MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI WAKIKALIA VIBAYA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA.

 

RAIS WA CHAMA CHA WALIMU NCHINI (CWT), GRATIAN MUKOBA, AKIINGIA MAHAKAMANI ALHAMISI AGOSTI 2 2012.
  • WAUTAKA UONGOZI WA CHAMA CHA WALIU TANZANIA KUTOA TAARIFA YA KUSITISHA MGOMO KWA WANACHAMA WAKE.

  • WASEMA CHAMA HICHO KILIPE GARAMA  NA KUFIDIA HASARA ILIYOPATIKANA KUTOKANA NA MGOMO HUO

  • NOTIS YA KUGOMA ILIYOTOLEWA NA CWT JULAI 27 MWAKA HUU SAA TISA ALASIRI WAKATI ZOEZI LA UPIGAJI KURAA ZILE LILIKUWA BADO HALIJAFANYIKA NA KWASABABU HIYO ZOEZI LILE LIMEKUWA BATILI: 

 

 Jaji Sophia Wambura wa Mahakama Kuu Divisheni ya kazi ya jijini Dar es Salaam, amesema mgomo wa walimu ni batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha heria ya Ajira na Mahusuano ya kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa dhamila mbaya, alitoa uamuzi huo Alhamisi Augost 2 2012 saa 9:14-37 alasiri huku ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo ukiwa umefurika walimu katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini. 

 

WANASHERIA WA SERIKALI WAKIWASILI MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI JIJINI DAR ES SALAAM ALHAMISI AGOSTI 02 2012 KUSIKILIZA UAMUZI WA MAHAKAMA.

Jaji Wambura alisema amesikiliza kwa makini hoja za mawakili waandamizi wa upande wa serikali Pius Mboya na Obadia Kameya ambao walikuwa wakiwawakilisha walalamikaji katika maombi hayo madogo namba 96/2012 yaliyoletwa chini ya hati ya dharula na Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku mlalamikiwa akiwa ni Chama cha Walimu Tanzania(CWT) ambao walikuwa wakiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Gabriel Mnyele. 

 

Jaji Wambura alisema mgogoro uliowasilishwa mbele yake na walalamikaji ni kwamba wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa mgomo wa walimu ni batili wakati wakili wa CWT, Mnyere alidai mgomo huo ni halali kwa sababu umekidhi matakwa ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WALIMU NCHINI (CWT) EZEKIEL OLUOCH AKIWASILI MAHAKAMANI ALHAMISI AGOSTI 02 2012

 

Jaji huyo alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kutofautiana na zoezi la upigaji kura za kuunga mkono mgomo ambalo liliendeshwa na CWT ambapo asilimia 97 ya walimu waliinga mkono kuanza kwa mgomo kwasababu zifuatazo:

  • Zoezi la upigaji kula lilikuwa likiwadanganya wanachama wa CWT kuwa zoezi hilo limeendeshwa rasmi na kwa mujibu wa sheria, zoezi lile halikukidhi matakwa ya sheria kwasababu wanachama wake walikuwa hawajaelewa na viongozi wa chama hicho madhara ya kufanya mgomo huo, zoezi lile halikufuata taratibu; 
  • Notis ya kugoma iliyotolewa na CWT Julai 27 mwaka huu saa tisa alasiri wakati zoezi la upigaji kura zile lilikuwa bado halijafanyika na kwasababu hiyo zoezi lile likikuwa batili: 
  • Kwa mdaiwa(CWT) kushindwa kufuata matakwa ya kifungu cha 42 na 43 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,ni wazi taratibu zote walizozifanya za kupiga kura ya kuunga mkono mgomo na kugoma mdaiwa alizifanya akiwa na dhamila mbaya kwani wajumbe wa chama hicho hakuwa na makubaliano ya jinsi mgomo utakavyoendeshwa na kusimamiwa”alisema Jaji Wambura huku baadhi ya walimu wakiwa wamejiinamia. 
  • Alisisitiza kuwa CWT imeitisha mgomo huo ikiwa na dhamira mbaya kwasababu ni CWT ndiyo alikataa kuendelea na mazungumzo na mwajiri wake badala yake akaanzisha mgomo wakati Julai 27 mwaka huu, pande zote katika hizo zilifika mbele yake kuomba na upande wa mlalamikaji ukaomba mahakama itoe amri ya kutaka pande zote zisiendelee na jambo lolote hadi mahakama itakapowasilikiliza lakini cha kushangaza siku hiyo hiyo saa tisa alasiri CWT ilienda kutoa noti ya kuanza mgomo kwa walimu nchi nzima ndani ya saa 48 wakati kulikuwa na amri ya mahakama iliyozitaka pande zote kutoendelea kufanya jambo lolote linalohusiana na kesi hiyo ambapo mgomo huo batili ulianza rasmi nchi nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii na hadi sasa unaendelea.

