MOJA YA PICHA ZA MFANO ZIKIONYESHA YESU KRISTU MEUSI

Karibu madhehebu yote ukiachilia mbali dini zile za Kiafrika wanahusisha rangi yeusi na Laana. Kwa wale wenye imani ya KIKRISTO, au wanao mwamini YESU KRISTO kuna hadithi nyingi ambazo kwa makusudi au bahati mbaya kwa kutumia simulizi (mafundisho) zinaonyesha au kuashiria kitu kibaya ni chenye rangi cheusi.

Kuna wale wanaokwenda mbali zaidi na kusema watu weusi wamelaaniwa na Mungu, sina hakika dhana hii imeanzia wapi, lakini litakalokuwa na liwe mwanzilishi wake lazima atakuwa anawaogopa watu Weusi.

HII NI PICHA NYINGINE IKIMUONYESHA YESU MWENYE ASILI YA KIAFRIKA

Jana jioni niletembelea kwa rafiki zangu “wapendwa” nikakuta wanaangalia mafundisho ya YESU KRISTO kupitia kwenya runinga! lazima ni kiri kuwa sikupanga kuangalia ila kwavile nilifika sehemu hiyo na kukuta wenzangu wanaangalia nililazimika kuendelea kuangali mkanda huo.

Wakati naangalia nikaona akionyeshwa mtu mweupe mwenye macho ya bluu, wakisema ni YESU KRISTO. Nikajiuliza je YESU alikuwa Myahudi au Mzungu? Ikumbukwe kuwa kuna wayahudi wenye ngozi nyeusi.

Nikajiuliza hivi wenzetu weupe “WHITE EVANGELICAL CHRISTIANS” wangeshiriki kumwamini na kumfuata YESU kama picha zingemuonyesha akiwa na ngozi nyeusi.

YESU MWENYE ASILI YA KIAFRIKA AKIWA NA MTOTO WA KIAFRIKA PIA

Ukipitia vitabu hasa Biblia na maandiko mengine utangundua wazi kuwa yamejipambanua wazi kuwa YESU KRISTO hakuwa mwenye ngozi nyeupe lakini cha ajabu kwa makusudi dunia imezidi kumwonyesha YESU KRISTO kama kijana mweupe mwenye nywele za rangi ya khaki na macho ya bluu.

Hivi wapendwa mnajua kama YESU alitoka familia yenye asili ya Afrika? Najua kwa hili nitakumbana na upinzani mzito, na wakosoaji wangu watakuwa wale wanaopenda kuwapotosha wenzao. Ila kwa wale waadilifu wachache watakubaliana na ukweli huu.

Ni ukweli usiopingika kuwa ngozi ya YESU ilikuwa na rangi nyeusi. Hebu jikumbushe kwa kupitia Biblia ni sababu zipi zilizowafanya watesaji wa Yesu kumlazimisha Simoni Mkirene kubeba msalaba wa YESU? Ukweli ni kwamba sababu ya pekee na moja tu ni yeye kuwa na asili ya Afrika kama YESU, Ikumbukwe kwamba maandiko yanaonyesha wazi kuwa Mkirene alikuwa anatokea mji uliokuwa unaitwa Krene (sasa Tripoli).

MOJA YA PICHA IKIMUONYESHA YESU MWENYE ASILI YA KIAFRIKA

Kumbukumbu hasa kitabu cha Biblia kinaonyesha wazi Uafrika wa familia ya YESU. Katika kitabu hicho kitakatifu kinacho aminiwa na wakristo wote duniani kinaeleza wazi kuwa Musa (Moses) alimuoa binti Yethro ambaye alikuwa Kuhani wa Midiani, huyu alikuwa mweusi kabisa, vilevile ushahidi mwingine ni ule wa mfalme Selemani naye kumpa ujauzito malkia wa sheba, kwa simulizi hizi kama ni za ukweli basi zinaondoa uwezekano kabisa wa kijana Yesu kuwa na nywele za khaki na macho ya bluu achilia mbali rangi ya ngozi kuwa nyeupe.

Ndiyo maana mpaka sasa kwenye jamii ya wayahudi kuna Wayahudi wenye asili ya Afrika na wale wengine.

Ziara ya mwisho ya Mtume Mathayo alipoenda tembelea Alexandria (Misri) wakristo wa huko kwa heshima yake walitengeneza sanamu za YESU. Kwa wale waliobahatika kuiona sanamu hiyo ilikuwa na pua kama za waafrika. Kumbukumbu hizi wakoloni waliziharibu ili kuondoa ushahidi huu.

Advertisements