AFRICAN BARRICK GOLD KUTENGA DOLA MILIONI 10 KILA MWAKA KWA AJILI YA UWEKEZAJI

Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG Greg Hawkins akizungumzia Mfuko wa Maendeleo wa ABG amesema mpaka sasa mfuko huo umewekeza dola za Marekani milioni 2.2 (zaidi ya shilingi bilioni 3.6) kusaidia kuboresha afya ya umma kwenye jamii zinazo zunguka migodi yake.

Amesema kwa upande wa elimu, Mfuko umetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 1.9 (takriban shilingi bilioni 3) kuwekeza kwenye sekta muhimu na kuwa uwekezaji wa mfuko huo umesaidia kujenga shule mpya na kuongeza idadi ya madarasa kwenye shule nyingine ili kuwapa watoto wengi zaidi fursa ya kupata elimu bora.

Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika (kulia) amesema lengo kubwa la kuwepo kwa mfuko huo ni kutaka kuhakikisha jamii iliyozunguka migodi hiyo inafaidika na kuwa lmtazamo bado uko katika masuala muhimu kama elimu, masuala ya maji, masuala ya afya na kwa kiasi Fulani masuala ya miundo mbinu.

Akizungumzia mgodi wa North Mara uliopo wilaya ya Tarime, amesema Mfuko umewekeza dola za Marekani 800,000 (sawa na shilingi bilioni 1.3) kwa ajili ya kuchimba visima vya maji ili kuwasaidia wananchi wapate maji safi na salama ya kunywa.

Corporate Manager – community Relations Steve Kisakye (wa pili kulia) akifafanua jinsi Mfuko huo unavyoweza kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali, ambapo ili kuboresha maisha ya jamii zinazozunguka migodi hiyo minne, Mfuko wa Maendeleo wa ABG umeweka dola za Marekani milioni 1.4 (zaidi ya shilingi bilioni 2) kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.

Mfuko wa Maendeleo wa African Barrick Golg ulioanzishwa mnamo Septemba 2011 umeweza kusimamia uwekezaji wa kampuni ya ABG kwenye jamii katika kipindi cha miezi 18 iliyopita na kufanikiwa kutekeleza zaidi ya miradi 50 yenye thamani ya dola za marekani milioni 7.5 (takriban shilingi bilioni 12) katika kipindi cha mwaka 2011/2012.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam  leo Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG Greg Hawkins amesema wanafurahi kuona mafanikio makubwa ambayo Mfuko wa maendeleo wa ABG umeyapata kwenye kipindi cha miezi 18 mpaka sasa.

Ameongeza kuwa walianzisha Mfuko huo kama sehemu ya jitihada zao za kuchangia kwenye maendeleo endelevu nchini Tanzania na tayari mafanikio makubwa yameonekana kwenye zaidi ya miradi 50.

Mfuko wa Maendeleo wa AGB unashirikiana na jamii husika kubaishinisha vipau mbele vyao ili wanajamii wenyewe wawe mstari wa mbele kwenye utekelezaji wa miradi.

Kampuni ya ABG inalipa gharama zote za uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo wa ABG ili kuhakikisha kuwa asilimia kuwa asilimia 100 ya fedha za Mfuko huo zinaenda moja kwa moja kwenye miradi ya jamii.

Advertisements