 

SEHEMU YA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WALIMU WAKIWASILI MAHAKAMANI

Kwa maelezo hayo nasisitiza mgomo huo ni batili kwani haujakidhi matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka,na mgomo uliondeshwa kwa siku tatu sasa ni batili na ninaamuru mgomo huo usitishwe mara moja na walimu wote warejee kazini na kwa kuwa mdaiwa aliitisha mgomo huo kwa mkutumia taarifa kwa vyombo vya habari pia naamuru kiongozi aliyetoa taarifa hiyo ya mgomo aende tena kwenye vyombo vya habari akatangaze kuwa mgomo waliokuwa wakiufanya ni batili na kuwataka walimu warejee kazini mara moja na mahakama hii imemshangaa sana wakili Mnyere kwa kushindwa kuwashauri wateja wake mapema kwamba mgomo waliokuwa wakiundesha ulikuwa umekiuka sheria” alisema Jaji Wambura.

 

VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI PAMOJA NA WALIMU WAKIWA MAHAKAMANI ALHAMISI AGOSTI 02 2012 WAKISIKILIZA KWA MAKINI HUKUMU YAO JUU YA MGOMO

Aidha pia naiamuru CWT kulipa gharama na fidia kwa kipindi chote ambacho wanafunzi wamekosa vipindi kwaajili ya mgomo huo batili na kama pande zote zinaona kuna ulazima wa kurudi mezani kwa majadiliano zilirudi kwenye meza ya majadiliano na zimualike mtaalamu wa sheria za kazi awasaidie kufikia mwafaka.

 

WANASHERIA WA SERIKALI WAKIFWATILIA KWA MAKINI MWENENDO WA KESI ALHAMISI AGOSTI 02 2012

Baada ya hukumu kutolewa,baadhi ya viongozi wa CWT waliwaomba waandishi wa habari waje nje ya mahakama kwani kutakuwa na mkutano lakini hata hivyo waandishi walipofika nje ya viwanja hivyo mahakama walimkuta Rais wa chama cha walimu,Gration Mkoba akiwa amenyongonyea na hata alipotakiwa atoe tamko ni lini atatekeleza amri ya mahakama iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari autangazie umma kuwa mgomo alioutisha ni batili na awatake walimu warudi kazini alishia kusema Ijumaa August 3 2012  atafanya mkutano na waandishi wa habari na kwa upande wa wakili wao Mnyere alisema amekubaliana na uamuzi huo wa mahakama.

Advertisements

2 thoughts on “MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI WAKIKALIA VIBAYA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA.

  1. Binafsi nadhani maamuzi yanaweza yakawa sahihi, ila kikubwa ni kuwa maamuzi yalilenga haswa taratibu zilizofanyika hadi kufikia mgomo na si kuhusu walimu wanahaki ya kudai au hawana. Hivyo serikali itazame hili pia kuwa kuna umuhimu wa kukaa na kusikiliza madai ya malipo ya walimu ambayo yanatokana na haki za kikatiba yaani haki ya kufanya kazi na haki ya kupata malipo sawa sawa na kazi iliofanyika.

  2. Mr. Mduma! inamaana chama cha walimu walishauliwa vibaya na Mwanasheria wao kuhusu hatua za kufuata katika kutekereza mgomo wao?

Comments are closed.