KIKWETE ATIMIZA SAFARI YA 333 NCHINI GHANA KWA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MILLS

SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAZISHI ZA ALIYEKUWA RAIS WA GHANA PROFESA JOHN EVANS ATTA MILLS KATIKA UWANJA WA INDEPENDENCE SQUARE JIJINI ACCRA AGOSTI 10, 2012

  • NI SAFARI YA 333 TOKA AINGIE MADARAKANI KAMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO.
  • NI SAFARI YA PILI KWA MWEZI WA NANE, MWEZI WA SABA ALISAFIRI MARA NNE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa Agosti 10 alitimiza safari yake ya 333 toka aingie madarakani. Safari hii ikiwa ni safari ya Msiba ulioikumba nchi ya Ghana huku akijumuika pamoja na viongozi wengine 16 wa nchi mbalimbali katika viwanja vya Independence Square katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIWA NA VIONGOZI WENZIE BAADA YA SHUGHULI YA MAZISHI YA RAIS JOHN EVANS ATTA MILLS WA CHANA JIJINI ACCRA AGOSTI 10 2012

Rais Kikwete akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe atakuwa amefikisha Miaka mitatu nje ya nchi kama hesabu za safari yake zitakuwa katika kila safari alitumia siku tatu.

Alipofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kotoka mjini Accra, Rais Kikwete alilakiwa na Waziri wa Chakula na Kilimo, Kwesi Ahwoi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kikwete alisema kuwa kifo cha Rais Mills kimemnyang’anya rafiki. “Sote tutakosa busara zake. Kwa hakika, kifo cha Rais John Atta Mills siyo pigo kwa Ghana pekee bali ni pigo kwa Afrika nzima na sote tutamkosa sana.

 

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO WAKATI SHUGHULI YA MAZISHI YA RAIS JOHN EVANS ATTA MILLS WA GHANA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA GHANA JIJINI ACCRA AGOSTI 10, 2012

Sote tulimheshimu sana kwa busara zake na urafiki wake. Binafsi, kifo hiki kimeninyang’anya rafiki wa karibu.”

Wakati Rais Kikwete anawasili kuaga mwili wa marehemu, maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Ghana wakiwa wamevalia nguo za rangi ya maombolezo nyeusi na nyekundu walikuwa bado wamepanga misururu mirefu kujaribu kuingia ukumbini kuona mwili wa Rais Mills ambaye amevalishwa kofia ya rangi ya maziwa, suruali nyeusi na kuzungushiwa bendera ya Taifa la Ghana ya rangi za nyekundu, njano na kijani.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITOA HESHIMA KWA ALIYEKUWA RAIS WA GHANA JIJINI ACCRA AGOSTI 10, 2012.

Toka alhamisi Agosti 9, 2012, maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Ghana wamekuwa wanajaribu kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 10 usiku hadi saa sita usiku na kila pembe ya mji wa Accra pamoja na wananchi wake wamepambwa kwa rangi nyeusi na nyekundu ambazo kwa jadi ndizo rangi rasmi za kuomboleza katika Ghana, rangi nyekundu ikiashiria damu na nyeusi ikiashiria giza.

Rais Mills ambaye alifariki dunia Julai 23 2012, akiwa na umri wa miaka 68 alishika nyazifa hiyo Januari 7, 2009, na katika kipindi chake cha uongozi kilikuwa kimebakia miezi mitano kukamilisha. Wakati wa kifo chake, tayari chama chake cha NDC kilikuwa kimeshamteua tena kuwania urais kwa mara nyingine.

Advertisements

2 thoughts on “KIKWETE ATIMIZA SAFARI YA 333 NCHINI GHANA KWA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MILLS

  1. Wakuu hapa naomba kujua, hizo 333 ni idadi ya safari ama idadi ya siku ambazo amekuwa nje ya nchi?

    Kama ni idadi ya safari basi anafaa kuingizwa kwenye Guiness Book of Records na tutumie hilo kama kigezo Kimojawapo cha kuvutia watalii e.g ‘Welcome to Tanzania the land of Kilimanjaro and home to the most traveling President’

  2. I have to thank you for the efforts you have put in penning
    this website. I am hoping to view the same high-grade blog posts by
    you in the future as well. In fact, your creative writing abilities has motivated me to get my own website now 😉

Comments are closed.