CHAMA CHA WAPIGAPICHA ZA HABARI HAPA NCHINI(PPAT)WATOA TAMKO KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI

TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWAKILISHI CHANNEL TEN IRINGA DAUDI

Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na jamii ya wanahabari nchini, watanzania wote  kutoa pole kwa Familia ya Marehemu Daud Mwangosi na KULAANI mauaji ya kikatili ya Mwandishi Daud Mwangosi wa Channel Ten mkoani Iringa.

Mwangosi ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu ya wanahabari Mkoani Iringa (IPS) alifikwa na umauti Septemba 2, 2012 majira ya saa 10 jioni wakati wa vurugu za Polisi na Wafuasi wa CHADEMA.

PPAT inalaani kwa nguvu zote kitendo hicho cha kinyama na ambacho kimetishia kwa kiwango kikubwa usalama wa waandishi wa habari hasa Wapigapicha kama Mwangosi ambao hutakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupiga picha za matukio mbalimbali.

Polisi ikiwa ni chombo pekee cha usalama wa raia na mali zao wakati wote ilishindwa kuhakikisha Mwandishi, Daud Mwangosi anakuwa salama na kutekeleza wajibu wake vyema.

Ni hao hao Polisi tumewaona katika picha kadhaa wakimshambulia na hatimaye kutawanyika baada ya kufa kwa Mwangosi lakini ajabu tunasikia kupitia taarifa zao kuwa Mwangosi alikuwa wakati akikimbia kutoka upande wa Wananchi.

PPAT inapenda kutoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema na kuwaajibisha Askari wote waliohusika katika tukio lile akiwepo RPC wa mkoa wa Iringa na kisha yeye mwenyewe pia kuwajibika kutokana na mauaji hayo ya kinyama.

PPAT pia inaungana na vyama vyote vya Waandishi wa habari nchini Tanzania katika kutaka uchunguzi huru na wahaki ulio katika uwazi katika kuchunguza kifo cha Mwandishi Mwenzetu Daudi Mwangosi na majibu yake yawekwe hadharani mapema iwezekanavyo .

Pia PPAT inawaunga mkono Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa (IPC) kuwazuia wanachama wake kuandika Habari zozote za Jeshi hilo Mkoani Iringa. PPAT inaomba vyama vyote vya mikoa na Jukwaa la Wahariri TEF kusitisha uandikaji wa habari zozote zinazolihusu Jeshi la Polisi nchini hadi watakapo wawajibisha waliotenda mauaji hayo.

 

IMETOLEWA NA:

 

Mroki Mroki

Katibu Mtendaji PPAT.

Advertisements

3 thoughts on “CHAMA CHA WAPIGAPICHA ZA HABARI HAPA NCHINI(PPAT)WATOA TAMKO KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI

  1. njia rahisi ya kuwafanya polisi kuacha kufanya kazi kama robbot ni kulipiza kisasi kwa familia zao popote zilipo.Hatua hii itawafungua akili kwa kuwa nao wataonja uchungu wa unyama.Kama wanadhani bunduki zao zitawalinda hata wazazi ,wake zao,watoto wao popote walipo basi muda si mrefu kitaeleweka.

Comments are closed.