WANANCHI WAJITOKEZA KUUZIKA MWILI ULIOSUSWA

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Burka kata ya Olasiti Mkoani Arusha Bw.Ishmail Losilale(aliyevalia nguo nyeusi)akiwa anatoa heshima ya mwisho katika ibada ya mazishi ya kumuaga Bi.Frola Magesa Mkala baada ya wananchi wa Burka kuchukua jukumu la kumzika kutokana na ndugu zake kutojitokeza

Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa burka kata ya Olasiti Bw.Ishmail Losilale katika ibada ya mazishi ya kumuaga Bi.Flora Magesa Mkala kilichotokea siku ya tarehe 23/7 mwaka huu katika hospitali ya Mt.Meru Mkoani Arusha ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua

Wananchi wakiwa wanapata chakula katika msiba

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwili huo wa marehemu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti kwa takribani siku saba kutokana na jamaa na ndungu zake kutojitokeza hali ambayo ilisababisha wanakiji wa Burka kuchukua uhamuzi wa kuuzika mwili huo katika makaburi ya JR yaliyopo Mkoani Arusha

Bw.Losilale aliwashukuru sana wananchi wa burka kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuuzika mwili huo huku akimtaja marehemu kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyependa kushirikiana na jamii katika majuku mbalimbali

Kwaupande wake Bi,Aisha Yoram ambaye alikuwa anaishi na marehemu kabla ya mauti hayajamkuta alisema kuwa alikaa na marehumu kwa muda wa wiki mbili ndipo alipoanza kuumwa na wakamkimbiza hospitalini

“Kweli siwajui ndugu zake na alishawahi kuniambia kuwa yeye hapa Arusha hana ndugu hata mmoja na hapa kwangu alikuja tu na nguo aliyokuwa amevalia akawa ananisaidia shughulu za nyumbani,,,,kiufupi alikuwa nia mtu ambaye hakuwa na makazi maalumu”alisema Bi.Aisha

Mchungaji Charles Gabriel wa kanisa la The New Pentecoste akiwa anafanya sala kabla ya kutoa neno la Mungu

Naye Mch.Charles Gabriel wa kanisa la The New Pentecoste katika mahubiri yake aliwaasa waajiri kuchukua jukumu la kujua wafanyakazi wao wanaishi wapi na pia kujua kama wanandugu karibu ili tatizo linapotokea waweze kujua ni namna gani wanaweza kulitatua kwa haraka

“Hizi ni nyakati hatari sana unapokaa na mtu au mfanyakazi wa ndani chuguza kwao ni wapi au ndugu zake wako wapi,,,kwa hili la leo hapa ni fundisho kwetu”Alisema Mch.Charles

Hadi zoezi la mazishi lilipokamilika nguo wala vitu vya marehumu havikupatikana kutokana nay eye kutokuwa na makazi maalumu.

Advertisements