WALIO TOSWA NA JK NDIYO WATABIRI WA KIFO CHA CCM!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kabla ya kikao cha NEC, leo mjini Dodoma. Wengine, waliokaa. Kutoka kushoto ni Mawaziri Wakuu wa zamani, John Malecela na Cleopa Msuya, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

 • YUMO MGEJA, LEMBELI, MKONO, BASHE, KINGWANGALLA, PREMJI.

MOJAWAPO ya sifa kubwa atakayokumbukwa nayo Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni kutoa kauli tata ambazo hubakia katika mjadala kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wana-CCM, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma Jumanne Septemba 25 2012

Tofauti kidogo na kauli za awali safari hii kauli yake imeondoka na vigogo wa chama hicho na kuwatupa nje ya kinyang’anyiro cha kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya za chama na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Habari kutoka ndani ya NEC, ziliwataja walioenguliwa kuwa ni pamoja na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana la CCM Taifa (UVCCM), Hussein Bashe.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni baada ya kuwasili Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma

Mbali ya hao, hasira za mwenyekiti huyo wa chama tawala zimemwangukia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

Wengine waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe. Wabunge hao ni miongoni mwa waliotia saini kutaka Waziri Mkuu Pinda ang’oke. Duru za siasa zinasema kuwa msimamo wa wabunge hao kuhusu Pinda, ndio ulisababisha wakatwe kuwania NEC.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Makamu (kushoto) baada ya kupiga picha ya pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kwenye viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni.

Athari za saini za kutaka kumng’oa Pinda ambazo zilisababisha Baraza la Mawaziri lipanguliwe na kuundwa upya, zimeonekana pia kumgusa Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ambaye ametupwa nje kuwania nafasi ya uenyekiti wa wazazi CCM taifa.

Hali ya mkosi bado inaendelea kumwandama Mbunge wa zamani wa Nyamagana, Antony Diallo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza aliyekuwa akitetea nafasi yake, Clement Mabina ambao nao majina yao yameng’olewa.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma

Wakati vigogo hao wakiugulia machungu ya kutoswa, Rais Kikwete ametoa kauli nzito ambayo moja kwa moja inaonekana kuwalenga wahanga hao ya kutaka wagombea waliopata kutoa kauli za vitisho dhidi ya chama hicho kufanya kile walichokusudia kukifanya.

Akizungumza kwa ukali, Kikwete ambaye juzi alitamba akisema CCM haitakufa kama inavyotabiriwa na baadhi ya watu, alihitimisha kauli yake kwa kusema watu wenye kauli za namna hiyo walikuwa hawafai kuendelea kuwa wanachama wa chama hicho.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Samwel Sitta akimsalimia kwa unyenyekevu Mjumbe mwenzake, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma.

Alisema hivi sasa wagombea wengi wamekuwa wakijitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na kung’ang’ania kupata ushindi kiasi cha wengine kufikia hatua ya kutoa kauli za vitisho kwa kusema wasipopata nafasi ‘patachimbika’.

“Inashangaza kuona kugombea NEC tu watu wanataka kuuana, wanakimbilia nini huko ndani?” alihoji Rais Kikwete.

Mjumbe wa NEC, Frederick Sumaye akimweleza jambo Mjumbe wa NEC mwenzake Kingunge Ngombale-Mwiru, baada ya kukutana nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma

“Ina maana watu hawa wanaonyesha dhahiri kuwa hawana nia njema na chama, bali wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo tuna kila sababu ya kuwakataa ili tujenge timu ya ushindi ambayo ndiyo nia yetu,” aliongeza mwenyekiti huyo.

Rais Kikwete alisema kama kuna wagombea ambao watajitoa ndani ya CCM na kuhamia chama kingine kutokana na majina yao kutopendekezwa, wajitoe.

Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma

“Hatuchagui wagombea wenye ndimi mbili ambao wanasema kama hatutapitishwa tutahamia chama kingine, hao tunawatakia kila lakheri  waende tu, kwani hawana nia njema na chama hiki,” alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa ukali, alisema anajua suala la kuwaengua baadhi ya wagombea litazua mjadala, lakini nia ya chama ni njema katika kuleta sura mpya na uhai.

Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma

“Kufanya hivyo ni pamoja na kupata viongozi watakaokiletea chama ushindi katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2014 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, hivyo lazima watu hao watambue kuwa kazi wanayoifanya ni kuunda timu ya ushindi wa chama na si wa watu.

“Najua kuna ndugu na marafiki ambao hawatateuliwa kutokana na kujaa kwa nafasi na mapungufu na madhaifu ambayo yalionekana baada ya Kamati ya Maadili kupitia majina yao, hivyo wasione kama wameonewa bali wajue kama ndio utaratibu wa chama wa kuhitaji viongozi shupavu, hodari na mwenye uwezo wa kukitetea na kukipigania chama na kukipa ushindi,” alisema Rais Kikwete.

Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

Aliwatahadharisha wagombea watakaotumia rushwa kwenye kampeni zao watambue kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wanafanya kazi yao muda wote, hivyo atakayekamatwa asije akamlaumu mtu.Naam Habari  ndiyo hiyo Kidumu Chama za Mapinduzi na zidumu Fikra za Mwenyekiti wa CCM  Imehaririwa na mtaalamu wa lugha za kimataifa Chocks Chokala wa Codeta Publishers

MKUTANO WA KAMATI KUU YA CCM DODOMA SEPTEMBA 24 2012

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katika Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akisoma utangulizi, mwanzoni wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.  (Picha na Bashir Nkoromo)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwaslimia wajumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Mjumbe wa NEC Oganaizeshenu, Asha Abdallah Juma na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, (Zanzibar Vuai Ali Vuai) kabla ya kuanza kukao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
Wajumbe wa Kamati Kuu, Maua Daftari na Simba wakijadili jambo taratibu, kabla ya Kikao cha kamati hiyo kuanza leo mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
Baadhi ya viongozi wa CCM wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi kwa awamu nyingine katika uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika Novemba mwaka huu, wakiwa nje ya ukumbi wakati kikao cha Kamati Kuu kikiendelea mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Azim Premji, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus-Rukwa, Wajumbe wa NEC Asha Baraka na Hkadija Kopa (Picha na Bashir Nkoromo).

KATIBA YA WATANZANIA AMBAO HAWAJATAYARISHWA KUIANDIKA

Eric Luwongo Mratibu wa Katiba wa Asasi ya HAKI-MADINI

TANZANIA iko kwenye mchakato wa kuandika historia mpya ya kuwa na Katiba iliyotungwa na kuwashirikishwa wananchi wenyewe, ingawa hatua za awali zinaonyesha kukumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kutoandaliwa kwa wananchi wenyewe.

Ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wa Tanzania hawajatayarishwa vya kutosha kushiriki katika mchakato huo hasa kutokana na ukweli kuwa wengi wa wananchi bado hawaijui katiba iliyopo sasa, hivyo, kushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya katiba kuwa ni tatizo kwao.

Eric Luwongo Mratibu wa Katiba wa Asasi ya HAKI-MADINI akiwa katika harakati zake za kuhamasisha umma kushiriki katika mabadiliki ya katiba hiyo mwishoni mwawiki jijini Arusha alibainisha kuwa moja ya changamoto ni sheria mbovu inayosimamia mchakato huo na kuvitaja baadhi ya vifungu kama vilivyo ainishwa kwenye Kazi ya Tume Tangazo la serikali Na. 394 la mwaka 2011 amri ya 2 aya (j)ibara ya 9-(1) na 17-moja mpaka mbili ya sheria mpya ya mabadiliko ya katiba ambayo inawanyanganya  mwananchi hakia ya kujadili baadhi ya mambo kwa madai kuwa ni ya kitaifa.

“Hata sisi waelimishaji kutoka katika Asasi mbalimbali tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubanwa na sheria mpya ya mabadiliko ya katiba hasa ibara ya 17 kifungu kidogo cha tisa ambacho kinatunyima hakia na uhuru wa kuelimisha umma kwa mapana yake” alilalamika Luwongo.

Aidha Luwongo alibainisha  tofauti na sensa ambayo serikali ilionyesha dhamili ya kweli na kutumia nguvu nyingi katika mchakato wake kwa kuyaacha makundi mbalimbali kufikisha elimu na ushawishi wake kwa watanzania zoezi la Katiba mpya linaonekana kupooza kwasababu vya sheria hii ambayo ina milolongo mingi anayopaswa kufuata mwamasishaji ndiyo maana utaona kama vyama vya Upinzani asasi mbalimbali na vyombo vya habari vinasuasua tofauti na sensa.

Kwa kuwanyima uelewa wausika ambao ni watanzania wenyewe je unategemea tutapata kweli katiba ambayo ni ya watanzania alihoji Mwandishi Mwandamizi wa siku nyingi Abiba Suedi.

Awali Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba alinukuliwa kuvionya vyama vya siasa kutoingilia mchakato wa zoezi la ukusanyaji maoni ya Katiba kwa kuwashawishi Wananchi kuzungumza mambo wanayoyataka wao wakati wa zoezi hilo jambo ambalo limepigwa vikali na baadhi ya wanaharakati wakidai kuwa vyama husika vinatimiza wajibu wao kwa wananchi ambayo ni kutoa elimu juu ya mchakato huu.

CHADEMA WALAANI KUBADILISHWA KWA MATUMIZI YA VIWANJA VYA CHADEMA SQUARE (NMC).

ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA (CHADEMA) AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI, NA KUSHOTO NI KATIBU WA CHAMA HICHO AMANI GOLUGWA JUMATANO SEPTEMBA 19 2012 KATIKA OFISI ZAO.
 • LEMA ASEMA MATUMIZI HAYO YAMEFANYIKA KISIASA ILI KUWAKOMOA CHADEMA NDIYO MAANA HAKUNA MAANDALIZI KATIKA ENEO HUSIKA KWA AJILI YA WAMACHINGA.

 • KATIBU WA CHADEMA MKOANI ARUSHA AMANI GOLUGWA AMESEMA HAWAWEZI KUKOSA SEHEMU YA KUFANYIA MIKUTANO, MIKUTANO ITAFANYIKA HATA KWENYE NYUMBA ZA WATU ILI KUONDOA UMASKINI.

 • OLE MILYA AISHANGAA SERIKALI YA CCM KWA KUBADILISHA MATUMIZI YA KIWANJA CHA WAZI CHA JAMII KUWA SEHEMU YA BIASHARA BILA KUJALI HASARA YA MAAMUZI HAYO.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema, ameishauri Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kupitia kwa Mkuu wa Wilaya hiyo John Mongela kuhakikisha kuwa anatumia busara zaidi  katika kubadilisha matumizi ya kiwanja cha CHADEMA SQUARE (NMC) kutoka kuwa viwanja vya wazi na kufanya sehemu ya biashara eneo la wamachinga.

