MABILONI YA MFUKO WA LOWASSA YAONGEA, SAFARI HII NI WANAKIKUNDI CHA VIKOBA MONDULI

Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.

 

Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa.

 

Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa.

 

Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ameanza mwaka kwa kutembeza ma bilioni yake safari hii waliyo bahatika ni vikundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli, tunu hii ya kiasi cha shilingi milioni nane ni kwa ajili ya kuendeleza shughuli za vikundi hivyo. Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi millioni moja zaidi.

hakimadini 001

Advertisements