KIJIJI CHA SAZA WAIONDOA SERIKALI YAO

  • NI MKATABA WA KUUZA MASALIA YA KIFUSI CHENYE  MIAKA  ZAIDI YA 50.

  • YADAIWA NI MIKATABA YA ZAMANI AMBAYO UTEKELEZAJI WAKE ULICHELEWA

  • DOLA 75,000 ZILIZOLIPWA MWANZO ZADAIWA  KUTOFANYA KAZI  ILIYO KUSUDIWA.

Mikataba mibovu ndiyo sababu iliyopelekea mpaka sasa kijiji cha Saza wilaya ya chunya mkoani Mbeya kukosa uongozi wa kijiji baada ya kuondolewa kwa uongozi uliokuwa madarakani kwa shutma ikiwemo ya kuuzwa kiolela kwa kifusi cha masalia ya makapi (mchanga ambao ulisha chenguliwa) kwa kampuni ya kigeni ya wawekezaji ya Shanta Gold Mine.

Kifusi hicho ni mkusanyiko wa mchanga ambao ulikuwa unachenguliwa (kutolewa dhaabu kwa mara ya kwanza) nyakati za enzi za ukoloni (Tanganyika). Kutokana na teknolojia ya zamani inasadikiwa kifusi hicho bado kina dhahabu ambayo inaghalimu zaidi ya mabilioni ya dola za kimarekani.

Taharifa za uhakika kutoka kijijini hapo zinasema mikataba hiyo ni ya muda mrefu ambapo makubaliano yaliwataka wawekezaji kutoa kiasi cha dola 75,000 kama malipo ya kufanya tathimini na walipo ridhia wakataka kulipa kiasi cha dola 250,000.

Changamoto kubwa  inaonyesha kuwa  wananchi hawakupewa nafasi ya kushiriki zoezi hilo  tokea mwanzo jambo ambalo lilipelekea wao kuiondoa serikali yao ya kijiji kwa kutokuwa na imani nayo. Tofauti na mikataba hiyo vilevile ni kushindwa kwa serikali hiyo kurejesha matumiza ya dola 75,000 ambazo zililipwa hapo awali na muwekezaji huyo.

 

WAANDISHI, WANAKIJIJI CHA SAZA PAMOJA NA TIMU YA UCHECHEMUAJI NA UZENGEZI YA HAKIMADINI WAKIWA KATIKA MLIMA SAZA AMBAO NI MASALIA YA KIFUSI CHENYE DHAABU KINACHODAIWA KUUZWA KWA MWEKEZAJI KWA BEI NDOGO.

WAANDISHI, WANAKIJIJI CHA SAZA PAMOJA NA TIMU YA UCHECHEMUAJI NA UZENGEZI YA HAKIMADINI WAKIWA KATIKA MLIMA SAZA AMBAO NI MASALIA YA KIFUSI CHENYE DHAABU KINACHODAIWA KUUZWA KWA MWEKEZAJI KWA BEI NDOGO.

 

WAANDISHI PAMOJA NA TIMU YA UCHECHEMUAJI NA UZENGEZI YA HAKIMADINI WAKIWA KATIKA MLIMA SAZA AMBAO NI MASALIA YA KIFUSI CHENYE DHAABU KINACHODAIWA KUUZWA KWA MWEKEZAJI KWA BEI NDOGO.

Advertisements