Hayo yalisemwa Jumatano Septemba 19 2012, katika mkutano wa viongozi wa CHADEMA na waandishi wa habari kuelezea hatua zilizo chukuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kupitia kwa Mkuu wake wa wilaya kwa kile CHADEMA wanacho dai maamuzi ya kisiasa yasiyo na maslahi kwa taifa.

“inamaanisha nini, leo tumeshapanga kufanya mkutano halafu Mkuu wa Wilaya anaelekeza watu wamwage Vifusi kwa ajili ya eneo la Machinga je wakati wote huo walikuwa wapi  na kama siyo kutogombanisha na wamachinga lakini bado tuna nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya mikutano hata kama ni majumbani kwetu, na tutaendelea tutawatetea hawa vijana mpaka mwisho wa dahari ”alisema  Lema

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi uligundua kuwa hatua hiyo imechukuliwa siku moja tu baada ya CHADEMA kutangaza kuwa watafanya mkutano wa hadhara katika eneo hilo. ili kukwamisha mkutano huo Halmashauri ikaagiza eneo hilo liwekwe uzio na kuanza kutenga vitalu vya kuwagawia sehemu wamachinga.

“ukiangalia viwanja hivi vya CHADEMA SQUARE (NMC) ambavyo vilikuwa vikitumika kwa shuguli za kijamii bado ni hafifu sana kutokana na kuwa hakuna miundombinu yoyote iliyo andaliwa kukidhi haja ya kuwa eneo la wafanyabiashara wamachinga  ila wamewakimbizia huko kwa ajili ya mkutano wetu  ambao ulikuwa wa kuchakaza sura ya Arusha kutokana na ukweli ambao sisi tunaujua na tungeusema”alilalamika Lema

 

 

Awali Katibu wa chama hicho wa Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa ilitokea sinto fahamu baada matayarisho yote kukamilika lakini walipo fika kwenye viwanja vya  CHADEMA SQUARE (NMC) walihamaki kukuta vinafanyiwa marekebisho na kuanza kupitishwa greda pamoja na  kuzungushiwa uzio huku Halmashauri wakidai kuwa matumizi ya uwanja huo ni kwa ajili ya wamachinga

Aliongeza kuwa mbali na hayo wamejipanga kuhakikisha Mji wa Arusha unakuwa na historia yake kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake ya msingi na wala siyo kuonewa na baadhi ya viongozi ambao hawana maadili ambao ndio chanzo kikubwa sana cha umaskini.

Kwa upande wake James Ole Milya alisema kuwa serikali ya ccm ina hila dhidi ya CHADEMA kwa kuwaondoa katika uwanja huo huku wakijua wazi kuwa maeneo hayo ni maskani yao.

Alisisitiza suala la haki lazima kutendeka kwa pande zote mbili na kusema kuwa viwanja vyote vimejengwa na wananchi hivyo itafika mahali wananchi watavidai kwa nguvu kwa kuwa fedha zao zilitumika katika kujenga

“Wahuni hawa CCM wameamua kuwaonea Watanzania kwa muda mrefu sasa kwa sababu viwanja vyote kama CCM kirumba na n.k vilijengwa kipindi tukiwa katika chama kimoja baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi utaratibu ule haukufanyiwa kazi ipasavyo na haiwezekani viwanja vikubwa kama hivyo eti vimilikiwe na hatutakubali tupo kwa ajili ya kutetea maslahi ya Watanzania”alisema Milya

MWANGOSI KAENDA ZAKE, TUMEBAKI WANAFIKI NA JUKWA LA WAHARIRI

 • Mkusanyiko wa picha kuonyesha tukio la kuzingirwa, kuteswa hadi kuuawa kinyama na askari wa Jeshi la Polisi kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi Jumapili  Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.

  JUKWA LA WAHARIRI HALI ONYESHI NIA THABITI NA YA UKWELI KATIKA KULAANI NA KUTEKELEZA MAAZIMIO YAKE JUU YA TUKIO HILI.

 • KAFARA YA POLISI KWA ASKALI WAKE WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA FFU MWENYE NAMBA G2372 PACIFICUS CLEOPHASE SIMON (23) SIYO SULUHISHO LA  KUTUNYAMAZISHA WATANZANIA.

 • NAKOSA JINA SAHIHI LA KUWAITA WANAHABARI PAMOJA NA WAWAKILISHI WETU, KWELI KUMBUKUMBU MARA NYINGI HUWAKIMBIA WATU WASIO JISUMBUA KUZITAFUTA.

  Waandishi wa habari mbalimbali wakitoa dukuduku zao mara baada ya kumalizika kwa maandamano ya kulahani Mauaji ya Polisi

Mimejizuia sana kuchangia chochote katika tukio la kuzingirwa, kuteswa hadi kuuawa kinyama na askari wa Jeshi la Polisi kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi Jumapili  Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.

Nimeandika zaidi ya mara ishirini na kufuta, hatua yangu hiyo hisichukuliwe kama hofu ya kuingilia uhuru wa mahakama, la hasha labda ni kutokana na hasira na kukerwa na tukio zima hivyo kupelekea  kusababisha maumivu ya kichwa yasiyo sikia dawa na msononeko wa moyo jambo linalonifanya nitoe dukuduku langu hili kutuliza hali hii kwasababu bila kufanya hivyo sitoweza kuandika chochote na kikubwa zaidi ni kuhidhulumu nafsi yangu.

Naona aibu kuwa mmoja ya watu ninao wakilishwa na jukwa la wahariri kwa kuniacha mpweke katika hili kama vile jua liwakalo peke mchana badala ya kuwa kama mbalamwezi usiku unaosaidiwa na nyota lukuki.

