HATIMA YA WATANZANIA KUJUA KILICHOMTOKEA Dk. ULIMBOKA KUAMULIWA KWENYE KIKAO CHA LEO.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka wakati Waziri Mkuu alipokutana na Madaktari Jijini Dar es Salaam wakati wa mgomo wa mwanzo uliofanyika mwezi wa Pili 2012.

WAKATI taarifa za kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka zinasemwa bila wausika kuthibitisha viongozi wa Jumuiya hiyo na Umoja wa Madaktari Tanzania (MAT), wanatarajia kukutana Jumanne Augosti 7, 2012 kujadili tukio zima lililomkumba kiongozi huyo. Baada ya kikao hicho, madaktari hao watakutana na familia yake na kisha kumuuliza Dk Ulimboka kama angependa kilichomtokea kiwekwe wazi kwa jamii.

Dk Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchi nzima, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatato ya Juni 27 mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji a Dar es Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya. Katika tukio hilo daktari huyo aling’olewa meno mawili na kucha za mkono mmoja na baadaye kulazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI).

Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Juni 30 mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika ya Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu. Kusafirishwa kwake kulifuatia taarifa ya jopo la madaktari lililokuwa linamhudumia kutoa taarifa kwa madaktari bingwa kuhusu mabadiliko ya afya yake. Taarifa za kurejea kwa Dk Ulimboka zimezagaa katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya watu wakizijadili katika mitandao ya kijamii.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwin Chitage, alisema kati ya Agosti 7 au 8, 2012 viongozi mbalimbali wa MAT na Jumuiya ya Madaktari, watakutana kujadili suala la kiongozi huyo. “Ndani ya siku mbili hizi (Agosti 7 au 8) viongozi tutakutana na kujadili ripoti ya matibabu ya Dk Ulimboka na tutajadili kama tuvieleze vyombo vya habari ama laa,” alisema Dk Chitange.

Hata hivyo Dk Chitange alisema hatua hiyo itategemea na kauli ya familia ya Dk Ulimboka na yeye mwenyewe (Dk ULimboka) kwa kuwa na wao pia watashirikishwa.

 “Dk Ulimboka na familia yake tutawashirikisha katika mambo ambayo tutayajadili,” alisema Dk Chitage. Alipoulizwa kama kiongozi huyo wa madaktari sasa anaweza kufanya shughuli zake kama awali, alisema hana uhakika kwa kuwa hana taarifa za ndani zaidi .

Advertisements

2 thoughts on “HATIMA YA WATANZANIA KUJUA KILICHOMTOKEA Dk. ULIMBOKA KUAMULIWA KWENYE KIKAO CHA LEO.

  1. Right here is the right blog for anybody who really wants to find out about this topic.
    You understand so much its almost tough to argue with
    you (not that I actually would want to…HaHa). You certainly put a fresh spin on a topic
    that’s been discussed for ages. Excellent stuff, just excellent!

  2. I love what you guys tend to be up too. This sort of clever work and
    exposure! Keep up the terrific works guys I’ve added you guys to our blogroll.

Comments are closed.