MABILIONI YANAYOKUSANYWA NA M4C KWENYE HARAMBEE NI USANII MTUPU; NAPE

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM, ITIKADI NA UENEZI, KIJANA MPAMBANAJI NAPE NNAUYE

  • CCM WADAI WANA USHAHIDI  KUONYESHA FEDHA HIZO ZILIZOKUSANYWA KWENYE HARAMBEE? .

  • WAFADHILI WANATOA FEDHA HIZO SIYO WEMA KWA TANZANIA.

  • ASHINDWA KUTAJA NCHI AU WATU WANAO TOA FEDHA HIZO.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi,  Kijana Mpambanaji Nape Nnauye amejitokeza kama ilivyo tegemewa na wengi Jumapili Agosti 12, 2012,  na kuweka bayana kushangazwa kwake na mabilioni yanayokusanywa na M4C ya chama cha CHADEMA mbele ya waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

Mbele ya waandishi mbalimbali Kiongozi huyo kijana Mpambanaji Nape Nnauye kwa unyonge tofauti na kawaida yake alikishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kukishutumu kufanya usanii wa kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la  kuhalalisha mabilioni ya chama hicho huku akidai kuwa hutolewa  na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

“Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii  kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanya kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni.” alisema Nape.

Nape alisisitiza “Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”

Mpambanaji huyo Kijana aliwaacha waandishi wakiwa wameduwaa baada ya kushidwa kuwataja wafadhili pamoja na nchi zinazotoa fedha hizo. Mwandishi mmoja mkongwe alisikika akihoji “Kazi ya upande wa mashtaka ni kuthibitisha mashtaka na si kazi ya mshtakiwa” Nape anataka CHADEMA wataje nini? Kama yeye anadai kuwa anayo ‘mikataba’ kwanini asiitoe? Alinong,ona Mwandishi huyo.

Nape aliendelea kudai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda  ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

Pamoja na kuwataka kuweka wazi masharti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo,  na  kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

“ Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasaidia  kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.

Baada ya Mkutano huo Mchambuzi wa mambo ya kisiasa wa M2S Bwana Jesse Rutahigwa alinukuliwa akisema “Inasikitisha sana kwa mtu wa cheo chake kusema vitu kama hivyo, Nilidhani yeye mwenye nyumba angekuwa wa kwanza kumtaja mkazi anayetaka kuichoma nyumba yake kwa kushirikiana na mtu wa nje kuliko kumtaka mchomaji huyo awaambie wakazi wengine wa nyumba hiyo ni nani anayeshirikiana naye katika njama mbaya hiyo”.

“Eti wasipowaeleza WATANZANIA ukweli yeye atasema. Ni nini kinachomzuia kusema sasa?” alihoji mchambuzi huyo. “Je anasubiri mpaka moshi uanze kufuka ndipo aseme jamani nyumba yangu inaungua na mchomaji ninamjua lakini sikutaka kumsema!!??”  Alisema Rutahigwa kwa sauti ya unyonge.

Advertisements

One thought on “MABILIONI YANAYOKUSANYWA NA M4C KWENYE HARAMBEE NI USANII MTUPU; NAPE

  1. Nepi umekosa vya kuongea na Watanzania wakakuona umeamua kusema ulivyoyasema. Kwa bahati mbaya watz wa sasa hawaendi kwa hisia kama zako. Wanataka facts. Toa facts ueleweke. Kama NYINYIEMU yenu inakufia usitafute wa kukusaidia kuizika.

Comments are closed.