Polisi wakimsaidia askali mwenzao aliye jeruhiwa na bomu huku mwili wa marehemu ikiwa umeachwa bila msaada wowote

Tunasema Dk. Slaa, aliongoza vurugu kule kijijini Iringa wakati wa kufungua tawi la CHADEMA, wakati siku ya tukio Dk. Slaa, alibaki Iringa mjini wala hakwenda kijijini kwa kuzingatia zuio lililokuwa limewekwa na Jeshi la Polisi.

Ukweli huu hautajwi na magazeti yoyote ya taifa hili na wala hakuna redio inayowafafanulia wananchi wake yaliyojitokeza siku hiyo.

Amekufa Daudi Mwangosi, tukaendeleza uongo kwamba alikufa kwenye vurugu ya Chama cha CHADEMA. Polisi zaidi ya wanane, walimvamia Mwangosi na kumpiga vibaya, sasa tunasema muuaji ni mmoja na ndiye amefikishwa mahakamani:

RPC AKIWA ANATOA MAELEZO BAADA YA KUWADHIBITI WAFUASI WACHACHE WA CHADEMA WALIO HUDURIA UFUNGUZI WA TAWI LAO

Wale polisi wengine, walioongoza kipigo cha mwandishi huyu mbona hawatajwi? Au ni danganya toto, ili kesho na keshokutwa tusikie kwamba Pasficus, yuko huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha pasi na makosa kwamba huyo ndiye muuaji. Sote tunakumbuka kesi ya Zombe; ilichukua muda mrefu, lakini hatimaye Zombe alishinda kesi.

Ni waandishi wangapi wameweka wazi kuwa tukio hilo lilitokea mbele ya Mkuu wa Polisi wa Mkoa?

Ni waandishi wangapi wametukumbusha historia ya Kamanda Michael Kamuhanda kama kamanda aliyesimamia mauaji ya wananchi wanne Iringa na ambaye badala ya kutiwa pingu na kupelekwa jela alihamishwa na kupelekwa mkoa mwingine matokeo yake kama ilivyokuwa Songea amekuja tena na maelezo yasiyo na mashiko akimlaumu aliyeuliwa kwa mauaji yake tena bila aibu?

POLISI WAKIWATAKA WAFUASI WA CHADEMA KUTAWANYIKA ENEO LA TUKIO OFISI ZA CHADEMA NYOLOLO MUFINDI

Ni mwandishi gani aliyehoji nani alimpa bomu la mlipuko polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mwenye namba G2372 Pacificus Cleophase Simon (23)? Tafsiri yake ni aliyempa bomu hilo ndiye aliyempa amri ya kuua! Suala la bahati mbaya halina nafasi hapa.

Ni mwandishi gani aliye jaribu kupitia vifungu vya sheria kujaribu kuona kama kitendo cha polisi kilikuwa ni halali? Japo kuchapisha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) 21(1,2)  hili wananchi wajuwe ukweli?

POLISI WAKIWA WAMEIZINGILA OFISI YA CHADEMA

Akuna mwandishi aliyehoji uhalali wa kuundwa kwa tume bubu ambazo hazina majibu kwa watanzania tena zikiundwa na wausika wenyewe wanaushutumiwa kufanya matukio. Historia inatuonyesha kuwa tume ziliwahi  kuundwa Arusha, Mbeya, Songea na Morogoro.

Kwenye nchi ambayo inaheshimu utawala wa sheria, kwa vile Kamanda Kamuhanda alikuwa ni shuhuda wa tukio (material witness) hakupaswa kuwa sehemu ya uchunguzi na kwa hakika hakupaswa kuendelea na wadhifa wake wakati uchunguzi wa mauaji yaliyotokea mbele yake na kwa sababu yake unafanyika. Kumwacha aendelee na nafasi yake ni mojawapo ya uvunjaji mkubwa wa haki ambao serikali imeruhusu na vyombo vya habari vinapayuka bila kujenga hoja au kutoa jibu mbadala.

Polisi wa FFU wakipiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ofisi za tawi la chama chao

Kama kasuku tukaendelea kuandika bila kuhoji pale Emmanuel Nchimbi Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya ndani alipo jitokeza na kuunda tume Dar es Salaam wakati (IGP) Said Mwema Kaunda ya kwake Iringa?

Alipo fundishwa kuwa hana mamlaka ya kuunda tume akaiita kamati. Tukio moja kamati ngapi? Ikitokea zikapingana, mtaunda nyingine itakayotoa suluhu? Inatia uchungu mzaha huu wa kitoto unafanyika mbele ya macho yetu wanahabari na sisi tunanungunika kimya kimya wakati ndiyo tunapaswa kutoa sauti?

Nakosa ujasiri na hoja wa kutetea fani yangu ya uandishi pale ninaposoma na kusikia vyombo vya habari vikiripoti bila kujipa muda wa kufikiri kidogo kabla ya kusambaza kwa ushabiki kauli ya Msajiri wa Vyama vya Siasa nchini Mweshimiwa John Tendwa.

OFISI YA CHADEMA NYALOLO IKIFUKA MOSHI WA MABOMU

“Ofisi yangu kwa sheria na kanuni zilizopo za vyama vya siasa inanipa uwezo wa kukifuta chama chochote cha siasa kinachovunja amani na utulivu wa nchi.” Alinukuliwa  Mweshimiwa John Tendwa.

