MSAADA WA TIBA YA MATENDE (ELEPHANTIASIS) KWA BEATRICE

 

BEATRICE SHIMENDE KANTIMBO AU MAMA KANTIMBO, VILE VILE ALIJULIKANA KWA JINA LA MC KIMBAUMBAU KUTOKANA NAKUFANYA U MC KATIKA TAFRIJA MBALI MBALI KABLA YA KUKUMBWA NA MARADHI YA MATENDE (ELEPHANTIASIS)

BEATRICE SHIMENDE KANTIMBO (48) pichani anasumbuliwa na maradhi na hivyo kuhitaji msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu kwani vipimo vya kitabibu vimeonyesha anasumbuliwa na matende (elephantiasis), matabibu wameshauri matibabu yake yafanyike nchini  India.

Kwa takriban miaka 12 hivi sasa Kantimbo anasumbuliwa na maradhi hayo na kumfanya awe tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.

Kwa uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…”Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesha pajani) maumivu yake yalikuwa mithili ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.

“Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali inayojulikana kwa jina la  Neema, Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.

“Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nao ukazidi kuvimba”

Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka  kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza. Anasema:

“Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligundulika tatizo kubwa lilikuwa kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.

“Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto, hivyo naomba wasamaria wema wanipe msaada ili niende India kwa matibabu zaidi.” alisema.

Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.ulizia Beatrice Kantimbo.

Advertisements