MADAKTARI SASA LAWAMANI KWA KUKWAMISHA UCHUNGUZI WA KIFO CHENYE UTATA CHA MWANAFUNZI HOTELINI DAR.

MWANAFUNZI

Ndugu na Jamaa wa marehemu Jacqueline Matiko wakijaribu kuhusitili mwili wa marehemu

  • Mpaka sasa washindwa kuwasilisha ripoti yao ingawa walitoa haadi ya kufanya hivyo toka ijumaa 4 Jan 2013.

  • Habari za awali zinadai uchunguzi wa madaktari ulikamili toka ijumaa 4 Jan 2013.

  • Utata wa kifo cha mwanafunzi huyo ni kutofautiana kwa wafanyakazi wa Hoteli ya Southern Beach kudai marehemu mauti yalimfika kwasababu ya kuzama kwenye bwawa na familia yake kutokukubaliana na taarifa hiyo.

SHUTUMA za ucheleweshwaji wa upepelezi wa kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi Jacqueline Matiko, ambaye mwili wake ulikutwa pembeni mwa bwawa la kuogelea katika Hoteli ya Southern Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa Mwaka 2013 zinaelekezwa kwa madaktari wa Muimbili kwa kuchelewesha ripoti itakayo thibitisha sababu ya kifo hicho.

Taharifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engerbelt Kiondo inadai kuwa madaktari wa Muhimbili hawajawasilisha ripoti yao ya uchunguzi wa mwili wa mwanafunzi huyo kinyume na haadi yao ya kufanya hivyo tokea ijumaa 4 Jan 2013.

“Mwili wameshaufanyia uchunguzi na tunawasubiri madaktari watupatie ripoti ili tuanze upelelezi lakini hadi sasa hawajafanya hivyo” alibainisha Kiondo.

Marehemu Jacqueline inadaiwa alikwenda katika hoteli hiyo kwa mapumziko ya sikukuu ya Mwaka Mpya, lakini alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na baadaye mwili wake ulikutwa pembeni mwa bwawa la kuongelea.

Utata kuhusu kifo hicho unatokana na madai ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwa marehemu alikufa maji.

Hata hivyo ndugu zake wanadai kuwa madai hayo si ya kweli kwasababu baada ya kutoweka kwake walifanya jitihada za kuutafuta mwili huo mpaka kwenye bwawa hilo lakini hawakuupata.

hakimadini sera

Advertisements