GREETINGS FROM MALAWI… ‘TIME TO SHOW STRONG LEADERSHIP’

TEST FOR PRESIDENT JOYCE BANDA TO DIPLOMATICALLY MANAGE THE DISPUTE ON THE BOUNDARY.

At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times.

During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time.

Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now?

Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts.

Statesmanship is a game because image is everything in international politics. A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!

It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image.

The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important!

When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’.

President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge.

If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian.

Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an unreasonable demand?

THIS ARTICAL  HAVE BEEN BROUGHT TO YOU WITH CURTEST OF NYASA NEWS WRITTEN BY  CEDRICK NGALANDE

Advertisements

WANASIASA NA LUGHA YA VITA: HEKIMA YA KUPUNGUZA SABABU YA KUINGIA VITANI NA MALAWI.

DARAJA LA KAGERA (KYAKA) LILILOBOMOLEWA NA IDI AMIN NA VIKOSI VYAKE PAMOJA NA MAJENGO YALIYOBOMOLEWA NAKUBAKIA MAJERAHA YA VITA

  • WANASIASA WANAOTOA LUGHA YA VITA HAWANA HEKIMA NA NI HATARI

  • WENGINE WANATAFUTA UJIKO WA KISIASA

  • TUSIZUNGUMZIE VITA KAMA HATUKO TAYARI KUPIGANA

  • VITA SI LELEMAMA

Sikutegemea kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje Bw. Lowassa kutoa kauli ambayo ikiunganishwa na ile ya Sitta na ya Membe inazidi kuchochea hali ya kutotafuta suluhu. Wote hawa watatu bila ya shaka wanasema kutokana na nafasi zao lakini pia yawezekana wanasema kwa sababu wote watatu wanatajwa vile vile kama wagombea watarajiwa wa urais mwaka 2015. Hata hivyo nazipima kauli hizi kwa jambo la kwanza na si kwa hilo la pili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Edward Lowassa.

Vita si jambo dogo na si jambo la mzaha kama watu wengine wanavyochukulia. Nimeona tangu Wamalawi walipozungumza suala la kudai “ziwa zima” la Nyassa kuwa ni lao baadhi ya watu wetu mwitikio wao wa kwanza umekuwa ni “tupeleke majeshi” au “tupeleke vijana wetu” na sasa leo Lowassa ananukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali kuwa JWTZ liko tayari kwenda vitani na Malawi kuhusu suala hili. Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta

Kufikiria vita siyo jambo dogo na wala si jambo la kutafuta ujiko au siasa. Ni sawa na kuamua kushika bunduki na kumuelekezea mtu. Polisi huwa wanaambiwa kuwa usielekeze Bunduki kama hauko tayari kuitumia. Wale ambao wanabeba silaha (nao ni raia) wanajua kabisa kuwa hutoi silaha kibindoni kama hauko tayari ku-pull the trigger. Maana ya yote haya ni kuwa kutoa silaha na kuishika mkononi siyo suala la ubishoo, urembo au kujionesha kuwa unaweza.

Bernard Membe Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya Jamhuri ya Muungano

Tusipokemea hili la wanasiasa mwisho tutaona watu wanaanza mazoezi ya kutuonesha vifaa vya kivita ili kuwapiga mkwara wa Malawi. Na kweli wapo ambao wanatamani kuona “vijana wetu” wanaanza kuelekea mpakani au kwenye ukingo wa Ziwa Nyassa ili kutuma ujumbe kuwa tuko tayari. Sasa hili ni zuri na linasisimua akili na hisia za “kizalendo”. Lakini tusije kuwa ni mambo ya Wag the Dog ambapo ili kushinda uchaguzi timu ya wanamkakati wa kampeni waliamua kutengeneza ‘vita isiyokuwepo’ ili kupoteza mawazo ya wapiga kura.


