RAIS WA AWAMU YA PILI ALIFANYA BIASHARA YA KUNUNUA NYUMBA ZA MAMILIONI NA KUPANGISHA; MZOMBE.

Rais Mwinyi

  • Nyumba tulizo nunua ni za maeneo ya Mikocheni, Msasani ambazo ziligarimu mamilioni ya shilingi.

  • Ununuzi wa nyumba hizo ulikuwa ni wa siri kubwa baina yetu sisi wawili.

  • Mzombe anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa kuaminiwaakiwa wa Sh. 37.44 akiwa ni wakala wa kukusanya  malipo ya kodi za pango la nyumba zinayo milikiwa na mzee mwinyi kabla ya kutoweka nazo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu siku ya Ahamisi 10 Jan 2013 ilistushwa na utetezi wa Mshtakiwa Abdallah Mzombe anayekabiliwa na kesi ya kumuibia Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kiasi cha Sh. 37.44 milioni baada ya mshtakiwa huyo kuibua shutuma za biashara ya ununuzi na upangishaji nyumba ya rais huyo mstahafu wakati akiwa madarakani.

Wananchi wa wastani walio jitokeza kusikiliza kesi hiyo walishuhudia mshtakiwa Mzombe akianza utetezi wake kwa kudai kuwa Rais wa awamu ya pili Mwinyi alimfungulia kesi hiyo ili kukwepa kutimiza ahadi aliyoitoa kwake ya kumjengea nyumba.

Akiendelea kujitetea dhidi ya mashtaka yanayomkabili, mshtakiwa huyo alidai kuwa Rais Mwinyi alitoa ahadi hiyo ya kumjengea nyumba wakati walipokuwa kwenye mazungumzo yao ya kawaida.

Mzombe alisema katika utetezi wake kuwa yeye na Mwinyi kwa muda mrefu walikuwa na uhusiano mzuri hadi akafikia kutumwa katika kazi zake zenye usiri mkubwa na kuhusisha fedha nyingi japo alilipwa ujira mdogo, alitabainisha kwa majonzi.

Mshtakiwa aliwastua wananchi waliofika mahakamani Kisutu alipo zitaja miongani mwa kazi alizokuwa akimfanyia Rais huyo Mstaafu ikiwamo ya kumtafutia nyumba alizokuwa akinunua maeneo ya Mikocheni, Msasani na kuzifanyia matengenezo kabla ya kuwaweka wapangaji.

Duru za uchunguzi zilibaini kuwa madai ya Mstakiwa yalionyesha kuwa nyumba hizo zilikuwa zenye thamani kubwa lakini akubainisha idadi yake pamoja na chanzo cha fedha ambazo alikuwa anapewa na Rais huyo Mstaafu.

Kama ikithibitika kuwa Rais huyo wa awamu ya pili alikuwa akifanya biashara hizo wakati wa utawala wake, hatua hiyo itahipa nguvu hoja ya Baba wa taifa ya wakati huo kuwa Ikulu ilikuwa imegeuzwa na kuwa pango la walanguzi.

hakimadini sera

Advertisements