map-chunya

  • Chunya ni moja ya wilaya zenye madini ya dhahabu ambapo uvunaji wake unategemea madini ya zebaki.

  • Uchunguzi wa asasi ya Agenda umebainisha kiwango kikubwa cha madini ya zebaki kinachosadikiwa kuwepo kwenye maeneo yamakazi ya watu.

ASASI isiyo ya kiserikali ya Agenda inayojihusisha na mazingira na maendeleo ya watu imetoa ripoti yake ya utafiti inayoonyesha wakazi wa vijiji vya Matundasi na Makongolosi Wilayani Chunya mkoani Mbeya wapo katika hatari ya kupata matatizo ya ubongo na figo.

Afisa miradi wa Agenda, Haji Rehani alisema madhara kwa wananchi hao yanatokana na kiwango kikubwa cha madini ya zebaki kilichopo kwenye maeneo wanayoishi.

Alisema utafiti wao unaonyesha kiwango cha ZEBAKI kilichopita viwango vya kamataifa kinacho ruhusiwa kuwepo kwenye maeneo ya makazi ya binadamu bila kuleta madhara ya kiafya.

hakimadini sera

Advertisements