Ninachoogopa zaidi ni kuwa wakati watawala wetu tumewabana kuhusu uongovi wao mbovu, sera zao zilizoshindwa na ukosefu wa maono usiokoma suala la mgogoro wa Ziwa Nyassa limewapa ‘gia’ ya kutokea na sasa hata watu waliokaa kimya wakati wananchi wetu wanauawa nakudhalilishwa na vyombo vya usalama wanasimama pasi ya kuomba radhi na kutaka tusimame nyuma yao.

Nimeshangaa kuona Lowassa leo ameweza kukutana na vyombo vya usalama na kupewa taarifa zinazohusu vita lakini huyu huyu hajakutana na vyombo hivi wakati maisha ya wananchi wetu yanahatarishwa na vyombo hivi. Alikuwa wapi kwenye matukio ya Arusha, Mbeya (Tukuyu), Tarime na Songea? Kote huku hakuonesha kujali sana lakini leo ameibuka na kuonesha kuwa ana uwezo wa kufuatilia vyombo vya usalama?


Kama nilivyosema hapo juu vita si lelemama kama baadhi ya watu wanafikiria. Najua wapo ambao wanafikiria kuwa vita dhidi ya Uganda ilikuwa ni uamuzi wa haraka na papara. Wengi (labda vijana zaidi) wanakumbuka tu maneno ya “nia tunayo na sababu tunayo” lakini ni wachache (hata wazee yumkini) wanaokumbuka kuwa kabla ya kufikia maneno hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alielezea juhudi mbalimbali za kutatua mgogoro wetu na Uganda licha ya “chokochoko” zilizoanza miaka karibu mitano nyuma. Kwa Tanzania kwenda vitani ilikuwa ni uamuzi wa mwisho pale ambapo njia zote za amani na kidiplomasia ziliposhindwa.


Leo viongozi wetu tena wakubwa na wenye dhamana nzito zaidi wanazungumza kana kwamba tumeshindwa kabisa kutafuta njia za amani na za demokrasia na sasa wanataka kuifanya Malawi kama wanavyofanyia wananchi wetu. Wananchi wakiandamana wanapigwa virungu na kuuawa na wakigoma wananyamazishwa kwa ghafla. Na hata mazungumzo wanataka yawe kwa masharti yao. Matokeo yake wamejenga fikra wanaweza kum-bully mtu yeyote, vyovyote, na kwa lolote kiasi kwamba wanataka kuanza kuibully Malawi. Hili linafanywa kwa sababu moja tu kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Malawi na inawezekana ina uwezo mkubwa wa kuishinda Malawi.

Wanaozungumza hivi wanafikiria vita inapigwana na wingi wa watu tu na vitu. Vita ni mikakati na mbinu lakini vile vile vita ni kujitoa muhanga. Tunapozungumzia lugha ya vita sijui kama tunafikiria viongozi wetu wanaweza kuhamasisha taifa kama ilivyokuwa miaka ya 1970 ambapo watu walichangia kuku, mbuzi na ng’ombe. Wangapi kati yetu leo watakuwa tayari kutoa magari na mabasi yao kwenda vitani? Wangapi wataamua kwa hiari yao kwenda kupigana chini ya viongozi hawa hawa? Itakuwaje kama watu wakiwa vitani kashfa kubwa ya ufisadi nyumbani inanguruma tena (mafisadi kwa asili hawabadiliki).


Tunapozungumzia vita tunazungumzia maisha ya watu kuuawa. Watu wasifikiri kuwa tukienda vitani na Malawi au nchi nyingine yoyote jirani basi tutakuwa kama tunamsukuma mlevi. Ni wangapi wanafikiria kulipuliwa kwa miji yetu inayozunguka ziwa Nyassa? Mbamba Bay, Kyela, Tukuyu, Rungwe, Mbeya, hata Songea? Kweli kina Lowassa wanapozungumza lugha ya vita wanafikiria kabisa kuwa tumesahau jinsi Amin alivyolipua Mwanza? au ndio viongozi wetu hata historia tena wamesahau? Au watu wamesahau jinsi tulivyolazimika kuchimba mahandaki na kufanya mazoezi ya kujihami hadi kuwa na kuku ndani kwa ajili ya kukimbia nao kwenye mahandaki? Au watu wameshasahau jinsi Idi Amin alivyoweza kuua mamia ya watu wetu pale vikosi vyake vilipovuka Mutukula na kuingia Kagera?


