ZANZIBAR YAINGIA KWA VITENDO KWENYE MFUMO WA DIGITALI KUPITIA MLADI WAKE MPYA WA E-GOVERNMENT

Afisa Usalama wa Mradi wa E-Governmet Ali Mohamed Khitu akimfahamisha Rais Shein mchoro unaoonesha jinsi Waya wa Mradi huo ulivyosambazwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba na kuwawezesha kugundua uharibifu popote pale utakapotokea.

Balozi  wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing akimkabidhi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa E-Government ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa mradi wa E-Government Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa katika picha ya pamoja na Maofisa mbali mbali katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa E-Government ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.(Picha zote kwa hisani ya Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

                  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed amesema Uzinduzi wa Mradi wa Serikali wa mawasiliano ya digitali ya kimtandao E-Government umefungua ukurasa mpya katika uendeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na utekelezwaji wake utaakisi lengo kuu la Mapinduzi ya Zanzibar la kuwakomboa Wananchi kimawazo na kiuchumi.

Lengo la Mradi wa E-Government ni kuiwezesha Serikali kuendesha shughuli zake kwa njia za kitaalamu zaidi na kuhakikisha kuwa kila mwananchi popote alipo anapata huduma au taarifa muhimu zinazotolewa na Serikali kupitia mitandao mbalimbali inayopatikana nchi nzima na ambayo imeunganishwa na E-Government.

Faida za mradi huu ni pamoja na kuchochea matumizi ya Teknologia ya habari na Mawasilino nchini ikiwa ni pamoja na kukuza Elimu katika Shule za Msingi na Sekondari kwa kupitia Mradi wa T21.

Mradi wa E-Government umeznduliwa kiwa ni moja ya shamra shamra za Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar umeigharimu Dola Milion 19 za kimarekani ambazo ni Mkopo nafuu kutoka nchi ya China.

hakimadini 001

Advertisements