comments are closed.