Ninachosema ni kuwa ipo haja ya haraka ya viongozi wetu kuonesha hekima ya kukwepa lugha ya vita. Si kwa sababu hatuna uwezo wa kupigana na Malawi (naamini tunao tena mkubwa na naamini tunaweza kushinda) lakini bado hatujawa na sababu ya kufanya hivyo. Watu kudai “ziwa zima” wakati sisi tumejenga bandari na watu wetu wanavua na kuishi kwenye ziwa hilo na tuna meli miaka nenda rudi na Wamalawi hawajarusha hata baruti ni jambo la kutufanya tufikiri. Kama kweli Wamalawi wangekuwa wanataka vita au ugomvi mbona wao sababu “wanayo” kuwa tumeingilia Ziwa lao na tunafanya vitu kinyume cha sheria?


Wamalawi walipozungumza kwa lugha ya Vita mara moja walitambua kuwa hakuna sababu ya ku-escalate tension kwenye eneo hilo hasa kwa vile tayari tumeshawahi kuwa na tension sana. Ndio maana Waziri wa Mambo ya Nje aliamua kupunguza makali ya lugha ya vita. NI wakati kwa viongozi wa TAnzania nao kupunguza ukali usio wa lazima na kuchochea lugha ya vita. Na sisi wananchi tusiuziwe kirahisi vita kwani ina gharama kuliko watu tunavyoweza kufikiria. Ikumbukwe vita ya Uganda iliigharimu Tanzania kuliko watu wengi wanavyojua na imeacha mojawapo ya majeraha makubwa katika mwelekeo wa uchumi wetu ambayo hadi leo tunasikia maumivu yake. Sijui kama tunataka vita nyingine hasa kwa sababu ambazo ni za kidiplomasia na kisiasa.


Hekima itusukume kufikiria mara mbili. Tutoe nafasi kwa diplomasia na mazungumzo ya amani na nina uhakika wa Malawi kama ni watu wa amani watanyosha mkono wa amani. Njia mojawapo kama tukitaka na sisi kutumia mbinu za diplomasia ni hilo nililosema kwenye mada nyingine badala ya kupeleka vifaru na askari wetu karibu na Ziwa Nyassa na sisi tuanze utafiti kwenye eneo tunaloamini ni letu na kuwaacha Wamalawi wafanye kwenye eneo lao. Kama wanafanya hivyo kwenye sehemu ya eneo letu basi tuna sababu ya kuhakikisha hizo ‘incursions’ hazitokei na hapo ikibidana kuweka boti zenye silaha kuhakikisha hayo hayatokei.


Endapo juhudi hizi za kuonesha sisi ni watu wa amani hazitapokelewa na kama juhudi za kidiplomasia zitashindwa na Wamalawi watapuuzia kabisa madai yetu na kuanza kutenda kanakwamba hatuna la kusema basi ni wakati huo Watanzania waandaliwe kwa kitu ambacho kinaweza kutokea – vita. Na hili lisizungumzwe na kila “dick, tom and harry” kwa sababu wanavaa suti za vyeo mbalimbali. Mtu pekee wa kuweza kulizungumzia hili kama uwezekano ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Endapo tutaacha wanasiasa ambao wanatafuta ujiko kwenye macho ya wananchi walizungumzia na kututia hamasa wakati wao wenyewe hawatoenda vitani na yawezekana hawana mtoto au ndugu hata mmoja JWTZ basi tutajikuta tunapelekwa vitani kisiasa na siyo kwa sababu tunatishiwa au tunajihami. Ni matumaini yangu viongozi wa upinzani (CHADEMA) hawatoingia mtego huu wa kuzungumza lugha ya vita. Hili waachiwe CCM na mashabiki wake mpaka pale ambapo juhudi zao za kisiasa zitakpokuwa zimeshindwa basi waseme tunaenda vitani na hapo viongozi wa upinzani watolee maoni na msimamo wao. Wapinzani wasizungumze lugha ya vita bali ya amani.