Akaongeza huku akibwata “Tumechoka na Tabia hiyo…. Kuanzia sasa chama chochote kitakachosababisha kifo nitakifuta kwa mujibu wa sheria zilizopo”.

Hayo yote aliyasema mbele ya wanahabari? Wangapi walioji kama Mweshimiwa huyo amejilidhisha kuwa kwa sheria zake, chama cha siasa kinaweza kufanya jinai?

Mwili wa Daud Mwangosi baada ya kusambaratishwa na bomu Aliyekaa jirani ni askari ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo

Wanahabari walishindwa nini kumsuta Mweshimiwa huyu na kumwambia kuwa matamshi yake ni hatari na yanapandikiza chuki ndani ya mioyo ya wanajamii wasiokuwa wanachama wa chama chochote na hivyo kusababisha serikali na yeye mwenyewe kuchukiwa na jamii.

Wanahabari kwanini awakumuhoji hili adhibitishe kuwa vifo vyote vilivyo tokea kwenye maandamano au mikutano ya vyama vya siasa hapa nchini marehemu waliuawa na wanasiasa na siyo polisi? Au ni wapi na kwenye mkutano gani aliwaona wanasiasa wakiwa wamebeba silaha ukimtoa rafiki yake Aden Rage wakati wa kampeni kule Igunga?

Gari ya kamanda wa polisi mkoa wa Iringa MIchael Kamuanda akiongoza msafara wa FFU

Napingana na wanahabari wanao andika habari hizi wakidai eti haya ni matamshi ya kisiasa. Haya ni matamshi ya kijinga kwasababu siasa na ujinga ni vitu viwili tofauti kabisa. Tunapaswa kuwaumbua viongozi wa ajabu ajabu hili kuiokoa nchi hii na mikosi.

Pamoja na kuwapa nafasi kubwa wapotoshaji wa habari aibu ni kushindwa kwa jukwa la wahariri kutekeleza maazimio yao kwa vitendo ya kususia shuguli zote za jeshi hilo….. kila kukicha habari za polisi zinatawala vyombo vyetu, nasikia mwishoni mwa wiki hiliyopita wawakilishi wetu hao walikuwa Morogoro kwa mwaliko wa waziri wa mambo ya ndani.

Ndiyo maana nakubaliana na wale walio sema mmoja wa viongozi wa juu wa Jukwaa la wahariri na aliyekuwa na jukumu la kuandaa maandamano hayo Bwana Nevil Meena ndie aliyemwalika waziri nchimbi kuhudhuria maandamano ya wanahabari.

Mwandishi wa habari Mkongwe Bw Jackton Manyerere akizungumza katika maadamano ya kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam

Bwana Meena anadaiwa kumruhusu waziri kuja kwenye maandamano kama mtu wa kawaida sababu watu wote walikuwa wanakaribishwa. Hii ndio sababu ilimfanya Meena kuwaomba wamsikilize lakini nguvu za waandishi zikamshinda.

Ni katika matukio mengi tu waandishi tumekuwa tukilalamikiwa kwakupindisha ukweli au kuuficha kabisa. Na hilo nimelidhihirisha mwenyewe katika baadhi ya matukio niliyoyashuhudia Kama lile la Tarehe 5 Januari 2011 Arusha (Sitorudia maelezo yake).

Wanahabari wenzangu huyo tuliyokuwa tunamsaidia kwa sababu yoyote hile iwe rushwa, kulinda mwajiri wetu, au kujipendekeza tu kwa mwajiri tujuwe mwisho wa siku ana msaada kwetu.

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena akitoa ratiba ya njia ambazo maandamano yatapita kabla ya kuanza kwa maandamano hayo wanaofuatia katika picha ni Profesa Rwaitama, Jane Mihanji na Rashid Kejo.

Kwani ikumbukwe katika kampeni za mwaka 2005 marehemu aliandamana na timu ya Jakaya Kikwete kwenye kampeni na kuzunguka nchi nzima leo hii yako wapi? Hawa wanatuchukulia poa wakidhani hatuna uwezo wa kufanya uchunguzi wala kuhoji hivyo ujifanyia na kusema wapendacho.

Wanahabari Nguvu tuliyonayo ni kubwa mpaka tukaitwa the “4th Estate” nyuma ya Executive(1st Estate), Legislature (2nd estate) na Judiciary (3rd estate), mbele ya Counter Crime Unit {polisi} (5th Estate).

Lakini wanahabari kwa njaa au uoga tumekuwa wadogo nakuwa tegemezi (dependants) mpaka wa 5th Estate, Tumeshindwa kujiamini na kujitegemea, hatuwezi kusema kweli. Sisi wenyewe tunakatishana tamaa, msema kweli anatengwa.

Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa tumekaa kimya, Jerry kashikishwa kesi tukakaa tu bila kufanya lolote. Na sasa mwenzetu kauwawa tena akiwa kazini (on field), Tunafanyaje?

 • Je tutakaa kimya upepo upite?

 • Je tutakubali pesa muudanganye Umma?

 • Je tutageuza kifo cha Daudi mtaji wa kupokea na kuomba rushwa a.k.a vibahasha?

 • Je sasa tutaona kama wakati umefika na kusimamia kweli na haki?

Najua, hata tukifanya utafiti wa namna gani, si msaada wowote kwa Mwangosi, amekufa na kuzikwa. Maisha yake yamekatishwa na hayarudi kamwe. Watoto wake wamebaki wakiwa, na mkewe amebaki na mzigo mkubwa kuwalea watoto hawa. Lakini ili jambo lisitokee tena ni lazima tujiulize chanzo cha chuki kati ya polisi na wananchi?

