KATIBA YA WATANZANIA AMBAO HAWAJATAYARISHWA KUIANDIKA

Eric Luwongo Mratibu wa Katiba wa Asasi ya HAKI-MADINI

TANZANIA iko kwenye mchakato wa kuandika historia mpya ya kuwa na Katiba iliyotungwa na kuwashirikishwa wananchi wenyewe, ingawa hatua za awali zinaonyesha kukumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kutoandaliwa kwa wananchi wenyewe.

Ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wa Tanzania hawajatayarishwa vya kutosha kushiriki katika mchakato huo hasa kutokana na ukweli kuwa wengi wa wananchi bado hawaijui katiba iliyopo sasa, hivyo, kushiriki katika mchakato wa mabadiliko ya katiba kuwa ni tatizo kwao.

Eric Luwongo Mratibu wa Katiba wa Asasi ya HAKI-MADINI akiwa katika harakati zake za kuhamasisha umma kushiriki katika mabadiliki ya katiba hiyo mwishoni mwawiki jijini Arusha alibainisha kuwa moja ya changamoto ni sheria mbovu inayosimamia mchakato huo na kuvitaja baadhi ya vifungu kama vilivyo ainishwa kwenye Kazi ya Tume Tangazo la serikali Na. 394 la mwaka 2011 amri ya 2 aya (j)ibara ya 9-(1) na 17-moja mpaka mbili ya sheria mpya ya mabadiliko ya katiba ambayo inawanyanganya  mwananchi hakia ya kujadili baadhi ya mambo kwa madai kuwa ni ya kitaifa.

“Hata sisi waelimishaji kutoka katika Asasi mbalimbali tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubanwa na sheria mpya ya mabadiliko ya katiba hasa ibara ya 17 kifungu kidogo cha tisa ambacho kinatunyima hakia na uhuru wa kuelimisha umma kwa mapana yake” alilalamika Luwongo.

Aidha Luwongo alibainisha  tofauti na sensa ambayo serikali ilionyesha dhamili ya kweli na kutumia nguvu nyingi katika mchakato wake kwa kuyaacha makundi mbalimbali kufikisha elimu na ushawishi wake kwa watanzania zoezi la Katiba mpya linaonekana kupooza kwasababu vya sheria hii ambayo ina milolongo mingi anayopaswa kufuata mwamasishaji ndiyo maana utaona kama vyama vya Upinzani asasi mbalimbali na vyombo vya habari vinasuasua tofauti na sensa.

Kwa kuwanyima uelewa wausika ambao ni watanzania wenyewe je unategemea tutapata kweli katiba ambayo ni ya watanzania alihoji Mwandishi Mwandamizi wa siku nyingi Abiba Suedi.

Awali Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba alinukuliwa kuvionya vyama vya siasa kutoingilia mchakato wa zoezi la ukusanyaji maoni ya Katiba kwa kuwashawishi Wananchi kuzungumza mambo wanayoyataka wao wakati wa zoezi hilo jambo ambalo limepigwa vikali na baadhi ya wanaharakati wakidai kuwa vyama husika vinatimiza wajibu wao kwa wananchi ambayo ni kutoa elimu juu ya mchakato huu.

Advertisements