CAG AWAKAANGA VIGOGO WA TANESCO

The Controller and Auditor General (CAG), Mr Ludovick Utouh

The Controller and Auditor General (CAG), Mr Ludovick Utouh

  • Ripoti imekamilika na kubaini madudu.

  • Yaonyesha kuna kasoro katika ununuzi kwa kutofuata utaratibu na ubadilishaji wa fedha za kigeni(Dola) katka benki ambazo shirika halina akauti.

  • Pamoja na ripoti ya CAG kubaini makosa ya William Mhando hawawezi kumshtaki mahakamani

HITIMISHO la sakata la vigogo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), litajulikana mwishoni mwa mwezi huu baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kukamilika na kuonyesha tuhuma nzito dhidi ya maofisa watatu wa shirika hilo.

Maofisa hao ambao kwasasa wanasubiri uamuzi wa bodi ya TANESCO ni pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi Harun Mattambo.

Maofisa hao walisimamishwa kazi julai 14 mwaka 2012 sambamba na aliyekuwa mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando, ambaye baadaye alifukuzwa kazi.

Akizungumza na gazeti moja la kila siku Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO Jenerali Mstaafu Robert Mboma alisema kazi ya kuwachunguza maofisa hao iliyokuwa ikifanywa na CAG imekamilika na wamepewa ripoti inayoonyesha kasoro kadha.

“Awali CAG alileta taarifa ambayo tuliikataa na kumtaka airekebishe. Hii ya sasa tumeikubali na kuielewa, kikubwa alichogundua ni manunuzi yasiyofuata utaratibu na suala la kubadilishwa kwa fedha za kigeni (Dola) katika benki ambazo Shirika halina akaunti,” alisema Mboma.

Aliongeza baada ya jopo la wakurugenzi kumaliza kuwahoji watuhumiwa hao, litawasilisha mapendekezo kwa bodi ambayo itatoa uamuzi wake.

Uchunguzi uliofanywa na M2S uligundua kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando hawezi kushtakiwa mahakamani kwa sababu makosa aliyoyafanya ya kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi ni makosa ya kiuadilifu na hayawezi kufunguliwa mashitaka.

hakimadini sera

Advertisements