MKUTANO WA 14 WA MAZINGIRA KWA NCHI ZA AFRIKA SEPTEMBA 10 ARUSHA.

MKUU WA MKOA WA ARUSHA, MAGESA MULONGO ANAONGEA NA WAANDISHI WA HABARI NJE YA JENGO LA MKUU WA MKOA.

ARUSHA itakuwa ni mwenyeji wa mkutano wa kumi na nne wa mazingira kwa Nchi za Afrika utakaoanza Septemba ,10 hadi 14  2012.

Mkutano huo unalenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu mazingira yakiwemo maazimio ya mkutano wa kimataifa wa mazingira uliofanyika huko Brazili.

Akiongea na Waandishi wa habari Alhamisi Agosti 24 2012 nje ya Jengo la ofisi zake Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Bw. Magesa Mulongo alisema kuwa mkutano huo utaweza kuwakutanisha wageni zaidi ya elfu tatu sanjali na Mawaziri wa Nchi hizo.

Alisema kuwa  mkutano huo utafunguliwa na Rais  wa Jamhuri ya  muungano wa  Tanzania mheshimiwa   Jakaya Kikwete.

Mulongo alibainisha kuwa hii ni fursa ya wananchi wa mkoa wa Arusha katika sekta mbalimbalia na hivyo kutoa mwito wahakikisha wana wakalimu  wageni hao.

Taarifa zinasema kuwa kabla ya kuanza kwa mkutano huo pia utatanguliwa na mkutano mwingine wa wadau wengine wa mazingira ambao nao wataweza kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta hiyo ya Mazingira hasa kwa nchi za Bara la Afrika.

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA MAZINGIRA (UNEP) KANDA YA AFRIKA; MOUNKAILA GOUMANDAKOYE AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) Kanda ya Afrika, Mounkaila Goumandakoye amesema mkutano huo unaowakutanisha Mawaziri wote wa mazingira kutoka nchi za Afrika utajadili mambo muhimu ya mazingira likiwepo suala la kudhibiti uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za viwanda na kuyatazama maazimio ya Mkutano wa kimataifa uliofanyika nchini Brazili.

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS TANZANIA SAZI SALULA AKIONGEA NA WANAHABARI.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula, alisema Tanzania ilichaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu huko Bamako nchini Mali mwaka 2010 na itakaa kwenye  nafasi ya Uenyekiti kwa  muda wa miaka miwili huku ikiratibu mikutano hiyo.

Advertisements