FILAMU YA ULIMBOKA YAENDELEA, YAMTAJA BALOZI WA KENYA YEYE ASEMA MPAKA AJILIZISHE.

JOSHUA MULUNDI

Mtuhumiwa katika kesi ya Dk. Ulimboka Joshua Mulundi kisindikizwa na Polisi Kutokea katika Mahakama ya Kisutu mwishoni mwa wiki.

  • Mshtakiwa aomba mahakama imuite balozi wa Kenya Mahakamani.

  • Balozi asema mpaka ajilizishe kwanza kama Mulundi kweli ni raia wa Kenya.

  • Ni baada ya wakili wa serikali kudai upelelezi wake bado ujakamilika.

  • Hakimu ajitetea kuwa hana uwezo wa kuwaamuru polisi kuharakisha upelelezi.

Katika kile kisa kilichogeuka na kufananishwa na mchezo wa kuigiza machoni mwa watanzania wengi cha kutekwa na kutaka kuuwawa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka na baadae kujitokeza kwa mtu na kudai kufanya jaribiyo hilo huku polisi wakijilizisha kuwa wamempata mshitakiwa wao bila kujiuliza maswali  limechukuwa sura mpya bahata ya mshtakiwa Joshua Mulundi, kuonyesha kutolizishwa na mwenendo wa kesi yake na kumtaka balozi wa Kenya hapa nchini kwenda mahakamani.

Mhinda anayedaiwa kuwa ni raia wa Kenya, alitoa ombi hilo siku ya Alhamisi 10 Jan, 2013 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam, Agnes Mchome.

Hatua hiyo ilitokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na himekuja kwa ajili ya kutajwa tu.

Hata hivyo hakimu Mchome alimwambia mshtakiwa kuwa yeye hana uwezo wa kuwaamuru polisi kuutaka upande wa mashtaka kufuatilia suala hilo.

“Mahakama haina uwezo wa kumwita balozi wako, kama unataka fuata utaratibu kwa kumwandikia barua ili apelekewe,” alisema Hakimu Mchome.

Hatua hiyo ilionyesha kumkera mshtakiwa na kuomba kuonana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, IIvin Mugeta ili aweze kumweleza malalamika yake.

Balozi wa kenya hapa Nchini alipo ulizwa kuhusiana na Kesi hii alidai kuwa yeye hanataharifa kama Mshitakiwa ni raia wa Kenya na hivyo kuomba kujilizisha kwanza kabla ya kujiusisha na sakata hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 23, 2013.

hakimadini sera

Advertisements