UNGANA NASI KUFWATILIA UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI WA KENYA, LIVE KAMA TUNAVYO PATA TAHARIFA BILA CHENGA

m2s breaking news

16:27 :Sehemu nyingi za starehe na ulevi mjini Nyeri Mkoa wa Kati zimefungwa na zitafunguliwa Jumanne ili kuwaruhusu wapiga kura kupiga kura. Eneo la Mkoa wa Kati lina tatizo la uraibu wa pombe

16:24: Ng’endo Angela ambaye yuko Mooa wa Kati ansema kuwa kuwa sababu ya hitilafi za kimitambo, tume imelazimika kutumia mfumo wa kawaida kwa kutumia daftari za wapiga kura. Ni Nyeri peke yake ambako shughuli hiyo ilifanikiwa kwa njia ya Elktroniki

15:54 Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kuwa foleni mjini Nakuru zimeanza kupungua na huenda wapiga kura wakamaliza shughuli hiyo itimiapo saa kumi na moja jioni muda wa mwisho wa kupiga kura


15:16 Mmoja wa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta ameelezea maskitiko yake kuhusu yaliyojiri Mombasa ambako washukiwa wa kundi la MRC waliwaua polisi na raia katika mashambulizi usiku wa kuamkia leo. Lengo lao lilikuwa kuvuruga shughuli ya uchaguzi

14:57 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu Ann Mawathe anasema milolongo ya watu imepungua sana katika sehemu nyingi za mji huo ikizingatiwa kuwa asubuhi watu walikuwa wamejaa pomoni


14:51 Kuna taarifa kuwa magari ya Abiria yameanza kuongeza nauli ya magari kwa sababu ya upungufu wa magari hayo wakati wakenya wakiwa wamejitokeza kupiga kura

Mpigaji kura mjini Mombasa

13:33 Tume ya uchaguzi imeagiza uachaguzi kurejelewa katika wodi tano kati ya zote 1’450 ambako mitambo ya tume hiyo ilikumbwa na hitilafu pamoja na makosa kwenye karatasi za kupigia kura

13:31 Katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa, taarifa zinasema kuwa watu wanaonekana kukata tamaa na wameamua kurejea nyumbani kwani foleni hazisongi


13:24 Mwandishi wa BBC Wanyama wa Chebusire anaripoti kuwa gari la mbunge mmoja wa zamani limeteketezwa moto maeneo ya Kakamega na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa mpinzani wake. hakuna taharifa za mahafa yoyote.

11:25 Mkuu wa Polisi David Kimaiyo asema kuwa takriban wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa Republican Council walivamia kituo cha polisi wa doria wakiwa wanaelekea kusambaratisha shughuli za kupiga kura. Inaarifiwa polisi wanne waliuawa katika makabiliano kati yao na wanachama hao.

11:14 Mgombea wa urais Uhuru Kenyatta anapiga kura yake katika eneo bunge lake la Gatundu , mkoa wa Kati


Milolongo mirefu ilishuhudiwa kote nchini

10:39 Mwandishi wa BBC aliye mjini Nyeri Ng’endo Angela anasema kila baada ya nyumba kumi kuna kituo cha kupigia kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi, baadhi ya mashine za tume ya uchaguzi zilishindwa kufanya kazi lakini baada ya kushughulikiwa mambo yakarejea kuwa sawa.

10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama wa Chebusire amesema vituo vilifunguliwa mapema, na mambo yameenda shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil kidogo, mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga


10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto inazokabiliwa nazo tume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa, vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura


10:22: Ingawaje tume ya uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu katika kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wa BBC Ann Mawathe ameshuudia dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na wapiga kura wenzake.

Katika kituo hicho hicho, baba fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni, naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.


Karani katika kituo cha kupigia kura

09:04 Waziri mkuu Raila Odinga ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera. Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa shwari

08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa


08:30 Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12

08:25 Hassan Majid mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa na panga katika eneo la Mishomoroni, taharifa hii aijajulikana kama inausiana na uchaguzi unao endelea hadi sasa.


08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen ametupa taharifa za kusikitisha pale alipotujuzakuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa zaidi kwa sasa

Mama mwenye mtoto alijitokeza mapema na hapa anaonekana amefanikiwa kupiga kura.

08:16: Frawaso Kimutai  yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru. kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe


08:15: Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina. hadi mida ya saa moja asubuhii, shughuli ya upigaji kura ilikuwa haijaanza


07:24 Kips Oscar: Kupitia Facebook yuko Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi

Kwa upande wa usalama, polisi na wanajeshi wanaonekana kudhibiti shehemu kubwa ya nchi ya Kenya. Magari ya Kijeshi yakiwemo madelaya ya kivita yalionekana yakishika dolia toka mapema asubuhi ya leo wakati upigaji kura ulipoanza

07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret


07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.

07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao


07:47 Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Watu walianza kupanga Foleni kuanzia saa tisa usiku, hii ni mara ya kwanza kwa wakenya kujitokeza kwa wingi kama hilivyo shuhudiwa leo hii.

07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa na hamasa ya kupiga kura. Wamepanga foleni tangu saa nane usiku.


07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao

Advertisements