Leo ningependa tumwangazie Mtunzi na muimbaji nguli wa fasihi simulizi kwa njia ya nyimbo zenye mahadhi ya ushairi ambayo yanauganisha mapokeo ya zamani na ya sasa, Nguli Mrisho Mpoto hususan katika kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la Chochea Kuni uliotengenezwa  katika studio za DATISHAIZO RECORDS.

Nyimbo yenyewe imetengenezwa kwa kutumia vyombo vichache hili msikilizaji aweze kusikiliza mashairi kwa upesi zaidi. Maadhi ya mirindimo yake ni ya kiafrika ikiandamana na vijisauti vya ndege na hivyo kutoa tswila halisi ya mazingira ya watanzania wengi wa kule pembezoni.

Mrisho Mpoto kama kawaida yake, anasafiri na msikilizaji wake na kumpa taswira halisi ya kile anacho analenga hadhira yake isikie (kuwasilisha). Mashairi yake yamepangika katika hali usika ya kukufanya utafakari kwa kina unapojaribu kuileta katika hali mahalia ya watanzania. Bonyeza kitufe cha kusikiliza wimbo wenyewe huku ukifuatisha mtiririko wa mashairi yake kama yalivyoandikwa hapo chini ya wimbo:

Mwisho kama unaswali au sehemu ambayo ujaelewa tujadili pamoja hili tujaribu kupata ujumbe sahihi wa huyu nguli wa mambo ya ushairi.

downloadbuttons150x40

BONYEZA HAPA UPATE WIMBO HUU

KIITIKIO:

Chocheeni kuni mbichi moto ukolee, Ugali uive mnachotaka kitokee, Alikeni mamluki, wakija wangojee, Mikeka waweke, wanachotaka kitokee, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea, chochea , chochea oooo, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA KWANZA:

Watanzania, mwenda kwao siku zote haogopi giza, Acheni nirudi nyumbani safari imenishinda, nauli zenu nitarudisha. Mtu anatapika nyongo yake, anailamba tena anaangaliwa? Ni sawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele, ayaaaa! Katika misimu minne kwa mwaka, tuongeze msimu mwingine wa tano wakujistusha, Raha ya jamvi siku zote ni viraka viraka, Na dungu, linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu? Eti ooo, imenyesha juzi tu, maji sio mengi, nisubirini kule, Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti, ndio mkawaambia watu wavuke? Mjomba, binaadamu ni kama ganda la kitabu, Mpaka umfungue maandishi, ndio uweze kumuelewa, Eti lilotokea mbali tufanye limepita, na haliwezi kumdhuru mwingine, Kweli! Inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu, Mimi, sidhani kama kujiponya kwa mambo mazito, Tunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa moto, Au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi ya kutumia neno sahau tu, Unawaulizaje watu magongo ya nini, wakati umesema kuna nyoka? Mjomba, wewe si uliwapaka wanja, ngoja wao wakupake pilipili, Halafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga

KIITIKIO:

Chocheeni kuni mbichi moto ukolee, Ugali uive mnachotaka kitokee, Alikeni mamluki, wakija wangojee, Mikeka waweke, wanachotaka kitokee, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea, chochea , chochea oooo Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA PILI:

Mngekuwa mnajua anachokula nyuki, msingethubutu kusema asali ni tamu, Niwashukuru, kwa kufikiri mjini mimi nilifaha niende, Halikuwa wazo baya kwa wakati ule, Maana mlionyesha ukomavu kutoka kwenye shingo kwenda chini na sio juu, Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani, kafungiwa kwa nje? Usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka, Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji unatofautiana, mtaanza kusema nina dharau na matusi, Lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno, Mnawezaje kumfikiria aliyekuwa ndani, kajifungia mwenyewe, funguo anazo mwenyewe, Kalala fo fo fo, asijue hata idadi ya misumari iliyoshikilia mlango wake, Kulipamba jeneza, hakumfanyi aliyekufa kufufuka nyinyi, Kama kusema nimeshasema sana, mwishowe nitakuwa kama mwanasiasa, Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa, Natoa katoni ishirini za sabuni ya unga, aliyekwambia wale wachafu nani? Kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndio mrudi kwa wananchi, Ndugu zangu, tawi kavu, kuanguka wala sio ajabu, Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga, Ninyi chocheeni kuni zilizoloa, maji yapate moto ugali usongwe, wakiwauliza, waambieni huu ni utani hehehe, Hapa kwetu tuna makabila 120, tunataniana, Waliopo hatuwataki, wanaotaka hatuwaamini, Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukijua maana yake, Kwa mfano neno la kitoto, mtoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza, Neno la kitoto, mtoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua, Mtoto akisema babaa, ile ndege yangu, Baba hata kama huna baiskeli, utamwambia ikitua nitakuletea, ndio utaratibu, Lakini maneno ya kitoto, mtu mzima kumwambia mtu mzima mwenzie, kuna walakini, Mimi safari imenishinda, na sitaki tena kuulizwa kwanini

KIITIKIO … hadi mwisho

Mashairi haya ni kama yalivyonukuliwa na M2S Songs Review Unit wakiwa wanausikiliza wimbo wenyewe. Sio mashairi rasmi, kwa maana kutoka kwa mtunzi na muimbaji mwenyewe.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3

Advertisements