Ndio maana kwa upande wangu ninaangalia sana watu wanaotaka kuwa ma-amiri jeshi wakuu, tusipoweza kuwaangalia wanavyoweza kutumia hekima watu hawa watakuja kutupeleka vitani na tukajikuta tunapigana na tukiulizwa tunapigania nini hatujui kumbe watu walitukaniana mama zao na taifa likaingizwa vitani. Na matumaini yangu JWTZ halitaingia kwenye hili suala la kisiasa na kidiplomasia. Tunataka JWTZ letu litakapozungumza iwe ni baada ya tangazo rasmi la vita nje ya hapo JWTZ iwaache wanasiasa wafanya mambo yao.


Siasa na Diplomasia vikishindwa tujiandae kwa ushindi wa Kivita. Hapo ndio tutoe silaha zetu kibindoni na kuzielekeza kwani tutakuwa tayari kuzitumia.


MAKALA HII IMEANDIKWA NA M. M. MWANAKIJIJI UNAWEZA KUWASILIANA NAE KUPITIA mwanakijiji@jamiiforums.com

VODACOM YAWAJALI WATOTO YATIMA KUPITIA RAMADHAN CARE AND SHARE MKOANI MTWARA.

Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share.

  • NI KUPITIA KAMPENI YA RAMADHAN CARE AND SHARE.

  • NI KATIKA MPANGO WA KUWATHAMINI NA KUWATAMBUA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

  • KAMPENI YA MTWARA NI YA PILI BAADA YA KUZINDULIWA TANGA.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imetoa misaada mbalimbali na kuwafuturisha watoto yatima na wa madrasa wapatao 500 mkoani Mtwara kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care and Share iliyo chini ya mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule

Misaada iliyotolewa kwa watoto hao ni pamoja na vifaa vya kujifunzia, vyakula,mafuta ya kula, mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid el fitr ikiwa ni katika kutimiza malengo ya mpango huo uliozinduliwa mapema wiki iliyopita mkoani Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami. akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia wapili toka kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Bw.Hassan Saleh, Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule

Kwa mujibu wa Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bw.Hassan Saleh, mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa waislamu wote nchini, sio tu kwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, bali pia ni kipindi kinachowapa nafasi ya kuwafikiria na kuwajali wale wasio na uwezo ndani ya jamii yetu.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami,akimkabidhi mtoto yatima ndoo ya mafuta ya kula Bi.Halima Juma, aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo….Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

 “Kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tunaendesha kampeni hii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua kuwa Waislamu walio wengi ni wateja wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaenzi kwa kutoa kile tulichonacho katika sehemu ya mapato yetu ili nao wajisikie kuwa miongoni mwa jamii ya Watanzania,” alisema Saleh.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto pamoja na Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mtoto yatima Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto wenzake yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kampeni ya Ramadhan Care and Share imekuwa njia pekee ambayo Vodacom Foundation imekuwa ikiitumia katika kushughulikia maswala mbalimbali yanayowakumba watoto  yatima waishio katika mazingira magumu. Kupitia kampeni hii maisha ya makundi mbalimbali ya watoto yameweza kuboreshwa na kunufaika kutoka kwetu.

Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia mtoto yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kampeni hii ni moja kati ya kampeni nyingi ambazo yetu imeanzisha katika kipindi cha Ramadhan. Tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wateja wa malipo ya kabla wamewezeshwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet bila kikomo kwa shilingi 250 kwa siku.

Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share mjini humo