Je, waandishi wataendelea kuwa salama? Je, wataendelea kuandika kwa uhuru bila kuogopa yale yaliyomtokea Mwangosi? Na kama kuna chuki kati ya polisi na waandishi wa habari, chuki hii itamalizika vipi?

Siamini kama chuki hii itamalizika kwa kuutunza uongo na kuuficha ukweli. Chuki hii haiwezi kwisha kwa baadhi ya wahariri na waandishi kujipendekeza na kujikomba kwa viongoji wa juu kwenye Jeshi la Polisi. Kuna ulazima wa kufanya utafiti wa kina na kufichua yote yaliyofichika.

Tusiogope, Tunachopigania leo ni kwa ajili ya maisha yetu na watoto wetu kesho. Wengi tutaumia, tutalemaa, tutafungwa na wengine kuuwawa lakini tusitishike tusonge mbele. Hata wazazi wetu walijinyima na bado wengine tunaendele kufanya hivyo ndio maana leo angalau unaweza hata kusoma hii makala.

Takwimu sinaweka wazi kuwa watoto wanaozaliwa kwa siku ni zaidi ya mara mia ya risasi zinazotengenezwa kwa siku, Hatutaisha wote, kuna watakaobaki kuelezea Stori hizi za ukombozi.

Mungu tupe wanahabari moyo wa ujasiri kushinda majaribu……

Mungu Ibariki Tanzania.

WE HAVE NO LEADERS IN AFRICA BUT RULERS – PROFESSOR CHRIS PETER MAINA.

There is no doubt that Africa is very rich in terms of resources, what is missing is patriotic management of this resources. These have been observed by The University of Dar es Salaam professor Chris Peter Maina.

Professor Chris Peter Maina 

The don, who was presenting a paper on ongoing the Tanzania forum on mining, oil and gas held in Dar es Salaam. Likened the country with Nigeria where, despite oil abundance, the country is in dire poverty while leaders enjoy huge wealth.

The forum with the theme “Industries, Sovereignty and Sustainable Development” was organized by Haki Madini, Interfaith Committee on Economic Justice and Integrity and Policy Forum, brought together hundreds of stakeholders from Tanzania, Kenya, Zimbabwe, Ghana and Uganda.

Director from Haki Madini Amani Mustafa from right talking with Chadema MP from Kigoma Kabwe Zitto left  and Semkae Kilonzona from Policy Forum.

He said the most disastrous thing is the confidentiality accorded to the contracts by the government in the country while you can easily access the same on bookshelves in the countries of investors’ origin.

He likened the Buzwagi controversial contract that was signed in London in 2007 to the exclusive land agreement signed between colonial agent Karl Peters and Sultan Mangungu in Tanga in 1885 where the latter unwittingly gave away a very big chunk of land to Germany.

Those in trusted with these resources in most Africa continent have no interest in heart but their own individualism interest. Resources are seems as the means toward political power or personal worth or both.

In the first generation of African leadership one could at least see elements of patriotism and love for the continent. One only needs to closely sturdy leaders like Kwame Nkuruma, Jomo Kenyata and Julius Nyerere to see traces and sense of belonging of love of the continent from this people.

Notwithstanding the alleged mistakes they have made in no way they can be compared to those running the continent today. We no longer have leaders in Africa we have rules, the current rules a largely out to sell the continent and its resources they are all alike civilians and militants worst  of all are military in civilian cloth’s with their pretenses  of democracy. There countries like Tanzania whose leaders had once been in the military have shown that we can only dream for Democracy.

Professor Maina noted that the Constitution does not clearly protect the natural resources as it gives the government a leeway to do anything with the resources, saying the new Constitution should avail citizens with more say in natural resources.

“We are just trustees in this country, all this wealth belongs to the future generation, therefore we need to have a Constitution that blocks greedy leaders from misusing minerals” said the professor.

SPEECH BY MR. ALLY BONDO SAMAJE, THE ACTING COMMISSIONER FOR MINERALS (TANZANIA) DELIVERED AT THE NATIONAL CONFERENCE ON MINERAL, OIL AND GAS SECTOR GOVERNANCE ON 5TH SEPTEMBER, 2012.

The Acting Commissioner for Minerals in the Ministry of Energy and Minerals, Mr Ally Bondo Samaje

BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO PLAZA

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

First and fore most, I wish to thank HakiMadini, Policy Forum and the Interfaith Committee on Economic Justice and Integrity of creation for organizing this very important conference on mineral, oil and gas Governance. I further thank you for allowing me to stand in front of you to give a keynote speech in regard to this event which I believe will provide good opportunity for the participants to share experiences and views in regard to resources extraction.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

Let me start my speech by sharing with you on mining sector. We all experienced mineral exploration boom in 1990s, most of the exploration activities concentrated on gold in particular. This was further facilitated by the establishment of the Mineral Policy of 1997 followed by the enactment of Mining Act of 1998.  This move resulted into the commissioning of large scale gold mines we have today.  However, of recent years we have experienced diversification in mineral exploration from gold to other minerals such as uranium, coal, base metals, Rare Earth Elements (REE) and Platinum Group Metals (PGM).  This has resulted into more discoveries of uranium, nickel and Rare Earth Elements making a possibility of having large scale mines for those minerals. Apart from minerals, Tanzania has also oil and gas potentials.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

