arusha

  • Wilaya zenye migogoro ni Monduli, Longido na Arumeru.

  • Migogoro hiyo yaofiwa kusababisha mapigano ya kikabila

  • Lowassa awashanga viongozi wa serikali ya mkoani Arusha kushindwa kutatua ilihali mipaka na ramani zipo.

  • Mkuu wa Mkoa wa Arusha asema tahadhari zinaitajika ili kumaliza migogoro badala ya kuchochea.

Migogoro ya mipaka ya wilaya za Monduli, Longido na Arumeru mkoani Arusha imeendelea na inadaiwa hivi karibuni ilisababisha mapigano ya kikabila.

Hatua hiyo iliwalazimu wajumbe walio hudhuri katika kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Arusha kuifanya migogoro hiyo kuwa moja ya agenda zao. Wajumbe mbali mbali waliopata fulsa ya kulijadili swala hilo akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Yeye alishauri viongozi wa serikali ya Mkoa wa Arusha kutoa kwa wakati uamuzi wa kusuluhisha migogoro ya mipaka baina ya wilaya hizo.

“Kinachopaswa kufanyika ni kutangazwa mipaka tu, mkuu wa mkoa usiofu, katangaze mipaka  kwani ramani zipo, ni bora kuchukuwa tahadhari na usiwe mwoga,” alinukuliwa Lowassa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema migogoro ya ardhi katika wilaya hizo inapaswa kutatuliwa kwa tahadhari kwani kuna uamuzi mwingine unaweza kuchochea migogoro badala ya kusuruhisha.

hakimadini sera

Advertisements