HATIMA YA ARUSHA KUPATA MBUNGE BADO IKO MIKONONI MWA MAHAKAMA

  • Kesi hiyo ya Lema inagusa hisia za watu wengi ususani mkoa wa Arusha na ndiyo sababu ya kila mara shauri lake linapofika mahakamani umati mkubwa kutiririka kusikiliza mwendelezo wa kesi zakewakiwemo wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema. Nje ya Mahakama, umati wa watu uliokusanyika mahakamani hapo,waliokuwa wamebeba bendera pamoja na matawi ya miti walitawanyika kwa maandamano huku wakiimba kwa sauti. Msafara wa wafuasi wa chadema ulielekea katika ofisi za Mkoa za chama hicho zilizopo Ngarenaro huku Lema akiwataka wananchi kuwa na subira hadi tarehe ya hukumu itakapo tajwa tena.

    • MAELFU WAJITOKEZA KUSIKILIZA KESI HIYO

    • UPANDE WA UTETEZI WADAI KESI IFUTWE BAADA YA MAWAKILI WA LEMA KUWASILISHA HATI YENYE MAPUNGUFU KISHERIA.

    • WAKILI WA SERIKALI ASEMA KOSA SI LA LEMA WALA MAWAKILI WAKE BALI TATIZO NI LA KIMAHAKAMA HIVYO WASIADBIWE KWA KOSA AMBALO SI LAO.

    • MAWAKILI WA LEMA WAN’GAKA NA KUSEMA KAMA HATI YA UKUMU NI BATILI BASI MTEJA WAO BADO NI MBUNGE WA ARUSHA, KWASABABU HAKUNA KILICHOMTENGUA……..

HAYAWI HAYAWI! Ndivyo ilivyo jitokeza siku ya Jumanne ya tarehe 2 Oktoba baada ya wananchi wa jiji la Arusha kushindwa kujiakikishia haki ya kuwa na mbunge katika siku za hivi karibuni kutokana na rufaa ya  aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kushindwa kusikilizwa katika Mahakama kuu kanda ya Arusha kutokana na pingamizi la awali lililowekwa na mawakili wa upande wa utetezi wakidai hati ya mashitaka imekosewa na hivyo hawana kesi ya kujibu.

Baada ya mabishano yaliyochukuwa takribani masaa 6 yaliwalazimisha majaji Salum Massati na Natalia Kimario waliokuwa wanaongozwa na Jaji Mkuu Mohammed Chande Othman kuahirisha kesi hiyo na kuahidi kuipangia tarehe upya.

Awali wakili upande wa utetezi Alute Mughwai katika kuonyesha mapungufu ya hati hiyo ya rufaa alisema “Rufaa ni batili kutokana na tafsiri ya mahakama kuu. Hati ya Rufaa haikubaliani na hukumu. Rejea ukurasa wa 957/958 kifungu cha 14 sheria ya uchaguzi. Mkurugenzi wa uchaguzi azingatie sheria ya uchaguzi. Hati ya Rufaa haija handikwa kama inavyotakiwa na sheria. Na katika hili tumeambatanisha hukumu ya mahakama hii tukufu iliyotolewa mwezi wa tano dhidi ya Gesud Bajuta ambaye alifanya kosa kama hili.”

Umati mkubwa wa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wakiwa nje ya mahakama kuu kanda ya Arusha jana mara baada ya hukumu ya Lema kuhairishwa wakielekea katika ofisi za chadema Mkoa

Kwa upande wa mawakili wanao mwakilisha Lema kupitia kwa Method Kimomogoro ulijibu hoja hizo kwa kusema “Mughawai anasema mwenyewe aliandika barua kuomba hati ya ukumu ambayo haikujibiwa. Kama yake haikujibiwa ya kwetu ingejibiwa vipi? Msomi mwenzangu amesema hakukuwa na wajibu wa kuakikisha taarifa zote zinatunzwa. Wakati kanuni zinamwelekeza hivyo.Waheshimiwa tunaomba muelekeze kama mlivyomwelekeza msomi mwenzangu. Mahakama ilisisitiza kwamba kanuni za mwongozo hazitaathiri muendelezo wa kesi. Kama Hati ya ukumu ni batili basi Mteja wetu bado ni mbunge wa Arusha, kwasababu hakuna kilichomtengua……”

Naye Wakili wa Serikali Bw.Timon Vitalis alisema anawaunga mkono hoja za Kimomogoro za kutaka rufaa hiyo isikilizwe kwani tatizo lililojitokeza kwenye hoja za wakili Mughwai si la Lema wala mawakili wake bali tatizo ni la kimahakama hivyo mkata rufaa asiadhibiwe kwa kosa ambalo si lao.

Alisema mahakama ndio inayopaswa kulalamikiwa katika kasoro zilizojitokeza na si mkata rufaa na kuhusu hoja iliyotolewa na Mughwai kuwa Lema achapwe fimbo kutokana na kasoro hizo aliongeza si sahihi kwani mahakama si sungusungu bali inasimamia na kutoa haki hivyo aliwaomba  majaji hao kuzipuuza pingamizi za kina Mughwai.

Kesi hiyo ya Lema inagusa hisia za watu wengi ususani mkoa wa Arusha na ndiyo sababu ya kila mara shauri lake linapofika mahakamani umati mkubwa kutiririka kusikiliza mwendelezo wa kesi zake wakiwemo wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema.

Nje ya Mahakama, umati wa watu uliokusanyika mahakamani hapo,waliokuwa wamebeba bendera pamoja na matawi ya miti walitawanyika kwa maandamano huku wakiimba kwa sauti.

Msafara wa wafuasi wa chadema ulielekea katika ofisi za Mkoa za chama hicho zilizopo Ngarenaro huku Lema akiwataka wananchi kuwa na subira hadi tarehe ya hukumu itakapo tajwa tena.

Advertisements