KIKWETE ATEMBELEA KAMBI YA EDO NA KUJINASIBU KUTOA KIFUTA JASHO CHA NG’OMBE 1500 KILA MWEZI KWA WANANCHI.

Rais Jakaya Mrisho kikwete akizindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jashp cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009

SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Ahadi hiyo imetolewa, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ng’ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na na ukame mwaka 2008/2009 ambapo walipoteza mifugo yao yote. Hafla hii imefanyika leo Monduli. Picha na Ikulu.

Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.

Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo

Advertisements

HATIMAE TAKUKURU YABUNI MBINU MPYA ZA KUWASHITAKI MUNGAI NA MWAKALEBELA

MUNGAI ALIPO PANDISHWA KIZIMBANI NA TAKUKURU  KWA MARA KWANZA
TAASISI ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa inajipanga upya kumfikisha Mahakamani aliyekuwa waziri katika wizara mbali mbali kwenye awamu tofauti katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai ili kujibu mashitaka ya kujihusisha na rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2010.
 
Kaimu Mkuu wa Takukuru Iringa, Stephen Mafipa alipoongea na vyombo vya habari alisema taasisi hiyo inafanya utaratibu wa kumfikisha Mheshimiwa Mungai Mahakamani ili kujibu mashitaka baada ya mahakama Kuu Kanda ya Iringa kupitia kwa Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo Sekieti Kihio kutupilia mbali rufaa yake.
 
Awali Mungai alikata rufaa akiiomba mahakama kuu kutupilia mbali uwamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa yaliyofanywa na Mheshimiwa Marry Senapee Tarehe 31 January.
Mungai alikuwa akitetewa na mawakili wawili Basiri Mkwata na Alex Mgongolwa ampapo walidai kuwa Mungai hakuwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashitaka kukosea hati ya mashitaka lakini mahakama hiyo ikutoa ruhusa ya kubadirishwa hati ya mashtaka kitendo kilishopingwa na jopo la mawakili hao.
katika hati ya rufaa mawakili wa Mungai aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi na kisha kutolea maamuzi hoja nyingine ambazo hazikutolewa maamuzi na mahakama hiyo ya hakimu mkazi, 
Mawakili hao walidai kuwa katika makosa yote 15 ya kutoa rushwa ambayo Mungai alikuwa akishitakiwa nayo yalikuwa siyo makosa ya jinai kwa kukosa maneno muhimu kisheria kama inavyotakiwa katika kifungu cha 15 (1)(b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mafipa amefafanua kuwa kifungu cha 21(1) (a) na kifungu cha 24 (8) cha sheria ya gharama za uchaguzi, sheria namba 6 ya mwaka 2010. ambayo mheshimiwa Mungai na wenzake walishitakiwa nayo kilikuwa hakitengenezi kosa la jinai kisheria .
MWAKALEBELA NA MKEWE WALIPO PANDISHWA MAHAKAMANI KWA MARA YA KWANZA NA TAKUKURU
Aidha taasisi hiyo inakusudia kumkamata na kumfikisha mahakamani aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchini TFF Fredrick Mwakalebela ili kujibu kesi kama hiyo ya rushwa ya uchaguzi mwaka 2010 baada ya rufaa yake inayofanana na ya mheshimiwa mungai kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Iringa siku chache zilizopita.
Mungai na mwakalebela walikuwa wagombea ubunge katika majimbo ya mufindi kaskazini na Iringa mjini ambapo wote wanatuhumiwa kuwa walitumia ushawishi wa rushwa kwa wapiga kura katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi ccm.
Habari hii imeandikwa kwa msaada wa http://www.jodanyp.blogspot.com/

WANANCHI WAJITOKEZA KUUZIKA MWILI ULIOSUSWA

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Burka kata ya Olasiti Mkoani Arusha Bw.Ishmail Losilale(aliyevalia nguo nyeusi)akiwa anatoa heshima ya mwisho katika ibada ya mazishi ya kumuaga Bi.Frola Magesa Mkala baada ya wananchi wa Burka kuchukua jukumu la kumzika kutokana na ndugu zake kutojitokeza

Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa burka kata ya Olasiti Bw.Ishmail Losilale katika ibada ya mazishi ya kumuaga Bi.Flora Magesa Mkala kilichotokea siku ya tarehe 23/7 mwaka huu katika hospitali ya Mt.Meru Mkoani Arusha ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua

Wananchi wakiwa wanapata chakula katika msiba

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwili huo wa marehemu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti kwa takribani siku saba kutokana na jamaa na ndungu zake kutojitokeza hali ambayo ilisababisha wanakiji wa Burka kuchukua uhamuzi wa kuuzika mwili huo katika makaburi ya JR yaliyopo Mkoani Arusha

Bw.Losilale aliwashukuru sana wananchi wa burka kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuuzika mwili huo huku akimtaja marehemu kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyependa kushirikiana na jamii katika majuku mbalimbali

Kwaupande wake Bi,Aisha Yoram ambaye alikuwa anaishi na marehemu kabla ya mauti hayajamkuta alisema kuwa alikaa na marehumu kwa muda wa wiki mbili ndipo alipoanza kuumwa na wakamkimbiza hospitalini

“Kweli siwajui ndugu zake na alishawahi kuniambia kuwa yeye hapa Arusha hana ndugu hata mmoja na hapa kwangu alikuja tu na nguo aliyokuwa amevalia akawa ananisaidia shughulu za nyumbani,,,,kiufupi alikuwa nia mtu ambaye hakuwa na makazi maalumu”alisema Bi.Aisha

Mchungaji Charles Gabriel wa kanisa la The New Pentecoste akiwa anafanya sala kabla ya kutoa neno la Mungu

Naye Mch.Charles Gabriel wa kanisa la The New Pentecoste katika mahubiri yake aliwaasa waajiri kuchukua jukumu la kujua wafanyakazi wao wanaishi wapi na pia kujua kama wanandugu karibu ili tatizo linapotokea waweze kujua ni namna gani wanaweza kulitatua kwa haraka

“Hizi ni nyakati hatari sana unapokaa na mtu au mfanyakazi wa ndani chuguza kwao ni wapi au ndugu zake wako wapi,,,kwa hili la leo hapa ni fundisho kwetu”Alisema Mch.Charles

Hadi zoezi la mazishi lilipokamilika nguo wala vitu vya marehumu havikupatikana kutokana nay eye kutokuwa na makazi maalumu.