Mining sector is supposed to contribute to over 10% of GDP by the year 2025. Currently the contribution of mining sector to GDP is at 3.3% (2011).  However, the 10 years implementation of Mineral Policy of 1997 (1997 to 2007) revealed some challenges which made the country to change the mineral policy. These challenges include the following:

 i.        Low level of integration of the mining industry to the rest of the economy, rendering the mining industry as enclave of its own;

  ii.        Low and slow growing contribution of the sector to the GDP as compared to the growth rate of the sector (sector growth from 7.7% in 1997 to 10.7% in 2007 while sector contribution grew from 1.4 % in 1997 to 2.7% in 2007). The current sector contribution to GDP is 3.3% (2011);

 1. Low level of mineral value addition activities as minerals mined were exported in raw form;

 iv.        Slow development of small scale mining;

   v.        Low capacity to administer mineral sector;

 vi.        Growing conflicts between mining projects and communities living around these projects that are mainly centred on insufficient compensation, relocation and resettlement schemes of communities that were originally artisanal and small scale mining communities before start of the large scale mining projects; and

 1. Growing negative public perception on mining, because of high expectation by the people that mining would provide direct benefits from the development of the mining venture in a shortest possible time.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

 

To respond to the above listed challenges, the Government reviewed the Mineral Policy of 1997 which resulted into the establishment of Mineral Policy of 2009, followed by the enactment of the Mining Act 2010. This process was performed by making sure that the international competitiveness in attracting more investment to our country is maintained, the interests of private sector investment that was already established over this period is safeguarded on the other hand addressing the general public concerns over the management of the nation’s mineral wealth.

 

Apart from the Government remaining as regulator, facilitator, service provider and promoter of private sector investment in the mineral sector it is now made possible under the same policy and legal regime the Government to participate in mining projects. Due to this, efforts are being made to strengthen the State Mining Corporation (STAMICO) to actively engage in mining sector on behalf of the Government.

Currently, STAMICO owns various exploration projects either at 100% ownership (potential for partnership) or under joint venture agreements. Some of the projects are at an advanced stage such as the Buckreef Gold Project located in Geita Region whereby STAMICO owns 45% stake and the balance is owned by private company, Tanzania American International Development Corporation 2000 Limited. Also, STAMICO provides consultancy services and drilling services after acquiring two new drill rigs.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

As already mentioned small scale mining is another area that has been emphasized in mineral policy of 2009. The Government has been trying to address the main challenges hindering the development of small scale mining. Small scale miners are faced by lack of skills, technology, financial resources and modern equipment. The government is establishing a loan scheme under coordination of STAMICO for small scale miners that will involve Tanzania Investment Bank (TIB) and other stakeholders where necessary. This will be a revolving fund in order to be sustainable and allow more small scale miners to access the loan in the long run.

Furthermore, the government will continue to demarcate areas suitable for small scale mining from relinquished areas during renewal of Prospecting Licenses as stipulated under section 15 of the Mining Act 2010. The aim is to formalize small scale operations so that they can easily be financed. However, small scale miners are encouraged to form groups so that they can easily qualify to access financial support from financial institutions or from capital market. We encourage the financial institutions and other stakeholders to support and collaborate with the Government in development of small scale mining.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

The Government will continue increasing its effort in supporting small and medium mining enterprises to make sure that the local content in mining increases. This will increase local participation, local beneficiation and value added as well as strengthening economic linkages. The Government is working proactively to ensure a win-win situation. Benefits from mining should not always be seen in terms of royalties or taxes, but in a wider socio-economic spectrum in which local content (economic linkages) brings more benefits than tax based benefits, which can results into the so called Dutch disease.

The Ministry is implementing the Sustainable Management of Mineral Resources Project, whose main objective is to strengthen the countries capacity to manage the mineral sector through various interventions as stated earlier. Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative is also being implemented at the ministry to ensure more transparency and good governance in the mining and petroleum sectors.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

May I breifly talk on oil and gas activities. Tanzania has so far made discoveries of two natural gas fields, Songo Songo (discovered in 1974) and Mnazi Bay (discovered in 1982). Production of gas from Songo Songo started in July 2004, and is being used for electricity generation as well as for thermal applications in 37 industries in boilers, kilns and furnaces. Plans are underway to supply natural gas for households and vehicles. The Songo Songo gas field is estimated to contain 1.6 (tcf) of natural gas while Mnazi Bay is estimated to stock in excess of 4 tcf. The other 5 discoveries namely Mkuranga, Kiliwani-1, Pweza-1, Chewa-1, and Chaza-1 are under appraisal programmes.The three fields recently discovered by Ophir/BG in the deep water offshore have an estimated potential of 7 trillion cubic feet (tcf).

Through Support and Agreement between Tanzania and China, a 532 km, 36 -inch pipeline will be constructed from Mnazi Bay, Mtwara to Dar es Salaam via Somanga Fungu. The maximum capacity of the pipeline is 286 bcf/year, which is sufficient to meet thermal and electricity demand of up to 3,900 MW.

Presently, more effort is being put on policies and legislations on oil and gas which are at different stages of preparations prior to approval. However, the guiding principles are: the use of resources to create lasting benefits to society; efficient resource management; Transparency and accountability; Competitiveness and productivity; Protection of the environment and conservation of biodiversity; and Co-operation among stakeholders.

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

Let me conclude by saying that, the Government policies on energy and minerals will continue emphasizing on sustainable development and growth in a win-win situation. The minerals and Energy sectors are the key economic sectors in Tanzania. It is important that we increase the socio-economic benefits of these sectors in the country by creating more positive partnerships between Government, Industry and local communities to ensure sustainable development. This requires understanding, transparency, trust and honesty. In this regard, the civil society and other stakeholders have an important role to play.

THANK YOU FOR YOUR KIND ATTENTION

FOB CONTRACTS

F.O.B. CONTRACTS:

Acronym for ‘free on board’; a contract whereby the seller of goods agrees to absorb the costs of delivering the goods to the purchaser’s transporter of choice.

The term FOB is a frequent feature of contracts for the sale of goods, especially when the goods are to be delivered to a foreign destination.

In 1879, a china clay merchant offered to buy clay “at 15s. per ton FOB Fowey”. The merchant went bankrupt after the clay supplier had delivered the clay to the port of Fowey, England, as per the FOB agreement. The case went before Justice Bacon who wrote, in Ex parte Rosevear China, and in an era when land transportation was by horse and cart:

“Delivery free on board (FOB) only means the price shall be that which we stipulate for, and you shall not have to pay for the wagons or carts necessary to carry the clay from the place where it is dug. We will bear all those charges and put it free on board the ship, the name of which you are to furnish.”

In a 1921 case, Colley v Overseas Exporters, Justice McCardle added an essential point of FOB contracts where the FOB is to a vessel:

“It seems clear that in the absence of special agreement the property and risk in goods does not in the case of an f.o.b. contract pass from the seller to the buyer till the goods are actually put on board.”

In contemporary international trade, the term continues with its traditional meaning: the vendor pays for delivery of the goods not just to the port, vessel, train, vehicle or ship of the purchaser’s designation, but also any loading costs. In most contracts, the moment of passing of risk is defined as the moment the goods pass the ship’s rail at the port of loading. For example, reference may be made to “FOB New Orleans” or “FOB Baie-Comeau”.

Over time, and in the context of contractual negotiations, some varieties of FOB are in use, as explained by Yale Law School professor Grant Gilmore in his 1975 book The Law of Admiralty:

“In a shipment FOB, the risk passes to buyer at the FOB point.

“If the contract term is FOB At Seller’s Factory, the buyer bears the risk of loss during transit. The seller completes his performance when he delivers conforming goods to the carrier. The price quoted does not include freight.

“Contrariwise, if the term is FOB Point of Destination, seller bears the risk during transit, completes his performance only by tender at that point, and the price quoted usually includes freight.”

References:

FOR MORE CONSULTATION PLEASE CONTACT:

Stephen Tumaini Mduma
Chief Executive Officer
SEMKO CONSULTANTS LTD
P.O.BOX 12027
Dar es Salaam
Tanzania
+255 713 00 00 96
email;sempaimduma@yahoo.com
Webpage. http://www.facebook.com/pages/Semko-Consultants-LTD/156975847746848

CHAMA CHA WAPIGAPICHA ZA HABARI HAPA NCHINI(PPAT)WATOA TAMKO KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI

TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWAKILISHI CHANNEL TEN IRINGA DAUDI

Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na jamii ya wanahabari nchini, watanzania wote  kutoa pole kwa Familia ya Marehemu Daud Mwangosi na KULAANI mauaji ya kikatili ya Mwandishi Daud Mwangosi wa Channel Ten mkoani Iringa.

Mwangosi ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu ya wanahabari Mkoani Iringa (IPS) alifikwa na umauti Septemba 2, 2012 majira ya saa 10 jioni wakati wa vurugu za Polisi na Wafuasi wa CHADEMA.

PPAT inalaani kwa nguvu zote kitendo hicho cha kinyama na ambacho kimetishia kwa kiwango kikubwa usalama wa waandishi wa habari hasa Wapigapicha kama Mwangosi ambao hutakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupiga picha za matukio mbalimbali.

Polisi ikiwa ni chombo pekee cha usalama wa raia na mali zao wakati wote ilishindwa kuhakikisha Mwandishi, Daud Mwangosi anakuwa salama na kutekeleza wajibu wake vyema.

Ni hao hao Polisi tumewaona katika picha kadhaa wakimshambulia na hatimaye kutawanyika baada ya kufa kwa Mwangosi lakini ajabu tunasikia kupitia taarifa zao kuwa Mwangosi alikuwa wakati akikimbia kutoka upande wa Wananchi.

PPAT inapenda kutoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema na kuwaajibisha Askari wote waliohusika katika tukio lile akiwepo RPC wa mkoa wa Iringa na kisha yeye mwenyewe pia kuwajibika kutokana na mauaji hayo ya kinyama.

PPAT pia inaungana na vyama vyote vya Waandishi wa habari nchini Tanzania katika kutaka uchunguzi huru na wahaki ulio katika uwazi katika kuchunguza kifo cha Mwandishi Mwenzetu Daudi Mwangosi na majibu yake yawekwe hadharani mapema iwezekanavyo .

Pia PPAT inawaunga mkono Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa (IPC) kuwazuia wanachama wake kuandika Habari zozote za Jeshi hilo Mkoani Iringa. PPAT inaomba vyama vyote vya mikoa na Jukwaa la Wahariri TEF kusitisha uandikaji wa habari zozote zinazolihusu Jeshi la Polisi nchini hadi watakapo wawajibisha waliotenda mauaji hayo.

 

IMETOLEWA NA:

 

Mroki Mroki

Katibu Mtendaji PPAT.

TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF) KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI

MWEYEKITI WACHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA (IPC) MAREHEM DAUDI MWANGOSI

UTANGULIZI:

 1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

 2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.

 4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

 5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.

 6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.


MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF


Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:

 1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

 2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

 3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

 4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

 5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

 6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

 7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

 8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

 9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.

IMETOLEWA NA:

NEVILLE MEENA,


KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012